Njoo, Unifuate
Machi 9–15. Yakobo 1–4: “Kupatanishwa na Mungu kupitia Upatanisho wa Kristo”


“Machi 9–15. “Yakobo 1–4: ‘Kupatanishwa na Mungu kupitia Upatanisho wa Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Machi 9–15. Yakobo 1–4,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
mwanamke akiwa amepiga magoti miguuni kwa Yesu

Kusamehewa, na Greg K. Olsen

Machi 9–15

Yakobo 1–4

Kupatanishwa na Mungu kupitia Upatanisho wa Kristo

Unaposoma Yakobo 1–4, tafakari ni kanuni zipi kutoka sura hizi ni za muhimu zaidi kwa watoto kujifunza. Tafuta mwongozo wa kiroho kujua jinsi ya kufundisha kanuni hizi vizuri zaidi, na andika misukumo yako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki jambo ambalo wao au familia zao walifanya wiki hii kujifunza kutoka Yakobo 1–4. Ungeweza pia kuwaomba kushiriki jambo wanalokumbuka kutoka kwenye somo la wiki iliyopita. Ni maswali yapi ungeweza kuuliza kuwasaidia kukumbuka?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Yakobo 1:6–8, 18; 2:1–11

Mungu huwaita viongozi wa Kanisa kunisaidia mimi kumfuata Yesu Kristo.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba watabarikiwa kwa kufuata ushauri wa viongozi wa Kanisa.

Shughuli za Yakini

  • Tengeneza vikaragosi rahisi kumwakilisha Yakobo na Yusufu, kaka wadogo wa Nefi, ambao walikuwa viongozi wa Kanisa. Shiriki baadhi ya mistari kutoka Yakobo 1 na 2 kuelezea kile viongozi wa Kanisa wameitwa kufanya. Kwa mfano, viongozi hutushawishi sisi ku “mwamini Kristo” (Yakobo 1:8), hutualika kutubu (ona Yakobo 2:5–6, 9–10), na “hutangaza neno la [Mungu]” (Yakobo 2:2, 11). Acha watoto watumie vikaragosi kujifanya wanatenda baadhi ya mambo haya.

  • Waalike watoto kutaja majina ya baadhi ya viongozi wa Kanisa wanaowajua, kama viongozi wa Msingi, washiriki wa uaskofu, na nabii na mitume. Wasaidie watoto kufikiria jinsi viongozi hawa wanavyotubariki.

Picha
Watu wawili wakisalimiana kwa mikono kwenye meza ya kuandikia

Viongozi wetu wa Kanisa hutusaidia kumfuata Yesu Kristo.

Yakobo 2:12–14, 17–21

Ninaweza kuwasaidia wengine wenye uhitaji pale ninaposhiriki nao.

Je, watoto unaowafundisha wanaelewa baraka zinazokuja pale wanaposhiriki na wale wenye uhitaji? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kujua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanawataka wao kuwasaidia wengine?

Shughuli za Yakini

  • Elezea kwamba baadhi ya watu katika kipindi cha Yakobo walikuwa matajiri sana, lakini hawakutaka kushiriki walichokuwa nacho na watu waliokuwa masikini. Soma Yakobo 2:17–19 kuwasaidia watoto kuelewa mafundisho ya Yakobo kwa watu hawa. Unapofanya hivyo, wape watoto picha au vitu kushikilia ambavyo vinaendana na maneno au kifungu cha maneno katika mistari hii.

  • Waalike watoto kuigiza jinsi wanavyoweza kushiriki kile walichonacho na mtu mwenye uhitaji. Shuhudia kwamba tunabarikiwa pale tunaposhiriki na wengine.

  • Leta kitu darasani ambacho unaweza kushiriki pamoja na watoto. Toa kiasi cha kitu hicho kwa kila mtoto, na elezea kwamba unashiriki. Waulize jinsi walivyohisi pale uliposhiriki nao. Je! Wanahisi vipi wanaposhiriki na wengine? Wasaidie kufikiria kitu fulani ambacho wangeweza kushiriki kumfanya mtu mwingine awe na furaha.

Yakobo 4:6

Ninaweza kuimarisha imani yangu katika Yesu Kristo.

Kama Yakobo alivyoishi kwa haki licha ya uovu uliomzunguka, imani yake ilikuwa imara sana kwamba isingeweza kutingishwa. Tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa nini inamaanisha kuwa na imani ambayo haiwezi kutingishwa.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya vitu wanavyofanya kuifanya miili yao iwe imara. Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha imani yetu? Fungua maandiko kwenye Yakobo 4:6, na wasaidie watoto kugundua kile Yakobo na watu wake walifanya kuifanya imani yao “isiyotingishika.”

  • Imba “The Wise Man and the Foolish Man” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281, pamoja na watoto. Katika upande mmoja wa ubao, chora nyumba iliyojengwa juu ya mchanga. Katika upande mwingine wa ubao, chora nyumba iliyojengwa juu ya mwamba. Kama inawezekana, leta mchanga na jiwe darasani. Kipi ni rahisi kutikisa au kuondoa? Kipi, mchanga au jiwe, tunataka imani yetu ifanane nacho?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Yakobo 1:6–8, 18; 2:1–6, 11

Mungu huwaita viongozi wa Kanisa kunisaidia mimi kumfuata Yesu Kristo.

Watoto unaowafundisha watabarikiwa wanapoamini na kufuata ushauri wa viongozi wa Kanisa.

Shughuli za Yakini

  • Soma pamoja na watoto Yakobo 1:6–8 na 2:1–6, 11, ukiwasaidia kutafuta vifungu vya maneno ambavyo vinaelezea jinsi watumishi wa Mungu wanavyoongoza Kanisa. Waombe waandike vifungu hivi vya maneno kwenye vipande vya karatasi na kisha weka karatasi hizo ubaoni. Je, ni kwa nini Mungu huwaita viongozi wa Kanisa kutuongoza? Waombe watoto kushiriki uzoefu wa kujifunza au kupokea mwongozo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa au mwalimu pamoja na baraka walizopokea.

  • Waombe watoto kuchora picha ya kiongozi wa Kanisa wanaemjua, na acha wanadarasa wengine wabahatishe ni nani waliyemchora. Ni nini viongozi hawa hufanya kutusaidia sisi kumfuata Yesu Kristo? Waalike watoto kuandika jumbe kwa viongozi wa Kanisa, wakiwashukuru kwa huduma yao.

  • Mwalike kiongozi wa Kanisa wa eneo lako kuwaambia watoto kile anachofanya kutimiza wito wake. Waombe watoto kutaja baadhi ya mambo wanayoweza kufanya kuwaunga mkono viongozi wao.

Yakobo 2:12–14, 17–21

Ninaweza kuwasaidia wengine kuwa na furaha kwa kushiriki nao.

Wafuasi wa kweli wa Kristo wako tayari kushiriki kile walichonacho pamoja na wengine. Washirikishe watoto kuleta furaha kwa wale wenye uhitaji kwa kushiriki nao.

Shughuli za Yakini

  • Waambie watoto kwamba watu wengi katika kipindi cha Yakobo walikuwa na kiburi na hawakuwa wakarimu kwa sababu walipenda utajiri (ona Yakobo 2:12–14, 17–21). Waalike watoto kadhaa kusoma Yakobo 2:17–19 kwa sauti, na wasaidie kuelewa maneno yoyote magumu. Ni nini tungepaswa kutafuta kabla ya kutafuta utajiri? Ni nini tungepaswa kufanya kwa utajiri tunaopata?

  • Soma Yakobo 2:17 kwa watoto. Ni baraka zipi ambazo Baba wa Mbinguni ameshiriki nasi? Ni kwa nini anataka sisi tushiriki na wengine? Waalike watoto kushiriki nyakati ambapo walishiriki kitu na mtu mwingine, ikijumuisha jinsi walivyohisi na jinsi yule mtu mwingine alivyohisi.

Yakobo 4:4–13, 17

Ninaweza kuimarisha imani yangu katika Yesu Kristo.

Imani ya Yakobo ilikuwa isiyotingishika pale alipotafuta maneno ya manabii na kupokea ushahidi wake mwenyewe (ona Yakobo 4:6). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na hamu ya kujenga imani isiyoweza kutingishika?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufikiria juu ya vitu vilivyokuwa imara na thabiti kulingana na muda, kama vile mti mkubwa. Ni kwa jinsi gani imani ni kama vitu walivyovifikiria? Ni vifungu gani vya maneno katika Yakobo 4:6, 10–11 huelezea kile tunachoweza kutenda kuifanya imani yetu isiyotingishika? Waombe watoto kutengeneza orodha ubaoni ya jinsi wanavyoweza kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo.

  • Shiriki analojia ya Mzee Neil L. Andersen ya mti unaokua katika mazingira yenye kimbunga, inayopatikana katika ujumbe wake “Vimbunga vya Kiroho” (Ensign au Liahona, Mei 2014, 18–21), au onyesha video “Vimbunga vya Kiroho” (ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini ni muhimu kwa imani yetu kuwa isiyotingishika na imara kama shina la mti? Je, vimbunga vya kiroho huwakilisha nini? Ni nini tunaweza kufanya kujenga imani isiyotingishika? Wasaidie watoto kufikiria analojia zingine ambazo hufundisha kuhusu imani ambayo haiwezi kutingishika.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufikiria kitu wanachoweza kushiriki na familia zao—ikijumuisha kushiriki jambo walilojifunza darasani leo. Wape nafasi katika somo lijalo kuzungumza kuhusu kile walichoshiriki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba wimbo kimya kimya au kimoyomoyo au kuonyesha picha ya Yesu.

Chapisha