“Machi 30–Aprili 12. Pasaka: ‘Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Machi 30–Aprili 12. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Machi 30–Aprili 12
Pasaka
“Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake”
Unaposoma maandiko yaliyopendekezwa hapa na kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, roho atakusaidia kujua kipi cha kutilia mkazo kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Mwokozi katika Jumapili ya Pasaka.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Zungumza na watoto kuhusu mambo unayofanya kumkumbuka Mwokozi kwenye Pasaka. Waalike kushiriki kile wao wanachofanya.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
1 Nefi 11:27; Mosia 3:5; 15:7; Helamani 14:16–17
Manabii wa Kitabu cha Mormoni walijua kwamba Yesu Kristo angekuja.
Kujifunza kile manabii wa Kitabu cha Mormoni walichofundisha kuhusu wito wa Yesu Kristo na huduma yake duniani kunaweza kusaidia kuimarisha imani ya watoto Kwake.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya Mwokozi akibatizwa, akiponya wengine, akisulubiwa, na kama kiumbe aliyefufuka (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii au Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 35, 41, 57, 59). Waombe watoto wakuambie nini kinachojiri katika picha. Elezea kwamba miaka mingi kabla Yesu hajaja duniani, Mungu aliwafunulia manabii katika Kitabu cha Mormoni kwamba angetenda mambo haya. Soma 1 Nefi 11:27; Mosia 3:5; 15:7; na Helamani 14:16–17, na wasaidie watoto kuoanisha maandiko haya na picha zinazohusiana.
-
Wakati watoto wakifanyia kazi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, zungumza kuhusu manabii walioonyeshwa na kile walichofundisha kuhusu Yesu Kristo. Shiriki pamoja na watoto baadhi ya mambo ya kupendeza Yesu aliyoyafanya kwa ajili yetu.
Yesu Kristo alifufuka.
Wafundishe watoto kwamba kwa kuongezea kwenye watu waliomuona Mwokozi aliyefufuka huko Yerusalemu, maelfu walimuona wakati Yeye alipotokea katika Amerika.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya kifo na Ufufuko wa Mwokozi. Waulize watoto ni nini wanachojua kuhusu matukio haya. Kama inavyohitajika, tumia “Mlango wa 53: Yesu Anasulubiwa” na “Mlango wa 54: Yesu Amefufuka” (Hadithi za Agano Jipya, 136–38, 139–44, au video zinazohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org) kuwasimulia watoto hadithi hizi.
-
Kwa kutumia picha kutoka Kitabu cha Sanaa ya Injili au Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, wasimulie watoto kuhusu matembezi ya Mwokozi aliyefufuka huko Amerika, kama ilivyoelezewa katika 3 Nefi 11:1–17. Rudia hadithi mara kadhaa, ukiwaalika watoto wakusaidie. Sisitiza maelezo ambayo unahisi yatakuwa na maana kwa watoto. Kwa kipekee, sisitiza kwamba japokuwa Yesu alikuwa amekufa msalabani, watu wangeweza kuona kwamba Yeye sasa alikuwa amefufuka. Acha watoto wafanye zamu kusimulia tena hadithi kwa maneno yao wenyewe.
-
Imbeni kwa pamoja “Easter Hosanna” au aya ya mwisho ya “Hadithi za Kitabu cha Mormoni” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69, 118–19). Waalike wanafunzi kuchora picha za vitu ambavyo wimbo unavielezea. Kisha waombe watoto kushiriki michoro yao na kile wanachofikiri kingeweza kuhisiwa kama kuwa pale wakati Yesu alipowatembelea Wanefi.
Yesu Kristo anajua jinsi ya kunifariji.
Kwa sababu Yesu Kristo aliteseka “maumivu na magonjwa ya watu wake” (Alma 7:11), Yeye anajua jinsi tunavyohisi, hata wakati hakuna mtu mwingine anayejua.
Shughuli za Yakini
-
Wasomee watoto mistari michache ya kwanza ya Mosia 3:7, na waalike kujifanya wanahisi “maumivu … , njaa, kiu, na uchovu [kuchoka].” Waombe kushiriki nyakati walipohisi mambo haya. Kisha waambie watoto kwamba mstari huu unaelezea baadhi ya mambo Yesu Kristo aliyohisi wakati alipoteseka katika Bustani ya Gethsemane. Kwa sababu ya hili, Yeye anajua jinsi ya kutusaidia tunapohisi mambo haya.
-
Soma Alma 7:11 kwa sauti, na waulize watoto kama wanamjua mtu anayeumwa au yuko katika maumivu. Shuhudia kwamba Yesu Kristo alihisi “maumivu” yetu yote na “magonjwa” ili kwamba aweze kuelewa jinsi ya kutufariji (Alma 7:12).
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
2 Nefi 9:10–15; Alma 11:41–45; 40:21–23
Kwa sababu Yesu Kristo alifufuka, mimi pia nitafufuka.
Kitabu cha Mormoni kwa uwazi huelezea kile ufufuo humaanisha na nani watafufuka. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kugundua kweli hizi?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto wakuambie kile wanachojua kuhusu kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Andika ubaoni maswali kama inamaanisha nini kufufuka? na ni nani watafufuka? wasaidie watoto kutafuta majibu katika 2 Nefi 9:10–15; Alma 11:41–45; na Alma 40:21–23 na kushiriki na darasa kile wanachopata.
-
Waeleze watoto kuhusu mtu fulani unayemjua ambaye amefariki dunia. Waombe kufikiria kwamba wewe hujui kuhusu ufufuo. Ni kwa jinsi gani wangeweza kukusaidia kuelewa ufufuo ni nini? Wahimize kutumia 2 Nefi 9:10–15; Alma 11:41–45; au Alma 40:21–23 kukufundisha kuhusu ufufuo. Pia waalike kutoa shuhuda za Ufufuko wa Mwokozi kama sehemu ya majibu yao.
Enoshi 1:2–8; Mosia 27:8–24; Alma 13:11–12; 24:7–19
Upatanisho wa Yesu Kristo hunisafisha na kunibadilisha.
Kitabu cha Mormoni hutoa mifano mingi ya watu ambao walibadilishwa kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi. Fikiria ni kwa jinsi gani uzoefu huu ungeweza kuwashawishi watoto kutubu na kurudi kwa Mwokozi.
Shughuli za Yakini
-
Waonyeshe watoto shati nyeupe safi na shati nyeupe chafu. Someni pamoja Alma 13:11–12. Ni kwa jinsi gani watu walifanywa wasafi kutoka dhambi zao? Ni kwa jinsi gani hii iliwafanya wahisi kuhusu dhambi? Zungumza kuhusu jinsi unavyohisi wakati unapotubu na kupokea msamaha, na toa ushuhuda wako wa nguvu ya Mwokozi kutusafisha kutoka dhambi.
-
Waalike watoto kuchagua mmoja kati ya watu wafuatao ili kujifunza kuwahusu: Enoshi (ona Enoshi 1:2–8), Alma Mdogo (ona Mosia 27:8–24), au watu wa Anti-Nefi-Lehi ( Alma 24:7–19). Mnaposoma hadithi pamoja, waalike watoto kugundua ni kwa jinsi gani mtu huyu au kundi lilibadilika kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa watu hawa?
Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu, na magonjwa.
Kwa kuongezea kwenye kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu, Mwokozi pia aliteseka maumivu yetu, magonjwa, na madhaifu mengine ili kwamba aweze kujua jinsi ya kutufariji.
Shughuli za Yakini
-
Mpangie kila mtoto kuchunguza moja ya mistari ifuatayo kutafuta kile Yesu Kristo alichoteseka: Mosia 3:7; Mosia 15:5; au Alma 7:11. Waalike kuorodhesha ubaoni kile walichopata na kufikiria nyakati walipohisi baadhi ya mambo haya. Kulingana na Alma 7:12, kwa nini Yesu aliteseka haya yote? Kwa nini ni muhimu kujua Yeye aliteseka mambo haya kwa ajili yetu?
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu Mwokozi, kama vile “Najua Mkombozi Wangu Anaishi” (Nyimbo za Kanisa, na. 136). Waalike watoto kutafuta wimbo wa kanisa kwa ajili ya vifungu vya maneno ambavyo huelezea jinsi gani Mwokozi anatufariji, na zungumza kuhusu kwa nini vifungu hivi vya maneno vina maana kwao. Shiriki hisia zako kuhusu Yesu Kristo, na waalike watoto kushiriki zao.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kumtafuta mtu fulani wiki hii anayehitaji faraja. Wahimize kushiriki na mtu huyu kile walichojifunza kuhusu Mwokozi akijichukulia juu Yake maumivu yetu ili aweze kutufariji.