Sura ya 9 Makao mapya katika Nchi ya ahadi Merikebu iliyowabeba Lehi na familia yake ilivuka bahari na kufika kwenye nchi ya ahadi. Watu wanaweka hema. 1 Nefi 18:23 Waliandaa udongo na kupanda mbegu walizokuja nazo. 1 Nefi 18:24 Wakati wakitembea kuzunguka nchi mpya, walikuta wanyama wa aina nyingi. Pia walikuta dhahabu, fedha, na shaba. 1 Nefi 18:25 Mungu alimwambia Nefi kutengeneza bamba za madini na kuandika juu yake. Nefi aliandika kuhusu familia yake na safari zao. Aliandika maneno ya Mungu. 1 Nefi 19:1, 3 Lehi alizeeka. Kabla hajafa aliongea na wanawe na kuwambia kuwa watii amri za Mungu. Pia aliwabariki wajukuu zake. 2 Nefi 1:14, 16; 4:3–11 Baada ya Lehi kufariki Lamani na Lemueli walipata hasira juu ya Nefi na wakataka kumuua. Hawakutaka Nefi, kaka yao mdogo, kuwa kiongozi wao. 2 Nefi 4:13; 5:2–3 Bwana alimwambia Nefi kuwaongoza watu walio wema kwenda nyikani. Walisafiri kwa siku nyingi na hatimaye walisimama kwenye nchi walioyoiita Nefi. 2 Nefi 5:5–8 Watu waliomfuata Nefi walimtii Mungu. Walifanya kazi kwa bidii na walibarikiwa. Nefi aliwafundisha watu wake kujenga kwa kutumia mbao na chuma. Walijenga hekalu zuri. 2 Nefi 5:10–11, 15–16 Wafuasi wa Lamani na Lamueli waliitwa Walamani. 2 Nefi 5:14 Walamani hawakumtii Mungu na waliondolewa kutoka kwenye uwepo Wake. Roho wa Bwana asingeweza kuwa pamoja nao mpaka watubu. 2 Nefi 5:20; Etheri 2:15 Walamani walijawa na fitina na mara kwa mara walipigana na Wanefi. 2 Nefi 5:24, 34