Sura ya 20 Alma na Nehori Kabla Mfalme Mosia hajafa, Wanefi walichagua waamuzi kuwaongoza. Alma mdogo alikuwa mwamuzi mkuu wa kwanza. Pia alikuwa ni kiongozi wa Kanisa. Mosia 29:41–42 Mtu mmoja mkubwa, mwenye nguvu aliyeitwa Nehori alianza kufundisha uongo. Alisema kila mtu angeokolewa bila kujali walikuwa wema au waovu. Watu wengi walimwamini Nehori. Alma 1:2–5 Nehori alifundisha kinyume na Kanisa la Mungu, lakini mtu mwenye haki aliyeitwa Gideoni alitetea Kanisa. Nehori alibishana na Gideoni, lakini Gideoni aliongea kwa maneno ya Mungu. Alma 1:7–8 Nehori alikasirika na akatoa upanga wake na kumuua Gideoni. Alma 1:9 Nehori alipelekwa kwa Alma kuhukumiwa. Nehori kwa ujasiri alijitetea. Alma 1:10–11 Lakini Alma alisema Nehori alikuwa na hatia kwa sababu alikuwa amewafundisha watu kuwa waovu na alimuua Gideoni. Alma 1:12–13 Alma alisema Nehori alitakiwa kuadhibiwa kwa kumuua Gideoni. Kulingana na sheria, Nehori lazima afe. Alma 1:14 Nehori alipelekwa kwenye mlima ulioko karibu na akauliwa. Kabla hajafa alisema kila kitu alichokifundisha kilikuwa cha uongo. Lakini watu wengi bado waliyaamini mafundisho ya uongo ya Nehori. Alma 1:15–16 Watu hawa walipenda utajiri na wasingetii amri za Mungu. Waliwadhihaki waumini wa Kanisa na kubishana na kupigana nao. Alma 1:16, 19–20, 22 Watu wema waliendelea kutii amri na hawakunung’unika hata wakati wafuasi wa Nehori walipowaumiza. Alma 1:25 Waumini wa Kanisa walishiriki kila kitu walichokuwa nacho na masikini, na waliwajali wagonjwa. Walitii amri, na Mungu aliwabariki. Alma 1:27, 31