Sura ya 31 Kapteni Moroni anamshinda Zerahemna Zerahemna, kiongozi wa Walamani, alitaka watu wake waendelee kuwachukia Wanefi na kuwafanya watumwa wao. Alma 43:5, 8 Wanefi walitaka kuiweka huru nchi yao na familia zao. Pia walitaka kuwa huru kumwabudu Mungu. Alma 43:9 Kapteni Moroni alikuwa kiongozi wa jeshi la Wanefi. Wakati Walamani walipokuja kupigana, Moroni na jeshi lake walikutana nao katika nchi ya Jershoni. Alma 43:15–16 Kapteni Moroni aliandaa jeshi lake kwa silaha, ngao, mavazi ya kivita na nguo nzito. Alma 43:18–19 Walamani walikuwa na jeshi kubwa lakini waliogopa wakati walipoona mavazi ya kivita ya Wanefi—Walamani walikuwa wamevaa nguo chache sana. Alma 43:20–21 Jeshi la Walamani halikuthubutu kupigana na jeshi la Kapteni Moroni. Walamani walikimbilia nyikani na kuamua kushambulia mji mwingine wa Wanefi. Alma 43:22 Moroni alituma wapelelezi kuwapeleleza Walamani. Pia alimuomba Alma asali kwa Bwana kwa ajili ya msaada. Bwana alimwambia Alma wapi Walamani wangeshambulia. Alma 43:23–24 Wakati Moroni alipopokea ujumbe wa Alma, aliacha baadhi ya wanajeshi kulinda Jershoni na akasonga na waliobaki kukutana na Walamani. Alma 43:25 Wanajeshi wa Kapteni Moroni walijificha kwenye pande zote mbili za mto Sidoni, wakisubiri kulitia mtegoni jeshi la Walamani. Alma 43:27, 31–35 Vita vilianza, Walamani walijaribu kutoroka kwa kuvuka mto, lakini wanefi wengi zaidi walikuwa wakisubiri upande mwingine wa mto. Alma 43:36, 39–41 Wakipigana kwa nguvu kuliko hapo awali, Zerahemna na jeshi lake waliwauwa wanefi wengi. Wanefi walimlilia Bwana kwa ajili ya msaada. Alma 43:43–44, 49 Bwana aliliimarisha jeshi la Wanefi. Jeshi liliwazunguka Walamani, na Moroni aliamuru vita kusimama. Alma 43:50, 52–54 Moroni alimwambia Zerahemna kwamba Wanefi hawakutaka kuwauwa Walamani au kuwafanya watumwa wao. Alma 44:1–3 Moroni alisema walamani wasingeweza kuiua imani ya Wanefi katika Yesu Kristo. Alisema Mungu angeendelea kuwasaidia Wanefi kupigana kama wangekuwa waaminifu. Alma 44:4 Moroni alimwamuru Zerahemna kusalimisha silaha zake. Walamani wasingeuwawa kama wangeahidi kutopigana na Wanefi tena. Alma 44:5–6 Zerahemna alimpa Moroni silaha zake lakini hakuahidi kutopigana. Moroni alimrudishia silaha zake ili walamani wajilinde. Alma 44:8, 10 Zerahemna kwa haraka alikwenda kwa Moroni ili kumuua, lakini askari wa Wanefi alimpiga na kuuvunja upanga wa Zerahemna. Alma 44:12 Kisha askari alitoa ngozi ya kichwa cha Zerahemna na, akakiweka kwenye ncha ya upanga, na kuinyanyua juu. Alma 44:12–13 Walamani wangeanguka ardhini kama ngozi ya kichwa ilivyoanguka, aliwaambia, isipokuwa wasalimishe silaha zao na kuahidi kamwe kutopigana tena. Alma 44:14 Wengi wa Walamani waliweka silaha zao miguuni pa Moroni na kuahidi kutopigana tena. Waliruhusiwa kwenda huru. Alma 44:15 Kwa hasira, Zerahemna aliwahamasisha askari waliobaki kupigana. Askari wa Moroni waliwauwa wengi wao. Alma 44:16–18 Wakati Zerahemna alipoona yeye na watu wake wangeuwawa, alimuomba Moroni kutowauwa. Aliahidi kutopigana tena na Wanefi. Alma 44:19 Moroni alisimamamisha vita na kuchukua silaha za Walamani. Baada ya kuwa wameahidi kutopigana, walamani waliondoka. Alma 44:20, 23