Njoo, Unifuate
Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4: “Walikuwa Wameimarishwa na Hawangeondolewa”


“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4: ‘Walikuwa Wameimarishwa na Hawangeondolewa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Alma Mdogo akihubiri

Alma Mdogo Akihubiri, na Gary L. Kapp

Mei 25–31.

Mosia 29–Alma 4

“Walikuwa Wameimarishwa na Hawangeondolewa”

Watoto unaowafundisha wanaweza kujifunza mengi katika darasa lako, lakini watajifunza mengi zaidi kama watajenga tabia ya kujifunza maandiko nyumbani. Fikiria ni kwa jinsi gani unaweza kuhimiza na kusaidia kujifunza injili nyumbani.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kukaa sakafuni katika duara, na zungusha mpira kwa mmoja wao. Muombe mtoto yule kushiriki jambo alilojifunza hivi karibuni kuhusu injili nyumbani au katika darasa la msingi. Kisha mwalike mtoto kuzungusha mpira kwa mwingine. Rudia hivi mpaka kila mtoto amepata nafasi ya kushiriki jambo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 1:2–9, 26–30

Kama muumini wa Kanisa, ninapaswa kuwapenda na kuwatumikia wengine.

Unaweza usichague kuwasimulia watoto mengi kuhusu mafundisho ya Nehori, lakini wangeweza kunufaika kwa kujua kwamba ndani ya Kanisa tunatumikia kwa sababu tunawapenda wengine, siyo kwa sababu tunataka kuwa matajiri au maarufu.

Shughuli za Yakini

  • Shiriki na watoto, kwa maneno rahisi, hadithi ya Alma na Nehori (ona Alma 1; “Mlango wa 20: Alma na Nehori,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 54–55, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Sisitiza kwamba japokuwa wafuasi wa Nehori walikuwa wakatili kwa waumini wa Kanisa, wengi wa waumini wa Kanisa walibaki wakarimu na wenye upendo.

  • Soma Alma 1:30 kwa watoto, na wasaidie kuelewa kwamba watu wa Kanisa walishiriki kile walichokuwa nacho na watu waliohitaji msaada. Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo ambayo wangeweza kushiriki na watu ambao wangeweza kushiriki nao mambo hayo. Wahimize watoto kuchora picha za mipango yao.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo na huduma, kama vile “Kindness Begins with Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 145), na wasaidie watoto kufikiria matendo ambayo yangeweza kwenda na wimbo.

Alma 2:28–30

Mungu atajibu maombi yangu.

Wakati Alma na Wanefi walipohisi “woga mwingi” (Alma 2:23), waliomba kwa ajili ya msaada na waliimarishwa. Wasaidie watoto kujifunza kutokana na mfano wao.

Shughuli za Yakini

  • Kwa kutumia picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au katika “Mlango wa 21: Waamlisi” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 56–57, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org), wasimulie watoto jinsi Wanefi walivyopata nguvu ya kuwashinda Waamlisi. Waulize watoto kuhusu mambo ambayo yanatisha au ni magumu kwao, na shuhudia kwamba wanaweza kusali kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya msaada kwa mambo haya.

  • Shiriki uzoefu ambapo Mungu alikusaidia baada ya kusali Kwake. Waalike watoto kushiriki uzoefu ambao wamekuwa nao kwenye sala.

Alma 4:19

Ushuhuda wangu unaweza kuwaimarisha wengine.

Mara nyingi “ushuhuda halisi” (Alma 4:19) wa mtoto unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wengine. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kupata njia za kushiriki shuhuda zao?

Shughuli za Yakini

  • Funua maandiko kwenye Alma 4:19, na elezea kwamba wakati Alma alipoona jinsi watu walivyokuwa waovu, aliamua njia nzuri zaidi ya kuwasaidia ilikuwa ni kutoa “ushuhuda halisi” kwao. Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwafundisha watoto ushuhuda ni nini na kile unachojumuisha. Wahimize kushiriki shuhuda zao.

  • Mimina maji masafi kwenye gilasi angavu, na elezea kwamba maji ni kama shuhuda zetu kwa sababu tunaweza kuzishiriki na wengine. Mimina gilasi ya maji kwenye kikombe kidogo kwa ajili ya kila mtoto, na waambie watoto kwamba tunaposhiriki shuhuda zetu, tunawasaidia wengine kuwa na shuhuda zenye nguvu pia.

  • Kama watoto wangependa, waache wafanye mazoezi kutoa shuhuda zao. Pendekeza njia kadhaa wanazoweza kuonyesha kwamba wanajua injili ni ya kweli, ikijumuisha kupitia matendo yao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 1:2–9

Ninaweza kujifunza kutambua mafundisho ya uongo.

Mahala fulani katika maisha yetu, sote lazima tukutane na watu kama Nehori—wale wanaojaribu kutudanganya kwa jumbe zinazoonekana kuvutia lakini ni za uongo na za kudhuru. Kushiriki tukio katika Alma 1:2–9 kungeweza kuwasaidia watoto kujiandaa kwa makabiliano hayo katika maisha yao.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kusoma Alma 1:2–4 kupitia upya baadhi ya mambo ambayo Nehori, mwalimu wa uongo, alifundisha. Wasaidie kutengeneza chemsha bongo ya kauli za kweli-au-si kweli kutoka kwenye mistari hii. Je, ni kwa nini Shetani wakati mwingine huchanganya kweli na uongo? Wasaidie watoto kufikiria baadhi ya mifano.

  • Baada ya kupitia tena Alma 1:2–9 kwa pamoja, muombe kila mmoja wa watoto kusoma moja ya maandiko yafuatayo: Mathayo 7:21–23; 2 Nefi 26:29–31; Mosia 18:24–26; na Helamani 12:23–26. Ni kwa jinsi gani maandiko haya yanakanusha mafundisho ya Nehori? Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia maandiko kuimarisha shuhuda zetu wenyewe za injili?

Alma 1:26–30; 4:6–13

Kama muumini wa Kanisa, ninapaswa kuwapenda na kuwatumikia wengine.

Wakati mwingine waumini wa Kanisa katika wakati wa Alma walikuwa wakarimu na wenye kutoa, na wakati mwingine walikuwa si wakarimu na wenye kiburi. Wasaidie watoto unaowafundisha kujifunza kutokana na uzoefu wao.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kusoma Alma 4:6–13, na kutoa maana ya maneno kama “kutesa,” “kufanyia madharau,” na “kudharau” (tumia kamusi ikibidi). Je, tunajisikiaje pale watu wanapotuchukulia kwa namna hizi? Waalike watoto kutafuta maneno katika Alma 1:26–30 ambayo yanaelezea jinsi Baba wa Mbinguni anavyotaka sisi tuchukuliane.

  • Waombe watoto kusoma Alma 1:27, 30 na tengeneza orodha ya aina za watu waliosaidiwa na waumini wa Kanisa. Waalike watoto kuwafikiria watu katika ujirani wao au mashuleni ambao wangeweza “[kuwa] katika uhitaji” (Alma 1:30) wa upendo na msaada wao. Kuimarisha kanuni hii, imbeni pamoja wimbo kuhusu ukarimu, kama vile “I’ll Walk with You” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41 ).

Alma 4:8–20

Ushuhuda wangu unaweza kuwaimarisha wengine.

Alma alijiuzulu cheo chake kama mwamuzi mkuu ili kutumia muda mwingi zaidi kushiriki ushuhuda wake na kuwasaidia watu kutubu. Mfano wake ungeweza kuwashawishi watoto kushiriki shuhuda zao mara kwa mara.

Shughuli za Yakini

  • Soma Alma 4:8–12, 15 pamoja na watoto, na waombe kuonyesha matatizo yaliyokuwa yakitokea Kanisani, kama ilivyoelezewa katika mistari hii. Waalike watoto kupendekeza baadhi ya mambo Alma angeweza kufanya kutatua matatizo haya. Wasaidie kupata, katika Alma 4:16–20, kile Alma alichoamua kufanya. Je, kwa nini ushuhuda una nguvu kubwa?

  • Kuwasaidia watoto kuelewa ushuhuda ni nini na kile unachojumuisha, onyesha video “Filamu ya Ushuhuda wa Mtume” (ChurchofJesusChrist.org); imbeni pamoja wimbo kuhusu mada, kama vile “Testimony” (Nyimbo za Kanisa, na. 137); au tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waombe watoto kushiriki kile walichojifunza kuhusu manabii kutoka kwenye shughuli hizo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kumfikiria mtu wanayeweza kushiriki nae shuhuda zao wiki ijayo. Wahimize kuandika mpango kuwasaidia kufikia lengo lao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali ambayo yanavutia ushuhuda. “Kuuliza maswali ambayo yanahimiza wanafunzi kushiriki ushuhuda kuhusu kanuni ambazo zinafundishwa inaweza kuwa njia yenye nguvu ya kumwalika Roho” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 32). Kuwaalika watoto kutoa shuhuda, uliza maswali yanayowashawishi kufikiria kuhusu na kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi au injili Yake. Ungeweza pia kuuliza kuhusu uzoefu waliokuwa nao kwenye sala, huduma, ibada kama ubatizo, au kuhisi ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Chapisha