Sura ya 38 Mauaji ya Mwamuzi Mkuu Watu waovu walikuwa waamuzi juu ya Wanefi. Waliwaadhibu watu wenye haki lakini si waovu. Helamani 7:4–5 Nefi alikuwa na huzuni kuona uovu mwingi miongoni mwa watu. Helamani 7:6–7 Siku moja alikuwa akisali katika mnara kwenye bustani yake. Bustani yake ilikuwa pembezoni mwa barabara iliyokuwa ikielekea katika soko la Zarahemla. Helamani 7:10 Watu waliopita barabarani walimsikia Nefi akisali. Kundi kubwa lilikusanyika, likishangaa kwa nini alikuwa mwenye huzuni. Helamani 7:11 Wakati Nefi alipoona watu, aliwaambia alikuwa na huzuni kwa sababu ya uovu wao. Aliwaambia watubu. Helamani 7:12–14, 17 Aliwaonya kwamba kama hawangetubu, maadui wao wangechukua nyumba zao na miji yao na Bwana hangewasaidia kupigana na adui zao. Helamani 7:22 Nefi alisema Wanefi walikuwa waovu zaidi kuliko Walamani kwa sababu Wanefi walikuwa wamefundishwa amri lakini walikuwa hawazitii. Helamani 7:24 Alisema kama Wanefi hawangetubu, wangeharibiwa. Helamani 7:28 Baadhi ya waamuzi waovu walikuwepo pale. Walitaka watu wamwadhibu Nefi kwa kuongea dhidi yao na sheria yao. Helamani 8:1–4 Baadhi ya watu walikubaliana na waamuzi waovu. Wengine walimwamini Nefi; walijua alikuwa nabii na aliongea ukweli. Helamani 8:7–9 Nefi aliwaambia watu kwamba walikuwa wameasi dhidi ya Mungu na karibuni wangeadhibiwa kama hawangetubu. Helamani 8:25–26 Nefi aliwaambia watu kwenda kwa mwamuzi wao mkuu. Angekuwa amelala chini kwenye damu yake mwenyewe, akiwa ameuwawa na kaka yake aliyetaka nafasi yake. Helamani 8:27 Wanaume watano kutoka kwenye umati walikimbia kwenda kumuona mwamuzi mkuu. Hawakuamini kwamba Nefi alikuwa ni nabii wa Mungu. Helamani 9:1–2 Wakati walipomwona Seezoramu, mwamuzi mkuu, amelala kwenye damu yake, walianguka ardhini kwa woga. Sasa walijua kwamba Nefi alikuwa nabii. Helamani 9:3–5 Watumishi wa Seezoramu walikuwa tayari wamemuona Seezoramu na walikimbia kuwaambia watu. Walirudi na kuwakuta wanaume watano wakiwa wameanguka hapo. Helamani 9:6–7 Watu walifikiri wale watu watano ndio waliomuua Seezoramu. Helamani 9:8 Waliwatupa gerezani na kutuma waraka kote kwenye mji kwamba mwamuzi mkuu alikuwa amuwawa na kwamba wauwaji walikuwa gerezani. Helamani 9:9 Siku iliyofuata watu walikwenda sehemu ambapo mwamuzi mkuu angezikwa. Waamuzi waliokuwa na Nefi bustanini waliulizia wapi walipokuwepo wale wanaume watano. Helamani 9:10–12 Waamuzi waliomba kuwaona watuhumiwa wa mauaji. Helamani 9:13 Watuhumiwa walikuwa ni wale watano ambao walikimbia kutoka bustani ya Nefi kwenda kwa mwamuzi mkuu. Helamani 9:13 Wale watu watano walisema walimkuta mwamuzi mkuu amelala kwenye damu, kama Nefi alivyosema. Kisha waamuzi walimtuhumu Nefi kwa kumtuma mtu kumuua Seezoramu. Helamani 9:15–16 Kwa kujua kwamba Nefi alikuwa nabii, wale watano walibishana na waamuzi, lakini hawakuwasikiliza. Walimfunga Nefi kwa kamba Helamani 9:18–19 Waamuzi walimuahidi Nefi fedha na maisha yake kama angesema kwamba alipanga kumuua mwamuzi mkuu. Helamani 9:20–21 Nefi aliwaambia waamuzi watubu uovu wao. Kisha aliwaambia waende kwa Seantumu kaka wa Seezoramu. Helamani 9:22, 26 Nefi aliwaambia wamuulize Seantumu kama yeye na Nefi walipanga kumuua Seezoramu. Nefi alisema Seantumu angejibu “hapana.” Helamani 9:27–28 Kisha waamuzi walitakiwa kumuuliza Seantumu kama alimuua kaka yake. Seantumu angesema “hapana, “ lakini waamuzi watakuta damu kwenye kanzu yake. Helamani 9:29–31 Nefi alisema Seantumu kisha angetetemeka na kunyauka na hatimaye atakiri kumuua kaka yake. Helaman 9:33–35 Waamuzi walikwenda kwenye nyumba ya Seantumu, na kila kitu kilitokea kama Nefi alivyosema kingetokea. Nefi na wale watano waliachiwa huru. Helamani 9:37–38 Wakati watu wakiachana na Nefi, baadhi walisema alikuwa ni nabii; na wengine walisema alikuwa ni mungu. Nefi alikwenda nyumbani, akiwa bado na huzuni kuhusu uovu wao. Helamani 9:40–41; 10:2–3