Njoo, Unifuate
Mei 4–10. Mosia 11–17: “Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza”


“Mei 4–10. Mosia 11–17: ‘Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 4–10. Mosia 11–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Abinadi akimshuhudia Mfalme Nuhu

Abinadi Mbele ya Mfalme Nuhu, na Andrew Bosley

Mei 4–10

Mosia 11–17

“Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza”

Tafakari na sali kujua jinsi gani unaweza kutumia hadithi ya Abinadi na mafundisho yake katika Mosia 11–17 kuwasaidia watoto unaowafundisha. Andika misukumo unayopokea.

Andika Misukumo Yako

Ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waruhusu watoto kushiriki kile wanachokijua kuhusu hadithi ya Abinadi na Mfalme Nuhu. Picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ingeweza kusaidia.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 11–1317

Ninaweza kusimamia ukweli, hata kama ninasimama peke yangu.

Wote Abinadi na Alma walikuwa na ujasiri katika kutetea ukweli. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia hadithi hii kujenga ujasiri wa watoto kwa nyakati ambazo wangetakiwa kutetea imani zao?

Shughuli za Yakini

  • Fupisha tukio la Abinadi, Mfalme Nuhu, na Alma inayopatikana katika Mosia 11–13 na 17. Ungeweza kutumia “Sura ya 14: Abinadi na Mfalme Nuhu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 38-42, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kuigiza tukio, ukiwapa zamu kuigiza majukumu tofauti.

  • Tembea na watoto pale wanapoimba wimbo unaoshawishi ujasiri, kama vile “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162). Someni maneno ya wimbo pamoja, na wasaidie watoto kutambulisha kile mtu shujaa au jasiri hufanya. Chagua mistari michache kutoka Mosia 11–13 na 17 kuwasomea watoto kuonyesha jinsi Abinadi na Alma walivyokuwa jasiri (kwa mfano, ona Mosia 13:1–4, 9).

Mosia 12:33–36; 13:11–24

Ninapaswa kutii Amri Kumi.

Makuhani wa Mfalme Nuhu walizijua amri lakini hawakuzifuata. Maneno ya Abinadi yanaweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kutii amri.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuhesabu mpaka 10. Au wapatie vipande vya karatasi vyenye namba mpaka 10 na waache waweke karatasi hizo katika mpangilio. Elezea kwamba Baba wa Mbinguni alitupatia Amri Kumi kutusaidia kurudi kuishi Naye. Wasaidie watoto kukariri pamoja nawe baadhi ya Amri Kumi kutoka Mosia 12:33–36 na 13:11–24.

  • Onyesha picha ya Musa akiwa na Amri Kumi (kama vile Kitabu cha Picha za Injili, na. 14), na kwa ufupi elezea jinsi Musa alivyopokea amri kutoka kwa Mungu (ona Kutoka 19–20). Kisha onyesha picha ya Abinadi (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia), na waambie watoto kwamba Abinadi alimkumbusha Mfalme Nuhu na makuhani wake kuhusu Amri Kumi. Chagua amri chache kutoka Mosia 12:33–36 na 13:11–24 ambazo unahisi ni muhimu hasa kwa watoto unaowafundisha, na jadili pamoja nao baraka zinazokuja kwa kutii amri hizo.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu amri, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146). Ni kwa nini tunatii amri?

Mosia 14:5; 15:7–9

Manabii kwa ushujaa wanashuhudia juu ya Yesu Kristo.

Abinadi alimfundisha Mfalme Nuhu na wengine kuhusu Yesu Kristo, hata pale ilipokuwa ya kuhatarisha. Ni kwa jinsi gani tukio la Abinadi huimarisha shuhuda za watoto juu ya manabii?

Shughuli za Yakini

  • Shiriki na watoto baadhi ya mambo Abinadi aliyofundisha kuhusu Yesu Kristo katika Mosia 14:5 na 15:7–9. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Abinadi alitaka Mfalme Nuhu na watu wake kumfuata Yesu ili waweze kuwa na furaha. Katika siku yetu, manabii wanaoishi hutufundisha kuhusu Mwokozi. Soma dondoo kutoka mkutano mkuu, au shiriki video fupi ya mmojawapo wa manabii wanaoishi akishiriki ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo (kwa mfano, ona “Mashahidi Maalumu wa Kristo” video kwenye ChurchofJesusChrist.org).

  • Onyesha au chora picha ya minyororo, gereza, na moto. Wafundishe watoto kwamba Abinadi alikuwa tayari kufungwa, kuwekwa gerezani, na hata kuunguzwa kwa moto ili kushiriki ushuhuda wake wa Yesu Kristo. Hata kama pengine kamwe hatutakumbana na hatari hizi, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa majasiri kama Abinadi katika kushiriki shuhuda zetu kwa vyote maneno yetu na chaguzi zetu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 11–1317

Ninaweza kusimamia ukweli, hata kama ninasimama peke yangu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwaandaa watoto unaowafundisha kwa ujasiri kusimamia ukweli, hata kama lazima wafanye hivyo peke yao?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchora picha za sehemu tofauti za tukio la Abinadi, Mfalme Nuhu, na Alma zinazopatikana katika Mosia 11–13 na 17. Wasaidie kutumia picha zao kusimulia tena hadithi, au tumia “Sura ya 14: Abinadi na Mfalme Nuhu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 38–42, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani Abinadi na Alma kila mmoja alisimamia ukweli? Je, ni kwa nini Mfalme Nuhu hakusimamia ukweli? (ona Mosia 17:11–12.) Wasaidie watoto kufikiria nyakati ambazo walisimamia kwenye kilicho kweli.

  • Wasaidie watoto kufikiria tukio ambapo wangeweza kusimamia ukweli, na waalike kuigiza baadhi ya nyakati hizi. Kwa mfano, ni nini wangeweza kufanya pale mtu anapojaribu kuwafanya waangalie sinema isiyofaa au pale rafiki zao wanapokataa kumjumuisha mtu mwingine katika mchezo wanaocheza?

  • Onyesha video “Thubutu Kusimama Peke yako” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani Rais Thomas S. Monson alikuwa kama Abinadi?

Mosia 12:33–36; 13:11–24

Ninapaswa kutii Amri Kumi.

Abinadi alimfundisha Mfalme Nuhu na makuhani wake waovu kuhusu Amri Kumi. Je, watoto unaowafundisha wanaelewa kwa nini tunapaswa kupenda na kutii amri za Mungu?

Shughuli za Yakini

  • Mpangie kila mtoto kusoma moja ya amri katika Mosia 12:35 na 13:11–24. Wasaidie watoto kufikiria njia za ubunifu kusaidiana kila mmoja kukumbuka kila amri (kama vile wimbo wa kifungu cha maneno, tendo, au ufupisho). Wimbo “The Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 112) unaweza pia kusaidia. Wape watoto vipande vya karatasi vyenye umbo la moyo, na waalike kuandika moja au zaidi ya Amri Kumi juu ya mioyo yao (ona Mosia 13:11)—pengine ile wanayohisi wanapaswa kuweka juhudi kubwa kuitii.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu amri, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146 ). Ni baraka zipi zinatokana na kutii amri?

baba na  mwanaye wakisoma maandiko

Maandiko yanatufunza amri za Mungu.

Mosia14:6; 16:4–9

Ninapofanya dhambi, ninakuwa nimepotea; kwa sababu ya Yesu Kristo, ninaweza kurejea.

Akifundisha kuhusu Yesu Kristo, Abinadi alimnukuu nabii Isaya, ambaye alitufananisha na kondoo aliyepotea. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mfanano huu kuwafundisha watoto kuhusu Mwokozi?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu ambapo walipoteza kitu au walipotea wao wenyewe. Walihisi vipi? Walifanya nini? Someni pamoja Mosia 14:6 na 16:4–9. Ni kwa jinsi gani sisi wakati mwingine “hugeuka” kutoka kwa Mungu? Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo hutusaidia kurudi?

  • Waalike watoto kufikiria kundi la kondoo. Ni kwa sababu zipi mmoja wa kondoo angeweza kupotea? Orodhesha majibu yao ubaoni. Ni kwa jinsi gani sisi ni kama kondoo wanaotangatanga? Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni angeweza kuhisi pale “tunaporejea” kupitia toba na Upatanisho wa Mwokozi? (ona M&M 18:10–13). Shiriki ushuhuda wako wa Mwokozi na wa toba.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwaomba wanafamilia wao kushiriki uzoefu ambapo walisimamia ukweli, au wahimize watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Marudio ni muhimu katika kujifunza. Watoto wananufaika kwa kusikia kanuni ya injili au kufanya shughuli zaidi ya mara moja. Jaribu kurudia shughuli katika njia tofauti tofauti.