Sura ya 25 Haruni Anamfundisha Baba wa Mfalme Lamoni Roho aliwaongoza Haruni na wenzake hadi nchi ya Nefi kumfundisha baba wa Lamoni, mfalme wa Walamani wote. Alma 22:1 Haruni alimwambia mfalme kuwa alikuwa kaka yake Amoni. Mfalme alikuwa akifikiria kuhusu ukarimu wa Amoni na kuhusu kile ambacho Amoni alikuwa amemwambia. Alma 22:2–3 Haruni alimuuliza mfalme kama aliamini katika Mungu. Mfalme alisema hakuwa na uhakika lakini angeamini kama Haruni angesema kuna Mungu. Haruni alimhakikishia mfalme kwamba Mungu yu hai. Alma 22:7–8 Haruni alimsomea mfalme maandiko. Alimfundisha kuhusu Uumbaji wa dunia, Anguko la Adamu, na misheni ya Yesu Kristo. Alma 22:12–14 Mfalme aliuliza kile ambacho alihitaji kufanya ili apate Roho Mtakatifu na awe tayari kuishi na Mungu. Mfalme alikuwa tayari kufanya chochote, hata kuacha ufalme wake. Alma 22:15 Haruni alimwambia mfalme kwamba alihitaji kutubu dhambi zake kikamilifu. Alihitaji kusali na kuwa na imani kwa Mungu. Alma 22:16 Mfalme alisali aweze kujua ikiwa kweli Mungu yupo. Alisema angetubu dhambi zake zote. Alma 22:17–18 Mfalme alianguka sakafuni na akaonekana kama amefariki. Wakati malkia alipomwona, alidhani ya kwamba Haruni na wenzake walikuwa wamemuua. Alma 22:19 Malkia aliwashurutisha watumishi wake wawaue Haruni na wenzake, lakini watumishi waliogopa. Aliwatuma wakawatafute watu wengine ambao wangefanya hivyo. Alma 22:20–21 Kabla ya umati mkubwa kukusanyika na kusababisha usumbufu, Haruni aliuchukua mkono wa mfalme na kumuambia asimame. Mfalme alisimama. Alma 22:22 Mfalme alimtuliza mkewe na watumishi waliokuwa wamejawa hofu na kisha akawafundisha injili. Wote waliamini katika Yesu Kristo. Alma 22:23