Scripture Stories
Sura ya 50: Wayaredi Wanaondoka Babeli


Sura ya 50

Wayaredi Wanaondoka Babeli

Picha
Yaredi na kaka yake wakiongea

Yaredi na kaka yake walikuwa watu wenye haki ambao waliishi katika mji wa Babeli. Waliishi mamia ya miaka kabla ya Wanefi.

Picha
Watu waovu katika Babeli

Wengi wa watu huko Babeli walikuwa waovu. Walijenga mnara kujaribu kufika mbinguni. Bwana alikasirika na akabadili lugha yao.

Picha
Yaredi akiongea na kaka yake

Yaredi alimuomba kaka yake kusali na kumuomba Bwana kutobadili lugha ya familia na rafiki zao.

Picha
Kaka wa Yaredi

Kaka wa Yaredi alisali, na Bwana akajibu sala yake. Yaredi, kaka yake, na familia na rafiki zao bado wangeweza kuelewana.

Picha
Yaredi na familia yake wakiondoka

Bwana alimwambia kaka wa Yaredi kukusanya familia yake na rafiki zake na kuondoka katika nchi. Walichukua wanyama na kila aina ya mbegu pamoja nao.

Picha
Wayaredi wakisafiri

Bwana alisema angewaongoza Wayaredi kwenda nchi ya ahadi.

Picha
Wayaredi

Wayaredi walikamata ndege na samaki kwa ajili ya kwenda nao.

Picha
Asali ya nyuki

Walichukua makundi ya nyuki wa asali.

Picha
Wayaredi wakisafiri

Wayaredi walisafiri nyikani. Bwana alizungumza nao kutoka katika wingu na kuwaambia njia ipi ya kupita.

Picha
Wayaredi

Bwana alisema watu walioishi kwenye nchi ya ahadi lazima wamtumikie Mungu au sivyo wataharibiwa.

Picha
Wayaredi wakipiga hema ufukoni

Wakati Wayaredi walipofika kwenye ufuko wa bahari, walipiga hema zao. Walikaa kwenye ufuko kwa miaka minne.

Chapisha