Njoo, Unifuate
Aprili 20–26. Mosia 4–6: “Mabadiliko Makuu”


“Aprili 20–26. Mosia 4–6: ‘Mabadiliko Makuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Aprili 20–26. Mosia 4–6” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Mfalme Benyamini akiwafundisha watu wake

Katika Kumtumikia Mungu, na Walter Rane

Aprili 20–26

Mosia 4–6

“Mabadiliko Makuu”

Ni yapi kati ya mafundisho ya Mfalme Benyamini katika Mosia 4–6 yatawasaidia vizuri zaidi watoto unaowafundisha kuanza kupata uzoefu wa “mabadiliko makuu” (Mosia 5:2) katika mioyo yao? Andika misukumo yako unapotafuta mwongozo kwa sala.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika jina la kila mtoto katika darasa lako katika kipande cha karatasi, na weka vipande hivyo ndani ya chombo. Unapotoa kila jina ndani ya chombo, mualike mtoto yule kushiriki jambo wanalokumbuka kutoka somo la wiki iliyopita au jambo walilojifunza kutoka Mosia 4–6 nyumbani wiki hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 4:1–3, 10

Toba huleta furaha.

Wasaidie watoto kujifunza kuhusu baraka za ajabu za toba ambazo hupatikana kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Tumia Mosia 4:1–3 na 10 kuwafundisha watoto kile kutubu inachomaanisha. Kwa mfano, wasaidie kugundua kuwa watu wa Mfalme Benyamini walijisikia vibaya kuhusu dhambi zao na kuomba msamaha (mistari 1–2), na Mfalme Benyamini aliwaambia kuacha kutenda dhambi zao (mstari wa 10). Soma mstari wa 3 kwao, na uliza ni jinsi gani watu walihisi pale walipotubu.

  • Waulize watoto jinsi inavyokuwa pale tunapochafua nguo zetu. Je, tunajisikiaje tunapokuwa wasafi tena? Eleza kwamba kama vile kufua nguo chafu, tunaweza kutubu pale tunapofanya kosa. Onyesha picha ya Yesu Kristo, na shuhudia kwamba Yeye anao uwezo kuondoa dhambi zetu na kutufanya wasafi tena kama tutatubu. Imbeni pamoja aya ya pili ya “Help Me, Dear Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 99). Waulize watoto ni nini wimbo unafundisha kuhusu toba.

Mosia 4:13–26

Ninapaswa kuwachukulia wengine kwa upendo na ukarimu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Mosia 4:13–26 kuwafundisha watoto “kupendana, na kutumikiana”? (mstari wa 15).

Shughuli za Yakini

  • Chora moyo mdogo ubaoni. Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyoweza kuwa wakarimu kwa wengine. Kila wakati wanaposhiriki, futa moyo na chora mkubwa zaidi. Shuhudia kwamba upendo wetu kwa wengine unakua pale tunapokuwa wakarimu kwao. Wape watoto mioyo ya karatasi, na waalike kuchora juu ya mioyo jinsi wanavyoweza kuonyesha upendo na kuwa wakarimu.

  • Wasaidie watoto kuja na matendo ya kufanya wanapoimba wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “Jesus Said Love Everyone” au “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61, 136).

Mosia 5:5–15

Ninapofanya maagano na Mungu, ninajichukulia juu yangu jina la Kristo.

Tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujiandaa kufanya maagano ya ubatizo na Mungu na “kuitwa watoto wa Kristo” (Mosia 5:7).

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kutengeneza beji zikionyesha jina “Yesu Kristo” na kuzibandika kwenye mashati yao juu ya mioyo yao (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Elezea kwamba Mfalme Benyamini alifundisha watu wake kwamba tunapofanya maagano, au ahadi, na Mungu, ni kama kuwa na jina la Kristo “kuandikwa daima mioyoni [mwetu]” (Mosia 5:12). Ni nini tunaahidi kufanya tunapobatizwa na kupokea sakramenti? (ona Mosia 5:8; M&M 20:37, 77, 79).

  • Waulize watoto nini wangefanya kuwa marafiki na mtu fulani (kwa mfano, kuzungumza nao, kufanya nao shughuli, na kuwa nao pamoja). Soma Mosia 5:13 kwa watoto. Ni nini tunaweza kufanya kumjua Yesu Kristo vizuri zaidi ili kwamba Yeye asiwe “mgeni” kwetu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 4:1–11

Ninaweza kutubu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kile inachomaanisha kutubu? Ni mistari ipi katika Mosia 4:1–11 unahisi itawasaidia?

Shughuli za Yakini

  • Andika neno msamaha ubaoni. Someni pamoja Mosia 4:1–3, na waombe watoto kutafuta maneno katika mstari wa 3 ambayo huelezea baraka zinazokuja pale tunapotubu na kupokea msamaha.

  • Waombe watoto kutaja mambo tunayolazimika kufanya ili kutubu kikamilifu na kwa dhati. Wasaidie kutafuta baadhi ya mambo haya katika Mosia 4:10, na kujadili maana ya maneno na vifungu vya maneno vinavyopatikana katika mstari huo. Shiriki hadithi inayoelezea kwa mfano kuhusu toba, pengine kutoka kwenye maisha yako mwenyewe au kutoka kwenye gazeti la Kanisa la karibuni.

  • Wasaidie watoto kutafuta maneno katika Mosia 4:6, 9, na 11 ambayo humwelezea Baba wa Mbinguni. Kwa nini ni muhimu kuelewa Baba wa Mbinguni yukoje pale tunapohitaji kutubu? Shiriki ushuhuda wako wa jinsi ulivyohisi upendo wa Mungu pale ulipotubu.

Mosia 4:12–26

Injili inanipa msukumo kuwachukulia wengine kwa upendo na ukarimu.

Mfalme Benyamini alifundisha kwamba tunapokuja kwa Kristo na kupokea ondoleo la dhambi zetu, tuna “jazwa na upendo wa Mungu” (Mosia 4:12), ambao hutuongoza kuwa wenye upendo na wakarimu kwa wengine.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kutafuta Mosia 4:13–16, 26 na kuonyesha vifungu vya maneno vinavyoelezea jinsi gani tunaweza kuwatumikia wengine. Waalike kuigiza mambo haya au kuchora picha zake, na waache watoto wengine wabahatishe kifungu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo na ukarimu nyumbani, shuleni, au kanisani?

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu ambapo walimpenda na kumtumikia mtu fulani na jinsi uzoefu huo ulivyowafanya wahisi. Ni kwa sababu zipi watu wanaweza kutotaka kuwatumikia wengine? Waulize watoto ni nini wangeweza kusema kwa mtu fulani kuwashawishi kuwasaidia watu wenye uhitaji. Wanaweza kupata mawazo katika Mosia 4:16–26.

Msichana akicheza na mtoto

Yesu Kristo alitufundisha kuwa wakarimu kwa wengine.

Mosia 5:5–15

Ninapobatizwa na kupokea sakramenti, ninajichukulia juu yangu jina la Kristo.

Wengi wa watoto unaowafundisha yawezekana wamekwishabatizwa na wanafanya upya maagano yao kupitia sakramenti. Wakumbushe kwamba sehemu muhimu ya agano lao la ubatizo ni kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Chora duara ubaoni, na weka picha ya Yesu Kristo katikati ya duara. Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe pale mnaposoma Mosia 5:8 pamoja. Ni nini mstari huu unasema tunapaswa kujichukulia juu yetu? Katika nini “tumeingia”? Waalike watoto kuandika jina la Kristo juu ya picha zao wenyewe na waweke picha ndani ya duara lenye Mwokozi. Ni maagano yapi tunafanya tunapobatizwa na kupokea sakramenti? (ona Mosia 18:8–9; M&M 20:77, 79).

  • Zungumza na watoto kuhusu kwa nini watu huweka majina yao kwenye vitu, kama vile kazi za shule, jezi za michezo, na kadhalika (ona Mosia 5:14–15). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba jina la Kristo “limeandikwa daima mioyoni [mwetu]”? (Mosia 5:12).

  • Mwalike msichana au mvulana kutoka kata yako kutembelea darasa lako na kuelezea maagano tunayofanya upya kwa kupokea sakramenti. Soma sala za sakramenti katika Mafundisho na Maagano 20:77 na 79 pamoja na watoto, ukiwaalika kutafuta vifungu vya maneno vinavyoelezea kile tunachoagana kufanya na kile Mungu anachotuahidi kama malipo.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuchora kitu walichojifunza leo na kutumia michoro yao kufundisha familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wafundishe watoto kuandika misukumo. Hata watoto wanaweza kujifunza tabia ya kuandika misukumo ya kiroho—kwa mfano, kwa kuwekea alama maandiko, kuchora picha, au kuandika kitu rahisi ndani ya shajara.