“Machi 16–22. “Yakobo 5–7: ‘Bwana hufanya kazi nasi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Machi 16–22. Yakobo 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Machi 16–22
Yakobo 5–7
Bwana hufanya kazi nasi
Soma, tafakari, na omba kujua namna nzuri zaidi unavyoweza kuwafundisha watoto kweli zinazopatikana katika Yakobo 5–7. Andika misukumo yoyote unayopokea.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kuanza mjadala kuhusu jumbe zinazopatikana katika Yakobo 5–7, waalike watoto kuzungumza kuhusu mambo katika maisha yao ambayo yanawasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani tunaonyesha upendo wetu kwa wengine?
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Wamisionari huwatumikia watoto wa Baba wa Mbinguni.
Fikiria jinsi unavyoweza kushiriki istiari ya miti ya mizeituni katika njia ambayo watoto wanaweza kuelewa.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya mti, au tembea nje kuangalia mti, na kwa ufupi pitia tena alama muhimu za istiari ya miti ya mizeituni katika Yakobo 5. Kwa mfano: Bwana wa shamba (ambayo ingeweza kumwakilisha Yesu) alifanya kazi kwa bidii kubwa kuitunza miti yake ya mizeituni (ambayo ingeweza kuwakilisha watu duniani) kwa sababu aliwajali sana. Aliwaita wafanyakazi (ambayo ingeweza kuwakilisha wamisionari) kusaidia kuitunza miti. Chagua mstari mmoja au miwili kutoka Yakobo 5 kuwasomea watoto (kama vile mistari 71–72).
-
Waulize watoto kama wanamjua mtu aliyetumikia misheni, au zungumza kuhusu yeyote unayemjua. Wasaidie watoto kuonyesha kwenye ramani maeneo ambapo wamisionari hao wanatumikia. Elezea kwamba Yakobo alilinganisha ulimwengu na kundi la miti ya mizeituni. Miti ni sawa na watu duniani, na kuitunza miti hiyo ni sawa na kile wamisionari hufanya kwa watoto wa Mungu. Ni nini wamisionari hufanya kuwabariki watoto wa Mungu? Tafuteni kwa pamoja baadhi ya majibu ya swali hili kwenye wimbo kama vile “Called to Serve” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 174–75). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama wamisionari?
Baba wa Mbinguni ananipenda.
Ni kwa jinsi gani unaweza kufundisha darasa lako kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote na ananyoosha “mkono Wake wa huruma” kwao?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kukumbatiana. Je, tunahisi vipi wakati mtu tunayempenda anapotukumbatia? Soma Yakobo 6:5 kwa watoto, na elezea kwamba kifungu cha maneno “[Mungu] huwashikilia” na “mkono wake wa huruma umenyooshwa kwenu” hufundisha kwamba Baba wa Mbinguni anatupenda na anataka sisi turudi Kwake siku moja.
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu upendo, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75). Waalike watoto kutaja mambo yanayowasaidia wao kuhisi upendo wa Mwokozi.
Ninaweza kusimamia kile ninachojua ni cha kweli.
Yakobo ni mfano bora wa mtu ambaye ushuhuda wake imara umemsaidia kutetea ukweli mbele ya upinzani.
Shughuli za Yakini
-
Simulia hadithi ya Yakobo na Sheremu (Yakobo 7:1–23) katika njia ambayo watoto wanaweza kuelewa. Ungeweza kutumia “Sura ya 10: Yakobo na Sheremu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni,, 27–29, au video zinazohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Kisha simulia hadithi tena, lakini wakati huu waruhusu watoto wasaidie kujaza maelezo. Waulize kile walichojifunza kutoka kwa Yakobo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wake?
-
Waalike watoto kuimba wimbo kuhusu kuchagua mema, kama vile “Dare to Do Right” au “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 158, 159). Waombe kusimama kila wanapoimba maneno kama mema au kweli.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Bwana anawajali watu Wake.
Yakobo anashiriki istiari ya miti ya mizeituni kusaidia kuwaalika watu Wake kuja kwa Kristo. Inaweza kufanya hivyo hivyo kwa watoto unaowafundisha.
Shughuli za Yakini
-
Soma na elezea kwa watoto mistari ya msingi inayofupisha istiari ya miti ya mizeituni, kama vile Yakobo 5:3–4, 28–29, 47, and 70–72, na waalike watoto kuchora picha ya kile mistari hii huelezea. Je, tunajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu jinsi Bwana anavyohisi kuhusu watu Wake? Waombe watoto wajifanye kuutunza mti wa mzeituni pale unapofanya ufupisho wa mistari 61–71 (wanaweza kuigiza kulima, kumwagilia, na kadhalika). Waalike watoto kadhaa kusoma Yakobo 5:11, 41, 47, na 72, wakitafuta mambo yanayoonyesha ni jinsi gani Bwana wa shamba (Yesu Kristo) alivyoitunza miti. Je, ni nini Mwokozi anafanya kuonyesha Yeye anatujali? Video “Shamba la Mizeituni la Agano la Kale”(ChurchofJesusChrist.org) inaweza kusaidia kwa shughuli hii.
-
Orodhesha baadhi ya alama katika Yakobo 5 ubaoni, kama vile shamba, bwana wa shamba, mtumishi, na miti ya mizeituni. Kisha tengeneza orodha nyingine, katika mpangilio usio sahihi, ya vitu alama hizi zingeweza kuwakilisha, kama vile ulimwengu, Mwokozi, viongozi wa Kanisa au wamisionari, na watu wa Mungu. Someni kwa pamoja mistari kutoka Yakobo 5 ambayo hutaja alama hizi, na wasaidie watoto kuchora mistari ubaoni kuunganisha alama na maana zake (ona, kwa mfano, mistari 3–4, 28–29, 47, 70–72).
Baba wa Mbinguni ananipenda na atanisamehe pale ninapotubu.
Ni muhimu kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba Mungu anawapenda na daima atawasamehe wanapotubu kwa dhati.
Shughuli za Yakini
-
Tengeneza chati ubaoni yenye safu mbili zilizoandikwa Baba wa Mbinguni na sisi. Someni pamoja Yakobo 6:4–5, na waulize nusu ya darasa kutafuta vifungu vya maneno ambavyo vinatumika kwa Mungu na nusu nyingine kutafuta vifungu vya maneno vinavyotumika kwetu. Andika kile wanachogundua kwenye safu inayohusika. Wasaidie kutoa maana ya maneno ambayo hawayaelewi.
-
Shiriki hadithi ya Mzee Allen D. Haynie kuhusu kuchafuka kwenye shimo la matope katika ujumbe wake “Kukumbuka katika Yeye Ambaye Tumemwamini” (Ensign au Liahona, Nov. 2015, 121–22). Je, ni nini hadithi hii hutufundisha kuhusu kile tunachopaswa kufanya kuokolewa katika ufalme wa Mungu? Kitu gani kingine tunachojifunza kutoka Yakobo 6:4–5?
Ninaweza kusimamia kile ninachojua ni cha kweli.
Ni kwa jinsi kwa gani unaweza kuwashawishi watoto kusimamia ukweli kama Yakobo alivyofanya?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kuigiza majibizano kati ya Yakobo na Sheremu, kwa kutumia Yakobo 7:1–23 kama mwongozo. Au onyesha video “Yakobo na Sheremu” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto kuzungumza kuhusu vipengele wanavyovipenda vya hadithi. Ni kwa jinsi gani Yakobo alisimama kwenye kile alichojua kilikuwa cha kweli? Waombe watoto kushiriki uzoefu wakati waliposimamia kweli, au shiriki wa kwako mwenyewe.
-
Waalike watoto kuimba wimbo kuhusu kuchagua yaliyo mema, kama vile ““Dare to Do Right” au “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 158, 159). Wagawe katika makundi, na waalike kutengeneza bango lenye ushawishi au tangazo ambalo linawakilisha jambo wanalolisimamia au kuliamini.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kufikiria jinsi wanavyoweza kuzisaidia familia zao kuhisi upendo wa Mwokozi—kwa mfano, kwa kuelezea kile walichojifunza kuhusu jinsi Bwana wa shamba alivyotunza miti yake ya mizeituni.