Njoo, Unifuate
Mei 11–17. Mosia 18–24: “Tumeingia kwenye Agano na Yeye”


“Mei 11–17. Mosia 18–24: ‘Tumeingia kwenye Agano na Yeye,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 11–17. Mosia 18–24,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Watu wa Limhi wakitoroka

Minerva K. Teichert (1888-1976), Kutoroka kwa Mfalme Limhi na Watu Wake , 1949 1949, oil on masonite, 35 7 / 8 x 48 inchi. Makumbusho ya sanaa ya Chuo Kikuu Cha Brigham Young, 1969.

Mei 11–17

Mosia 18–24

Tumeingia kwenye Agano na Yeye

Unaposoma Mosia 18–24, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia kugundua kweli ambazo zitahusika kwao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya mtu akibatizwa, na waalike watoto kushiriki jambo wanalojua kuhusu ubatizo. Wangeweza kushiriki jambo walilojifunza wakati wakisoma Mosia 18–24 pamoja na familia zao, wakati wakihudhuria ubatizo, au katika mazingira mengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 18:7–16

Wakati ninapobatizwa, ninafanya agano na Mungu.

Moja ya njia ya muhimu zaidi kuwasaidia watoto kujitayarisha kwa ubatizo ni kuwafundisha kuhusu agano watakaloweka wakati wanapobatizwa.

Shughuli za Yakini

  • Pitia tena hadithi ya Alma na watu wake katika Maji ya Mormoni kwa kutumia Mosia 18:7–16 au “Mlango wa 15: Alma anafundisha na Kubatiza” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 43–44, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Onyesha picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na acha watoto wakuambie kile wanachojua kuhusu hadithi.

  • Kwa kutumia Mosia 18:8–10 kama mwongozo, wafundishe watoto kwa maneno yako mwenyewe baadhi ya mambo watakayoahidi kufanya wakati wanapobatizwa. Kwa mfano, wataahidi kumfuata Baba wa Mbinguni na Yesu kwa kuwapa faraja watu wenye huzuni. Shiriki hadithi ya jinsi wewe au mtu mwingine unayemjua alivyotunza ahadi hizi. (ona pia M&M 20:77 79; Carole M. Stephens, “Tuna Sababu Kuu ya Kushangilia,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 115–17.)

  • Eleza kwamba wakati tunapobatizwa, Baba wa Mbinguni pia anatoa ahadi kwetu. Shiriki ahadi hizi, kama ilivyoelezewa katika Mosia 18:9–10.

Mosia 18:17–28

Wakati ninapobatizwa, ninakuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo.

Wasaidie watoto kuelewa kile inachomaanisha kuwa waumini wa Kanisa kupitia ubatizo na kuthibitishwa.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtu ambaye amebatizwa karibuni kushiriki uzoefu wake. Soma Mosia 18:17, na elezea kwamba wakati tunapobatizwa tunakuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kuahidi kumfuata Yesu.

  • Waonyeshe watoto picha zinazowakilisha mambo yaliyoelezewa katika Mosia 18:17–28. Kwa mfano, picha Utawazo kwenye Ukuhani (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 106) ingeweza kuwakilisha mstari wa 18, na picha Malipo ya Zaka (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 113) ingeweza kuwakilisha mistari 27–28. Acha watoto waelezee kile wanachoona kwenye picha, na kutumia picha na mistari kuwasaidia kuona kile inachomaanisha kuwa muumini wa Kanisa.

Picha
ubatizo ndani ya bahari

Tunafanya agano na Mungu wakati tunapobatizwa.

Mosia 24:8–17

Mungu anaweza kuifanya miepesi mizigo yangu.

Ni lini Mungu amefanya mizigo yako kuwa miepesi? Fikiria jinsi unavyoweza kushiriki uzoefu na ushuhuda wako pamoja na watoto.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kufikiria matendo rahisi wanayoweza kufanya wakati ukisimulia kile kilichotokea kwa watu wa Alma katika Mosia 24:8–17. Onyesha kwamba kwa sababu Alma alichagua kufuata mafundisho ya Abinadi kuhusu Yesu, yeye na watu wake walitendewa kikatili, lakini kamwe hawakukoma kuamini katika Yesu.

  • Soma Mosia 24:14–15 kwa watoto. Jaza mfuko kwa vitu vizito (kuwakilisha mizigo), na mwalike mtoto kushikilia mfuko. Elezea kwamba pale tunapokuwa na huzuni, wagonjwa, au kuwa na matatizo mengine, inaweza kuwa kama kubeba kitu kizito. Waalike watoto kufanya zamu kumsaidia mtoto kubeba mfuko ili kwamba uwe mwepesi. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni anaweza kufanya mizigo yetu miepesi tunapotafuta msaada Wake kupitia sala, kuwatumikia wengine, na kadhalika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 18:7–16

Wakati ninapobatizwa, ninafanya agano na Mungu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa agano tunalofanya kwenye ubatizo?

Shughuli za Yakini

  • Mpe kila mtoto kipande cha karatasi. Someni pamoja Mosia 18:8–10, na waalike watoto kuandika au kuchora kwenye upande mmoja wa karatasi zao ahadi tunazofanya kwenye ubatizo na, upande mwingine, baraka Baba wa Mbinguni anazotuahidi. Waache washiriki na darasa kile wanachokipata. Wanapokuwa wakishiriki, uliza maswali kama haya: ni kwa jinsi gani tunaweza “kuomboleza na wale wanaoomboleza”? Je, inamaanisha nini kuwa shahidi wa Mungu “katika mahali popote”? (mstari wa 9). Ni nini tunaweza kufanya kutunza maagano yetu?

  • Waalike watoto kadhaa ambao wamebatizwa kushiriki kile wanachokumbuka kuhusu uzoefu wao. Ni nini kilifanya siku ile iwe ya kipekee? Walihisi vipi? Elezea kwamba kila Jumapili wanafanya upya agano lao la ubatizo pale wanapopokea sakramenti. Wasaidie watoto kulinganisha agano la ubatizo lililoelezewa katika Mosia 18:8–10 na sala za sakramenti (ona M&M 20:77, 79). Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya sakramenti kuwa muda wa kipekee, wa staha, kama vile ubatizo wetu ulivyokuwa?

  • Muombe muongofu mpya kushiriki jinsi alivyojifunza kuhusu Kanisa na jinsi ilivyokuwa kubatizwa. Waache watoto waulize maswali, kama vile nini kilimsaidia mtu yule kutaka kufanya ahadi katika Mosia 18:7–16.

Mosia 18:17–28

Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kuwa na shukrani kwa ajili ya baraka za kuwa waumini wa Kanisa?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kusoma Mosia 18:17–28, wakitafuta mafundisho ya Kanisa la Kristo katika kipindi cha Alma ambayo yanafanana katika kipindi chetu. Andika majibu yao kwenye matofali au vikombe, na waache watoto wavitumie kujenga umbile linalowakilisha Kanisa la Yesu Kristo.

  • Imba pamoja na watoto au soma maneno kwenye “Kanisa la Yesu Kristo” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77), na waalike kusikiliza mambo tunayoahidi kama waumini wa Kanisa. Wasaidie kufikiria jinsi wanavyoweza kutunza ahadi hizi.

Mosia 21:1–5, 13–16; 22:1–11; 24:8–22

Mungu anaweza kuifanya miepesi mizigo yangu.

Hadithi ya watu wa Alma inaweza kuwaonyesha watoto kwamba wakati mwingine Mungu husaidia kwa kutuimarisha kuvumilia majaribu yetu badala ya kuyaondoa. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kujifunza kutokana na hadithi hii?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kugundua matukio muhimu kutoka kwenye tukio la watu wa Limhi katika Mosia 21:1–5, 13–16; na 22:1–11 na watu wa Alma katika Mosia 24:8–22. Kisha muombe kila mtoto kuchora moja ya matukio haya. Waalike watoto kuweka michoro yao katika mpangilio sahihi ili kusimulia hadithi. Wanapofanya hivyo, sisitiza kwamba Mungu aliwasaidia watu kuvumilia mizigo yao.

  • Alika watoto wasome Mosia 21:14–15 na 24:13–14. Ni kwa jinsi gani Bwana alijibu sala za watu wa Limhi na watu wa Alma? Waombe watoto kushiriki nyakati ambapo walisali kuomba msaada kwa jaribu na Baba wa Mbinguni aliwasaidia, au shiriki uzoefu wako mwenyewe.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumuelezea mtu mwingine kile watakachoahidi au walichoahidi kufanya kama sehemu ya agano lao la ubatizo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa na usikivu kwa watoto. Kama watoto hawaonyeshi kushiriki, inaweza kuwa wakati muafaka wa kujaribu shughuli nyingine au kufanya matembezi mafupi, ya utulivu. Kwa upande mwingine, kama wanashiriki na kujifunza, usijisikie kushinikizwa kuendelea mbele ili kuhakikisha unapitia nyenzo zaidi za somo.

Chapisha