Sura ya 23 Amoni: Mtumishi Mkuu Wana wanne wa Mosia waliondoka Zarahemla kwenda kufundisha Walamani injili. Kila mmoja alikwenda katika mji tofauti. Alma 17:12–13 Amoni alikwenda katika nchi ya Ishmaeli. Alipokuwa akiingia kwenye mji, Walamani walimfunga kamba na wakamchukua mpaka kwa mfalme, Lamoni. Alma 17:20–21 Amoni alimwambia Mfalme Lamoni kwamba alitaka kuishi kati ya Walamani. Lamoni alifurahi na akawaambia watu wake wamfungue Amoni. Alma 17:22–24 Amoni alisema angekuwa mmoja wa watumishi wa mfalme. Mfalme alimtuma aende kuchunga mifugo. Alma 17:25 Siku moja wakati Amoni na baadhi ya watumishi wengine walikuwa wakipeleka mifugo kunywa maji, Walamani wezi waliitawanya mifugo na kujaribu kuiiba. Alma 17:26–27; 18:7 Watumishi waliokuwa na Amoni waliogopa. Mfalme Lamoni alikuwa amewauwa watumishi wake wengine waliopoteza mifugo. Alma 17:28 Amoni alijua hii ilikuwa ni fursa ya kutumia nguvu za Bwana kuvutia mioyo ya Walamani. Kisha wangesikiliza mafundisho yake. Alma 17:29 Amoni aliwaambia watumishi kwamba kama wangeikusanya mifugo iliyotawanywa, mfalme asingewaua. Alma 17:31 Amoni na watumishi wengine haraka waliipata mifugo na kuirudisha katika sehemu ya kunyweshea. Alma 17:32 Walamani wezi walirudi tena. Amoni aliwaambia watumishi wengine kuichunga mifugo wakati akipigana na wezi. Alma 17:33 Walamani wezi hawakumwogopa Amoni. Walifikiri wangemuua kiurahisi. Alma 17:35 Nguvu za Mungu Zilikuwa pamoja na Amoni. Aliwapiga na kuwauwa baadhi ya wezi kwa mawe, kitu ambacho kiliwafanya wezi waliosalia kupata hasira sana. Alma 17:35–36 Walijaribu kumuua Amoni kwa rungu zao, lakini kila mara mwizi aliponyanyua rungu kumpiga, Amoni alikata mkono wa mwizi. Kwa kuogopa, wezi walikimbia. Alma 17:36–38 Watumishi walipeleka mikono iliyokatwa kwa Mfalme Lamoni na kumwambia ambacho Amoni alikuwa amekifanya. Alma 17:39; 18:1 Mfalme alishangazwa na nguvu kuu ya Amoni. Alitaka kumuona Amoni lakini aliogopa kwa sababu alidhani Amoni alikuwa ni Roho Mkuu. Alma 18:2–4, 11 Wakati Amoni alipokwenda ndani kumuona, Mfalme Lamoni hakujua nini cha kusema. Hakuongea kwa muda wa saa moja. Alma 18:14 Roho Mtakatifu alimsaidia Amoni kujua nini mfalme alikuwa akiwaza. Amoni alifafanua kwamba yeye hakuwa Roho Mkuu. Alikuwa ni mtu. Alma 18:16–19 Mfalme alimuahidi Amoni chochote alichotaka kama angemwabia ni nguvu gani alitumia kuwashinda wezi na kujua mawazo ya mfalme. Alma 18:20–21 Amoni alisema kitu pekee alichokitaka ni Mfalme Lamoni kuamini kile ambacho angekisema. Mfalme alisema angeamini chochote ambacho Amoni angemwambia. Alma 18:22–23 Amoni alimuuliza Mfalme Lamoni kama aliamini katika Mungu. Mfalme alisema kwamba aliamini katika Roho Mkuu. Alma 18:24–27 Amoni alisema kwamba Roho Mkuu ni Mungu, ambaye aliumba kila kitu mbinguni na duniani, na kwamba anajua mawazo ya watu. Alma 18:28–32 Amoni alisema watu waliumbwa kwa mfano wa Mungu. Pia alisema Mungu alimwita kufundisha injili kwa Lamoni na watu wake. Alma 18:34–35 Akitumia maandiko, Amoni alimfundisha Mfalme Lamoni kuhusu Uumabji, Adamu, na Yesu Kristo. Alma 18:36, 39 Mfalme Lamoni alimwamini Amoni na alisali ili kusamehewa dhambi zake. Kisha alianguka ardhini na kuonekana kama mfu. Alma 18:40–42 Watumishi walimbeba mfalme mpaka kwa mke wake na kumlaza kitandani. Baada ya siku mbili watumishi walidhani alikuwa amekufa na walitaka kumzika. Alma 18:43; 19:1 Malkia hakuamini kwamba mume wake alikuwa amekufa. Akiwa amesikia kuhusu nguvu kuu ya Amoni, alimuomba amsaidie mfalme. Alma 19:2–5 Amoni alijua Lamoni alikuwa chini ya nguvu za Mungu. Alimwambia malkia kwamba Lamoni angeamka siku iliyofuata. Alma 19:6–8 Malkia alikaa pembeni mwa Lamoni usiku mzima. Siku iliyofuata Lamoni aliamka na alisema alimuona Yesu Kristo. Mfalme na malkia walijazwa na Roho Mtakatifu. Alma 19:11–13 Lamoni aliwafundisha watu wake kuhusu Mungu na Yesu Kristo. Wale walioamini walitubu dhambi zao na walibatizwa. Alma 19:31, 35