Njoo, Unifuate
Juni 1–7. Alma 5–7 : “Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?”


“Juni 1–7. Alma 5–7: ‘Mmeshuhudia mabadiliko haya makuu katika mioyo yenu?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 1–7. “Mmeshuhudia mabadiliko haya makuu katika mioyo yenu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Yesu akiwa amembeba mwana kondoo

Hamjasahauliwa, na John McNaughton

Juni 1–7.

Alma 5–7

“Mmeshuhudia mabadiliko haya makuu katika mioyo yenu?”

Kwa sala fikiria kanuni katika Alma 5–7 ambazo unahisi zinahusika hasa kwa watoto unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki kile wanachokumbuka kujifunza kuhusu Alma Mdogo wiki chache zilizopita. Elezea kwamba baada ya Alma kuongoka, aliwafundisha watu mambo muhimu kuhusu injili. Waache watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu mambo aliyofundisha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 5:44–48

Ninaweza kupata ushuhuda wangu mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu.

Watoto unaowafundisha wanaweza kujenga shuhuda zao imara, hata wakati wakiwa wadogo.

Shughuli za Yakini

  • Tumia picha ya Alma Mdogo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 77) ili kupitia tena tukio la malaika akimtembelea (ona Mosia 27). Kisha waombe watoto kuelezea ushuhuda ni nini, na wasaidie penye ulazima. Elezea kwamba Alma alifanya kazi kupata ushuhuda baada ya malaika kumtembelea. Taratibu soma Alma 5:46 mara kadhaa, na waalike watoto kusikiliza kile Alma alichofanya na jinsi alivyojua ukweli. (Unaweza kuhitajika kuelezea kwamba kufunga humaanisha kutokula chakula na kunywa maji.)

  • Onyesha picha ya vitu vinavyokua taratibu na vinahitaji matunzo thabiti, kama mmea au mtoto wa mnyama. Waombe watoto kushiriki jinsi tunavyovitunza vitu hivi na kuvisaidia kukua. Wakumbushe kwamba lazima pia daima tutunze shuhuda zetu.

  • Tumia puto tupu kuwakilisha ushuhuda na jaza hewa ndani yake kila mara unaposhiriki jambo ambalo husaidia shuhuda kukua. Funga puto na litoe kwa kila mtoto, ukiwaomba watoto kushiriki jambo moja wanaloweza kufanya kusaidia shuhuda zao kukua. Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe wakifanya mambo ambayo yataimarisha shuhuda zao.

wavulana wawili pamoja na watoto wa wanyama

Tunapoikubali injili, ni kama kuanza maisha mapya.

Alma 7:10–13

Mwokozi alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu, na mateso.

Kweli katika Alma 7:10–13 zinaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Yesu Kristo anawajali na anaweza kuwasaidia.

Shughuli za Yakini

  • Waonyeshe watoto picha ya Yesu. Elezea kwamba Yeye anajua vile ilivyo kuumizwa, kuwa na huzuni, au kuogopa. Soma baadhi ya maneno katika Alma 7:11–13 ambayo huelezea kile Mwokozi alichoteseka, na elezea maneno ambayo watoto wangeweza kutoyaelewa. Onyesha kwamba Yesu anaweza kutusaidia na kutufariji pale tunapokuwa na huzuni. Shiriki jinsi ambavyo Mwokozi amekusaidia na kukufariji.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu ambapo walikuwa wagonjwa au katika maumivu au walikuwa na tatizo lingine ambalo liliwafanya wawe na huzuni. Toa ushuhuda wako kwamba Mwokozi ameteseka mambo hayo na anajua jinsi ya kutusaidia.

Alma 7:19–20

Njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo imenyooka.

Unawezaje kutumia maelezo ya Alma ya njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni kuwasaidia watoto kujifunza kufanya chaguzi nzuri?

Shughuli za Yakini

  • Soma Alma 7:19 kwa watoto, na elezea kwamba tunapofanya chaguzi nzuri, tunakua katika njia inayoongoza kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Wape watoto mfuatano wa chaguzi au matendo (kama vile kutokuwa mkarimu kwa wana familia au kuwatumikia). Waombe wakuambie kama kila uchaguzi ni mzuri na unaongoza kurudi kwa Mungu au kama ni mbaya na unaongoza mbali na Yeye.

  • Soma Alma 7:20 na wasaidie watoto kuelewa maneno katika mistari hii ambayo huelezea njia ya kurudi kwa Mungu. Chora ubaoni njia iliyonyooka kutoka kwetu kwenda kwa Baba wa Mbinguni. Kisha chora njia kombo ambayo inajumuisha miisho isiyoendelea ambayo huongoza mbali na Mungu. Waalike watoto kufuatisha njia zote kwa vidole vyao. Njia ipi ni nzuri zaidi? Wasaidie kufikiria juu ya chaguzi nzuri ambazo zitawasaidia kubaki kwenye njia iliyonyooka.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 5:12–14, 27–28, 57; 7:14–24

Sina budi kuzaliwa upya na kisha kuifuata njia inayoongoza kurudi kwa Mungu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kile inachomaanisha kuzaliwa upya?

Shughuli za Yakini

  • Waonyeshe watoto picha ya mtoto mchanga, na waalike kuzungumza kuhusu vile mtoto anavyokuwa anapokuwa amezaliwa mara ya kwanza. Mwalike mtoto asome Alma 5:14. Kuwasaidia watoto kuelewa kile inachomaanisha “kuzaliwa … kiroho katika Mungu,” waombe kufikiria kuhusu vile Alma Mdogo alivyokuwa kabla hajaongoka. Alikuwa vipi baada ya kuongoka? (Ona Mosia 27:23–32 na Alma 36:12–24.) Elezea kwamba tunapokuwa na imani katika Yesu Kristo na kuishi injili Yake, ni kana kwamba tumeanza maisha mapya, kama alivyo mtoto.

  • Someni pamoja Alma 7:19, na elezea kwamba baada ya kuwa tumezaliwa upya, lazima tufuate “njia ile inayoelekea katika ufalme wa Mungu.” Ficha karatasi kuzunguka chumba zikiwa na marejeleo yafuatayo ya maandiko yameandikwa juu yake: Alma 5:12–13, 27–28, 57; 7:14–16, 23–24. Waalike watoto kutafuta karatasi, kuangalia maandiko, na kushiriki kile ambacho kila andiko hufundisha kwamba ni lazima tufanye ili kurudi katika uwepo wa Mungu.

Alma 5:14, 44–48

Ninaweza kupata ushuhuda wangu mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu.

Alma alitembelewa na malaika, lakini ushuhuda wake “ulifanywa kujulikana [kwake] na Roho Mtakatifu” (Alma 5:46).

Shughuli za Yakini

  • Soma pamoja na watoto Alma 5:44–46. Ni nini Alma alifanya kupata ushuhuda wake mwenyewe wa injili? Mpatie kila mtoto kipande cha karatasi, na waalike kutengeneza mpango wa kufanya jambo moja wiki hii kuimarisha shuhuda zao.

  • Pitisha kioo na waache watoto kutazama mfano wao wakati ukisoma Alma 5:14. Je, inamaanisha nini kupokea mfano wa Mwokozi katika nyuso zetu? Shiriki nyakati ambapo mtu alisema au kufanya jambo ambalo lilikukumbusha juu ya Mwokozi, na waombe watoto kufanya vivyo hivyo.

Alma 7:10–13

Mwokozi alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu, na mateso.

Unapojifunza Alma 7, tafakari jinsi unavyoweza kujenga imani ya watoto katika Yesu Kristo ili kwamba waweze kumgeukia Yeye katika majaribu yao.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kusoma Alma 7:11–13, wakitafuta mambo ambayo Yesu Kristo aliteseka. Wanaweza kuwa tayari kushiriki uzoefu wakati walipohisi maumivu, magonjwa, au mateso. Kulingana na mistari hii, ni kwa nini Mwokozi alikuwa radhi kuteseka haya yote? (Elezea kwamba “kusaidia” humaanisha “kutoa msaada.”)

  • Waambie watoto kuhusu ugonjwa, dhara, au mateso mengine ambayo umekuwa nayo, na waulize kama wamepitia jambo sawa na hayo. Someni pamoja Alma 7:11–13, na onyesha kile Yesu alichoteseka kwa ajili yetu. Wasaidie watoto kufikiria nyakati ambapo Mwokozi alipitia mambo haya, kama vile wakati alipojaribiwa (ona Matthew 4:1–11) au wakati alipoteseka katika Gethsemane. Ni jinsi gani inasaidia sisi kujua kwamba Yesu anaelewa masumbuko yetu? Shiriki ushuhuda wako wa nguvu ya Yesu kwenye kufariji, kusaidia, na kutuponya

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuning’iniza picha ya Yesu mahala ambapo wataiona mara kwa mara ili kuwakumbusha kile walichojifunza kuhusu Yeye leo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kujiboresha kama Mwalimu Aliye kama Kristo. Kama mwalimu, ni muhimu kutafakari jinsi unavyoweza kuongeza uwezo wako kuwasaidia watoto kujenga imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Fikiria kutumia maswali ya kujitathmini kibinafsi kwenye ukurasa wa 37 wa Kufundisha katika Njia ya Mwokozi.