Scripture Stories
Sura ya 29: Alma Anafundisha kuhusu Imani na Neno la Mungu


Sura ya 29

Alma Anafundisha kuhusu Imani na Neno la Mungu

Picha
Alma akiwafundisha Wazoramu

Alma aliwafundisha Wazoramu kuhusu imani. Alisema wale watu ambao huhitaji ishara kabla ya wao kuamini hawana imani.

Picha
Alma akihubiri

Alma alisema imani ni kusadiki kwamba jambo fulani ni la kweli bila hasa kuliona.

Picha
mkono ukipanda mbegu

Alielezea kwamba imani hukua wakati mtu anapokuwa na hamu ya kuamini na kusikia neno la Mungu. Neno kisha linapandwa katika moyo wa mtu huyo, na kama mbegu linaanza kukua.

Picha
wenza wakiutazama mti

Wakati mtu anapojifunza zaidi kuhusu injili, mbegu inachipuka na kuendelea kukua. Mtu huyo anajua kwamba mbegu hiyo ni nzuri, na imani yake inakua imara zaidi.

Picha
mume na mkewe wakichuma matunda

Alma alisema kwamba kama vile mbegu nzuri inavyozaa matunda mema, neno la Mungu linaleta baraka kwa watu walio na imani.

Chapisha