Njoo, Unifuate
Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10: “Kwa Nguvu za Bwana”


Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10: ‘Kwa Nguvu za Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Amoni akimfundisha Mfalme Limhi

Minerva K. Teichert (1888-1976), Amoni mbele ya Mfalme Limhi , 1949-1949, oil on masonite, 35 15 / 16 x 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu Cha Brigham Young, 1969.

Aprili 27–Mei 3.

Mosia 7–10

“Kwa Nguvu za Bwana”

Kwa sala soma Mosia 7–10, ukitafakari misukumo unayopokea. Ni kwa jinsi gani kweli katika sura hizi husaidia kukidhi mahitaji ya watoto unaowafundisha?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wahimize watoto kushiriki chochote wanachoweza kujua kuhusu matukio katika sura hizi. Unaweza kupata msaada katika “Mlango wa 13: Zenivu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 36–37, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 7:18–20, 33

Mungu aliwasaidia watu katika maandiko, na Yeye anaweza kunisaidia mimi.

Watu wa Limhi, ambao walikuwa katika utumwa kwa Walamani, walihitaji imani kwamba Mungu angewasaidia, hivyo Limhi aliwakumbusha juu ya nyakati ambazo Mungu aliwasaidia watu Wake.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kushiriki wakati ambapo walihitaji msaada. Elezea kwamba watu wa Mfalme Limhi walikuwa katika matatizo, hivyo alishiriki hadithi ili kuwasaidia kuwa na imani. Soma Mosia 7:19 kwa watoto, na onyesha picha ya wana wa Israeli wakivuka Bahari ya Shamu (ona Musa Akigawanya Bahari ya Shamu, ChurchofJesusChrist.org). Pitia tena hadithi hii na hadithi ya mana, na wasaidie watoto waigize hadithi hizo (ona sura ya 17 na 18 katika Hadithi za Agano la Kale, au video zinazohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani Bwana aliwasaidia watu? Shuhudia kwamba Bwana anaweza kutusaidia pia.

  • Soma Mosia 7:33 kwa watoto, na wasaidie kuelewa kile mstari unachotufundisha kufanya ili kupokea msaada kutoka kwa Bwana. Wasaidie watoto kufikiria matendo ya kuwakilisha mambo haya, na rudia mstari wakati wakifanya matendo. Ni nini baadhi ya mambo tunahitaji msaada kwayo? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba tunamwamini Bwana? Shiriki uzoefu ambapo ulimwamini Bwana na Yeye alikusaidia.

  • Chagua baadhi ya mistari ya “Hadithi za Kitabu cha Mormoni” au “Nephi’s Courage” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 118–19, 120–21) ili kuimba na watoto. Wasaidie kugundua ni kwa jinsi gani Bwana aliwasaidia watu katika Kitabu cha Mormoni. Shiriki hadithi zingine za maandiko ambazo unahisi zingewasaidia watoto kujifunza kumwamini Bwana.

Mosia 8:16–17

Mungu ametupatia manabii, waonaji, na wafunuzi.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Mosia 8:16–17 kuwafundisha watoto kuhusu kazi ya nabii kama mwonaji?

Shughuli za Yakini

  • Waonyeshe watoto jinsi ya kushikilia mikono yao juu kwenye macho yao kana kwamba walikuwa wakitazama kupitia miwani au darubuni. Soma Mosia 8:17, na waombe watoto kuvaa “miwani” zao kila mara wanaposikia neno “mwonaji.” Elezea kwamba Mungu ametupatia manabii na kwamba mojawapo ya kazi za nabii ni kuwa “mwonaji” kwa sababu anaweza “kuona” mambo yajayo. Shiriki baadhi ya mifano ya mambo ambayo manabii wameona na kutufunulia (ikijumuisha maandiko), au shiriki mfano wa wakati nabii alipokuwa akitenda kama mwonaji (kama vile 1 Nefi 11:20–21).

  • Tengeneza nyayo za karatasi, na chora juu yake picha ya mambo ambayo manabii wametushauri kufanya. Weka nyayo hizi kwenye njia kuzunguka chumba, na toa maelezo ya picha. Acha watoto wafanye zamu kuigiza kama nabii na kuwaongoza watoto wengine katika kufuata nyayo hizi.

  • Onyesha picha iliyopo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waombe watoto kuelezea kile wanachokiona. Elezea kwamba Nabii Joseph Smith alikuwa mwonaji. Bwana alimpa zana ziitwazo Urimu na Thumimu na jiwe la mwonaji kutumia katika kutafsiri Kitabu cha Mormoni.

  • Onyesha video fupi ya ujumbe wa karibuni wa mkutano mkuu kutoka kwa Rais wa Kanisa (au onyesha picha yake na soma jambo alilofundisha). Toa ushuhuda wako kwamba yeye ni nabii, mwonaji na mfunuzi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 7:18–20, 33; 9:14–19; 10:6–10, 19–21

Mungu aliwasaidia watu katika maandiko, na Yeye anaweza kunisaidia mimi.

Zenivu na watu wake, ambao walikuwa wakikaa katika ardhi ya Walamani, walikuwa wakishambuliwa na Walamani na walihitaji msaada wa Mungu. Ni nini watoto wanaweza kujifunza kutoka kwenye hadithi hii kuhusu Mungu kuwasaidia watoto Wake?

Shughuli za Yakini

  • Wagawe watoto katika makundi matatu, na alika kila kundi kujifunza mojawapo ya hadithi za maandiko zifuatazo: Waisraeli wakivuka Bahari ya Shamu (ona Kutoka 14:10–14, 21–31), familia ya Lehi ikisafiri nyikani (ona 1 Nefi 16:9–16; 17:1–6), na watu wa Zenivu wakikombolewa kutoka kwa Walamani (ona Mosia 9:14–19; 10:6–10, 19–21). Ni kwa jinsi gani watu katika hadithi hizi wanaonyesha kwamba walimwamini Mungu? Ni kwa jinsi gani Mungu aliwasaidia? Ni kwa jinsi gani Yeye hutusaidia sisi pale tunapomwamini?

  • Waalike watoto watatu kuandika jaribu au changamoto waliyonayo ubaoni. Muombe mtoto asome Mosia 7:33, na wahimize watoto wengine kufuta moja ya jaribu au changamoto kila mara wanaposikia jambo wanaloweza kufanya kupokea msaada wa Bwana. Ni kwa jinsi gani kumwamini Bwana hutusaidia kushinda changamoto zetu?

Mosia 8:12–19

Mungu hutoa manabii, waonaji, na wafunuzi kuwanufaisha wanadamu.

Tunawakubali Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha watoto kuhusu thamani ya manabii?

Shughuli za Yakini

  • Chagua maneno kadhaa muhimu kutoka Mosia 8:12–19, na yaandike ubaoni. Mwalike mtoto kusoma mistari hii, na waombe watoto wengine kunyanyua mikono yao pale wanaposikia kila neno ubaoni. Acha kusoma na jadilini kila neno kama darasa.

  • Waombe watoto kupitia tena Mosia 8:16–18 kujifunza mwonaji ni nani. Andika sentensi hii ubaoni: Mwonaji ni kama . Wasaidie watoto kufikiria jinsi ya kumalizia sentensi kuelezea kwa nini mwonaji ni baraka kwetu—kwa mfano, mwonaji ni kama mlinzi wa maisha, ambaye anatuonya kuhusu hatari.

  • Chukua kishazi kutoka Mosia 8:16–17, na kiandike ubaoni, ukibadilisha kila neno kwa alama iliyotengenezwa. Wape watoto orodha ya alama na maneno yanayowakilisha, na waache wasimbue au “kutafsiri” kishazi kama waonaji wanavyofanya. Ni kwa jinsi gani nyingine manabii, waonaji, na wafunuzi ni “faida kubwa” kwetu?? (Mosia 8:18

Mosia 9:14–18; 10:10–11

Ninapokuwa dhaifu, Bwana anaweza kuniimarisha.

Pale watoto wanapopata changamoto, wakati mwingine wanahisi wadhaifu na wasiokuwa na msaada. Tumia tukio la watu wa Zenivu kuwafundisha watoto kwamba wanaweza kupokea nguvu kutoka kwa Bwana.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kushiriki jinsi wanavyoweza kuwa imara kimwili. Inamaanisha nini kuwa na “nguvu za wanadamu”? (Ona Mosia 10:11). Inamaanisha nini kuwa na “nguvu za Bwana ”? (Ona Mosia 9:17–18; 10:10). Ni kwa jinsi gani tunapokea nguvu za Bwana?

  • Waalike watoto kuchora picha ya mtu fulani ambaye wanahisi ana nguvu za Bwana na kushiriki kwa nini walimchora mtu huyu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki pamoja na familia zao hadithi kutoka kwenye maandiko ambayo inawashawishi wao ku “weka imani [yao] kwa Mungu” (Mosia 7:19).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali yaliyo na mwongozo. Uliza maswali yanayoalika watoto kushiriki shuhuda zao kuhusu kweli za injili. Kwa mfano, kama mnajadili manabii, ungeweza kuwaomba watoto kushiriki ni kwa jinsi gani manabii wamewabariki.

Chapisha