Sura ya 40 Samueli Mlamani Anazungumza Kuhusu Yesu Kristo Walamani walitii amri za Mungu. Walikuwa wenye haki zaidi kuliko Wanefi. Helamani 13:1 Samueli, nabii wa Kilamani, alikwenda Zarahemla kuhubiri kwa Wanefi waovu. Aliwaambia watubu. Helamani 13:2 Wanefi walimfukuza Samueli nje ya mji, na akaanza kurudi katika nchi yake. Helamani 13:2 Lakini Bwana alimwambia Samueli arudi Zarahemla na kuwaambia watu vitu ambavyo Bwana aliviweka katika moyo wake. Helamani 13:3 Wanefi hawakumruhusu Samueli kurudi kwenye mji, hivyo alipanda juu ya ukuta wa mji na kuhubiri kutokea pale. Helamani 13:4 Alitoa unabii kwamba Wanefi wangeangamizwa ndani ya miaka 400 isipokuwa watu watubu na kuwa na imani katika Yesu Kristo. Helamani 13:5–6 Samweli aliwaambia Wanefi kwamba Yesu Kristo angezaliwa ndani ya miaka mia tano na kwamba angewaokoa wale wote waliomwamini. Helamani 14:2 Samueli aliwaambia kuhusu ishara ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Nyota mpya ingetokea, na usiku kabla ya Yesu kuzaliwa kusingekuwa na giza. Helamani 14:3–5 Kisha Samueli aliwaambia ishara ya kifo cha Yesu. Kungekuwa na siku tatu za giza totoro—jua, mwezi na nyota havingetoa nuru. Helamani 14:20 Pia kungekuwa na ngurumo na radi na matetemeko ya nchi. Milima ingeanguka, na miji mingi ingeharibiwa. Helamani 14:21–24 Baadhi ya Wanefi walimwamini Samueli na wakatubu dhambi zao. Walikwenda kumtafuta Nefi, Mnefi mwenye haki ambaye angewabatiza. Helamani 16:1 Wanefi waliobaki hawakumwamini Samueli. Walimrushia mawe na mishale. Lakini Bwana alimlinda, na hakuna kati ya jiwe au mshale ulimpiga. Helamani 16:2 Watu walipoona kwamba hawezi kupigwa, wengi wao walimwamini na wakaenda kwa Nefi kubatizwa. Helamani 16:3 Nefi pia aliwafundisha watu kuhusu Yesu. Alitaka wao wamwamini Yesu, watubu na kubatizwa. Helamani 16:4–5 Wengi wa Wanefi, hata hivyo, hawakumwamini Samueli. Walijaribu kumkamata. Helamani 16:6 Samueli aliruka chini kutoka ukutani na kukimbia katika nchi yake. Helamani 16:7 Samueli alinza kuwafundisha Walamani. Hakusikika tena kati ya Wanefi. Helamani 16:7–8