Njoo, Unifuate
Juni 22–28. Alma 17–22 : “Nitawafanya Muwe Chombo”


“Juni 22–28. Alma 17–22: ‘Nitawafanya Muwe Chombo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 22–28. Ufunuo 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Alma akizungumza na Mfalme Lamoni

Amoni na Mfalme Lamoni, na Scott M. Snow

Juni 22–28

Alma 17–22

“Nitawafanya Muwe Chombo”

Kama vile Lamoni na wenzake katika tukio hili walivyokuwa na uzoefu wa kiroho wa kubadilisha maisha, watoto unaowafundisha wanaweza kuwa na uzoefu wa kiroho wa maandiko ambao utashawishi maisha yao kwa miaka mingi ijayo. Weka wazo hili akilini unapotafakari jinsi utakavyowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha inayoeleza kwa mchoro tukio katika Alma 17–22 (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waombe watoto wakuambie kile wanachoona katika picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 17–19

Ninaweza kushiriki injili pamoja na wengine.

Ni kwa jinsi gani mfano wa wana wa Mosia unashawishi darasa lako kushiriki shuhuda zao na wengine?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kuigiza hadithi ya Amoni katika Alma 17–19. Ungeweza pia kurejelea “Mlango wa 23: Amoni: Mtumishi Mkuu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 64–68, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Kama unadhani watoto wangeifurahia, leta mavazi na vitu rahisi. Waambie watoto kile unachojifunza kutoka kwenye hadithi na waalike kufanya vivyo hivyo.

  • Onyesha chombo au kifaa, na zungumza na watoto kuhusu kinatumika kufanya nini. Ni vifaa gani vingine watoto wanavijua? Waalike kujifanya kutumia kifaa. Elezea kwamba kama vile tunavyotumia vyombo au vifaa ili mambo yafanyike, Baba wa Mbinguni anaweza kututumia kuifanya kazi Yake. Soma Alma 17:11, na elezea kwamba Amoni na kaka zake walikuwa vyombo vya Baba wa Mbinguni kuwasaidia Walamani kujifunza injili.

  • Waalike watoto kukimbia mahali walipo na kujifanya kubisha milangoni wakati ukisimulia hadithi ya Abishi akienda nyumba hadi nyumba kuwaambia watu kuhusu nguvu ya Mungu (ona Alma 19:16–34). Wasaidie watoto kufikiria jinsi wanavyoweza kuwa kama Abishi na kushiriki injili pamoja na wengine.

  • Waalike wanafunzi kuchora picha zao wenyewe wakishiriki injili na mtu fulani. Wasaidie kufikiria juu ya mambo mahususi wanayoweza kushiriki. Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168). Wapatie nafasi ya kushiriki hisia zao kuhusu mambo Amoni aliyofundisha.

Alma 17:21–25; 20:9–27

Ninaweza kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo kwa kuonyesha upendo wangu kwao.

Upendo na huduma ya Amoni vililainisha moyo wa Mfalme Lamoni na baba yake. Ni nini watoto wanaweza kujifunza kutoka kwenye matukio haya?

Shughuli za Yakini

  • Fanya ufupisho wa Alma 17:21–25 kwa watoto, ukisisitiza kwamba Amoni alitaka kumtumikia Lamoni. Waalike watoto kushiriki uzoefu wakati walipomtumikia mtu fulani. Wakumbushe watoto kwamba huduma kuu ya Amoni ilimsaidia Mfalme Lamoni kutaka kujifunza kuhusu injili (ona Alma 18:15–23). Waalike watoto kumfikiria mtu fulani wanayeweza kumtumikia leo, na jadili ni kwa jinsi gani wanaweza kumtumikia mtu huyo.

  • Wasimulie watoto tukio katika Alma 20:8–27. Unaweza kutumia “Mlango wa 24: Amoni Anakutana na Baba wa Mfalme Lamoni” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 69–70, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto kufikiria juu ya matendo tofauti wanayoweza kufanya kila mara unapotaja Amoni, Lamoni, au baba ya Lamoni. Onyesha kwamba sababu moja iliyofanya moyo wa baba wa Lamoni kubadilika ilikuwa ni kwa sababu Amoni alimpenda sana Lamoni. Waalike watoto kuchora picha ya jambo wanaloweza kufanya kuonyesha upendo kwa mtu fulani.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 17:1–4

Ushuhuda wangu unakua pale ninaposoma maandiko, kusali, na kufunga.

Wana wa Mosia walikuwa imara katika injili na wakawa wamisionari wenye uwezo mkubwa kwa sababu kwa bidii walijifunza maandiko, walisali, na walifunga. Mambo sawa na haya yanaweza pia kuwasaidia watoto unaowafundisha.

Shughuli za Yakini

  • Leta darasani vitu vinavyowakilisha maandiko, sala, na kufunga, kama vile maandiko, picha ya mtu akisali, na picha ya chakula, na elezea kile ambacho kila kimoja kinawakilisha. Soma Alma 17:1–4, na waulize watoto ni kwa jinsi gani vitu hivi viliwasaidia wana wa Mosia. Ni kwa jinsi gani kusoma maandiko, kusali, na kufunga hutusaidia kuja karibu na Baba wa Mbinguni?

  • Tumia kielezo cha mada nyuma ya Kitabu cha Nyimbo za Watoto kuwasaidia watoto kutafuta nyimbo kuhusu kujifunza maandiko na sala. Imbeni baadhi ya nyimbo hizi pamoja, na wasaidie watoto kuonyesha kile ambacho nyimbo hizi hufundisha kuhusu ni kwa jinsi gani kufanya mambo haya hutubariki.

Alma 17:1–18; 22:1–3

Ninaweza kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo kwa kuonyesha upendo wangu kwao.

Hamu ya Amoni kuwa mtumishi wa Lamoni hatimaye ilipelekea kwenye fursa ya kumfundisha Lamoni wakati moyo wake ulipokuwa umefunguliwa na tayari kupokea injili.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kusoma mistari kutoka Alma 17:21–39 ambayo husimulia tukio la huduma ya Amoni kwa Mfalme Lamoni. Waalike watoto kuchora picha za watu au matukio katika hadithi na kisha kusimulia hadithi hiyo kwa maneno yao wenyewe. Wasaidie watoto kuona jinsi huduma ya Amoni ilivyomshawishi mfalme (ona Alma 18:9–23). Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio hili kuhusu jinsi ya kuwasaidia wengine kujifunza zaidi kuhusu injili?

    Picha
    Amoni akiwanusuru kondoo wa mfalme

    Minerva K. Teichert (1888-1976), Amoni anaokoa makundi ya kondoo ya mfalme, 1935-1945, oil on masonite, 35 x 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu Cha Brigham Young

  • Soma Alma 22:1–3, na uwaombe watoto kusikiliza ni kwa jinsi gani mfano mzuri wa Amoni ulimuathiri baba ya Mfalme Lamoni. Waalike kumfikiria mtu fulani wanayemfahamu ambaye anahitaji kujua kuhusu injili. Pendekeza kwa watoto kwamba upendo wao na mfano wao mzuri ungeweza kumsaidia mtu huyu kuona jinsi gani injili ilivyo nzuri. Wasaidie watoto kufikiria njia ambazo wao wanaweza kuwa mifano mizuri na kuonyesha upendo kwa watu waliowafikiria.

  • Waalike wamisionari wa muda wote au mmisionari aliyerudi karibuni kushiriki hadithi ya Amoni katika Alma 17–18. Waombe kushiriki kile walichojifunza kuhusu kazi ya umisionari kutoka kwa Amoni na jukumu ambalo huduma ilifanya katika juhudi zao. Jadili na watoto jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa Amoni.

  • Kama darasa, andikeni orodha ubaoni ya mambo watoto wanayoweza kufanya kuwatumikia wanafamilia wao. Ni kwa jinsi gani kufanya matendo haya ya huduma hubariki familia nzima?

Alma 18:24–43; 19:16–34

Ninaweza kushiriki injili pamoja na wengine.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia matukio katika mistari hii kuwashawishi watoto kuwa wamisionari kama Amoni na Abishi walivyokuwa?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha zinazowakilisha baadhi ya kweli Amoni alizoshiriki na Mfalme Lamoni zinazopatikana katika Alma 18:24–40 (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Waalike watoto kujifanya kuwa wamisionari na kushiriki kile wanachojua kuhusu kweli hizi na kila mmoja wao.

  • Soma tukio la Abishi pamoja na watoto (ona Alma 19:16–20, 28–29). Waalike watoto kufanya zamu kujifanya kuwa kama Abishi kwa kubisha hodi kwenye mlango wa darasa na kushuhudia juu ya kile kilichotokea katika Alma 19:1–17. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Abishi na kushuhudia juu ya kweli tunazozijua?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kwa sala kuweka lengo na familia zao la kushiriki injili na mtu fulani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia mialiko ya kutenda. Unapowaalika watoto kutenda katika kile wanachojifunza, fuatilia mwaliko huo wakati wa darasa lijalo. Hii inawaonyesha watoto kuwa unajali kuhusu jinsi gani injili inavyobariki maisha yao. Wanaposhiriki uzoefu wao, wataimarishwa na watasaidiana kuishi injili (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Chapisha