Njoo, Unifuate
Mei 18–24. Mosia 25–28: “Waliitwa Watu wa Mungu”


“Mei 18–24. Mosia 25–28: ‘Waliitwa Watu wa Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 18–24. Mosia 25–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
malaika akimtokea Alma na wana wa Mosia

Kuongoka kwa Alma Mdogo, na Gary L. Kapp

Mei 18–24.

Mosia 25–28

“Waliitwa Watu wa Mungu”

Baba wa Mbinguni anajua kile watoto katika darasa lako wanahitaji kujifunza na jinsi ya kuwafikia. Tafuta mwongozo Wake unaposoma Mosia 25–28 na kupitia tena muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha iliyopo kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waombe watoto kuelezea nini kinatendeka katika picha. Kama watoto wanaijua hadithi ya Alma Mdogo na wana wa Mosia, waache washiriki kile wanachojua.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 26:30–31

Bwana ananitaka nisamehe.

Bwana alimfundisha Alma kwamba Yeye bila kikwazo huwasamehe wale wanaotubu. Tunapaswa kufuata mfano Wake kwa kuwasamehe wale wanaotenda dhambi dhidi yetu.

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto kifungu hiki cha maneno kutoka Mosia 26:31: “Na pia nyinyi mtasameheana.” Acha watoto wafanye mazoezi kusema “nimekusamehe” mara kadhaa, na tafuta kama wanajua kile inachomaanisha kusamehe. Shiriki uzoefu kutoka katika maisha yako wakati ulipomsamehe mtu au wakati mtu alipokusamehe.

  • Wasaidie watoto kuigiza kusameheana. Muombe mtoto mmoja kujifanya kwamba amefanya jambo la kumuumiza au kumkwaza mtoto mwingine. Ni nini mtoto yule mwingine anaweza kusema au kufanya kuonyesha msamaha?

  • Waalike watoto kuchora uso wa huzuni upande mmoja wa karatasi na uso wa furaha upande wa pili. Waombe kunyanyua juu uso wa huzuni wakati wanaposimulia uzoefu pale ndugu au rafiki alipowavuruga. Waombe kunyanyua juu uso wa furaha wakati wakisimulia jinsi walivyomsamehe au watakavyomsamehe mtu yule.

Mosia 27:8–37

Injili huwasaidia watu kubadilika na kuwa zaidi kama Yesu.

Uongofu wa Alma Mdogo na wana wa Mosia unaonyesha kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo na injili Yake, mtu yeyoye anaweza kubadilika na kuwa zaidi kama Yesu.

Shughuli za Yakini

  • Kwa ufupi simulia kuhusu uongofu wa Alma Mdogo na wana wa Mosia, kama ilivyoelezewa katika Mosia 27:8–37. Kwa msaada, ona “Sura ya 18: Alma Mdogo Anatubu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 49–52, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Kisha simulia hadithi tena, ukiwaruhusu watoto kushiriki maelezo wanayokumbuka. Waache waigize hadithi, na wasaidie kuona tofauti kati ya vile Alma na wana wa Mosia walivyokuwa kabla ya kutubu na baada ya kufanya hivyo.

  • Wasaidie watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kusimulia hadithi ya Alma na wana wa Mosia. Soma Mosia 27:24, na wasaidie watoto kuelewa kwamba Alma na wana wa Mosia walibadilika kwa sababu walitubu dhambi zao na kuikubali injili ya Yesu Kristo.

    Picha
    Alma Mdogo akipelekwa kwenye nyumba ya baba yake

    Baba Yake alijawa shangwe, na Walter Rane

Mosia 28:1–8

Ninaweza kushiriki injili.

Baada ya uongofu wao, wana wa Mosia walikuwa na shauku ya kushiriki injili na kila mtu, ikijumuisha adui zao, Walamani.

Shughuli za Yakini

  • Tumia Mosia 28:1–8 kuwasimulia watoto kuhusu wana wa Mosia wakiamua kuhubiri injili kwa Walamani. Kwa msaada, ona “Sura ya 19: Wana wa Mosia Wanakuwa Wamisionari” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 53, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini walitaka kushiriki injili? (ona mstari wa 3).

  • Msaidie kila mtoto kumfikiria mtu anayehitaji kujua zaidi kuhusu injili. Wasaidie watoto kupanga kile watakachosema kwa watu waliowafikiria.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168). Onyesha vifungu vya maneno katika wimbo ambavyo vinapendekeza jinsi tunavyoweza kushiriki injili na wengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 26:22–23, 29–30; 27:8–37

Mungu bila kikwazo huwasamehe wale wanaotubu.

Kama yeyote katika darasa lako anajiuliza kama kweli anaweza kusamehewa, maneno ya Mungu kwa Alma Mkubwa na uzoefu wa Alma Mdogo vinaweza kusaidia.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kujifanya wanazungumza na mtu fulani ambaye hadhani Mungu ataweza kumsamehe. Waalike kupitia tena maneno ya Mungu kwa Alma Mkubwa katika Mosia 26:22–23, 29–30. Ni nini wanapata ambacho kingeweza kumsaidia mtu yule?

  • Kabla ya darasa, muombe mmoja wa watoto asome kuhusu uongofu wa Alma Mdogo, unaopatikana katika Mosia 27:8–37, na kuja amejiandaa kusimulia hadithi kwa darasa kama vile yeye alikuwa Alma Mdogo. (Kama itahitajika, pendekeza kwamba amuombe mzazi kusaidia.) Wakati mtoto anasimulia hadithi, uliza maswali kama vile “ni kwa jinsi gani ulihisi wakati … ?” au “Nini kilitokea baada ya hapo?”

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ya maneno kutoka Mosia 27:8–10 inayoelezea vile Alma na wana wa Mosia walivyokuwa kabla ya uongofu wao. Kisha waombe kutengeneza orodha nyingine kutoka Mosia 27:32–37 inayoelezea walivyokuwa baada ya hapo. Kulingana na mistari 24–29, nini kilisababisha badiliko hili kuu kwa Alma?

Mosia 26:29–31

Ili kusamehewa, lazima nisamehe.

Wasaidie watoto kuona uhusiano kati ya msamaha wanaotoa kwa wengine na msamaha wanaotumainia kwa ajili yao.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kusoma Mosia 26:29–31 na hesabu ni mara ngapi neno “samehe” linatokea. Ni nini mistari hii hutufundisha kuhusu kusamehe wengine? Ni kwa jinsi gani msamaha huwasaidia wote mtu aliyefanya jambo baya na mtu anayesamehe?

  • Muombe mtoto kuchora daraja ubaoni, na shiriki kauli hii iliyonukuliwa na Rais Thomas S. Monson: “Yeye ambaye hawezi kusamehe wengine huvunja daraja ambalo juu yake yeye mwenyewe lazima apite kama angetaka kufika mbinguni, kwani kila mmoja anahitaji msamaha” (George Herbert, iliyonukuliwa katika “Chembeo Zilizofichika,” Ensign, Mei 2002, 19). Futa sehemu ya daraja, na waombe watoto wakusaidie kulijenga upya, kipande baada ya kipande, wakati wakishiriki jinsi wanavyoweza kutoa msamaha kwa wengine. Waalike kumfikiria mtu wanayehitaji kumsamehe.

Mosia 27:8–24

Ninaweza kusali na kufunga kwa ajili ya Mungu kuwabariki wale ninaowapenda.

Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kufunga kunaweza kuimarisha imani yao pale wanaposali kwa ajili ya watu wanaowapenda.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Mosia 27:8–24, na uwaombe watoto kuonyesha kile Alma na watu wake walifanya kumsaidia Alma Mdogo. Shiriki uzoefu ambapo ulifunga na kusali kwa ajili ya mtu fulani, na wahimize watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe.

  • Waalike watoto kumfikiria mtu fulani wanayemjua anayehitaji msaada wa Mungu katika maisha yake. Toa ushuhuda wako kwamba watoto wanaweza kusali na kufunga kwa imani kwa ajili ya Mungu kumbariki mtu huyu. Waalike watoto kusali kwa ajili ya mtu waliyemfikiria na, kama wanaweza, kufunga kwa ajili yao pia.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto kuchagua jambo moja walilojifunza kutokana na uzoefu wa Alma Mdogo na wana wa Mosia ambalo wangependa kushiriki na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Saidia Wazazi. “Wazazi ni walimu muhimu sana wa injili kwa watoto wao—wana vyote jukumu kuu na nguvu kubwa zaidi ya kuwashawishi watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–7). Unapofundisha watoto Kanisani, kwa sala tafuta njia za kuwasaidia wazazi wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha