Njoo, Unifuate
Juni 8–14. Alma 8–12: “Yesu Kristo Atakuja Kuwakomboa Watu Wake”


“Juni 8–14. Alma 8–12: ‘Yesu Kristo Atakuja Kuwakomboa Watu Wake,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Juni 8–14. Alma 8–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Alma akihubiri

Kufundisha Mafundisho ya Kweli, na Michael T. Malm

Juni 8–14.

Alma 8–12

“Yesu Kristo Atakuja Kuwakomboa Watu Wake”

Unaposoma kile Alma na Amuleki walichowafundisha watu wa Amoniha, ni nini kinaonekana kuhusika hasa kwa watoto unaowafundisha?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuelezea kile wamisionari wanachofanya na kukuambia kuhusu mtu yeyote wanayemjua anaetumikia misheni. Ni nini wamisionari huwafundisha watu? Wasaidie watoto kuona kwamba Alma na Amuleki walikuwa wamisionari walioshiriki injili na watu wa Amoniha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 8

Ninaweza kushiriki injili.

Alma alisafiri kote katika nchi kuhubiri injili, na Amuleki alihubiri katika mji wake kwa rafiki zake na majirani. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kufuata mfano wao na kushiriki injili na wengine?

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja nusu ya kwanza ya “Mlango wa 22: Misheni ya Alma huko Amoniha” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 58-63, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kuunganisha mikono katika jozi na kujifanya kuwa Amuleki na Alma, ambao walifundisha injili pamoja, pale wanapoimba wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168).

  • Wasaidie watoto kurudia ukweli wa injili mara kadhaa, kama vile “Kitabu cha Mormoni hushuhudia juu ya Kristo” au “ninajua Yesu ananipenda.” Kisha mwalike kila mtoto kufanyia mazoezi kushiriki ukweli huu na mtu mwingine darasani. Kama sehemu ya shughuli hii, ungeweza kuwasaidia watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

  • Waombe watoto wakuambie kuhusu jambo ambalo wameshiriki na mwanafamilia au rafiki—kama vile mwanasesere au peremende. Wasaidie kuorodhesha baadhi ya mambo muhimu tunayoweza kushiriki na wengine kuhusu Yesu Kristo. Elezea kwamba kwa sababu injili ni ya muhimu sana, Alma alikwenda kuishiriki na watu katika miji mingine mingi ili kwamba wangeweza kujifunza jinsi ya kuwa na furaha.

Alma 8:18–22

Ninaweza kuwa rafiki mzuri.

Huduma ya Amuleki kwa Alma ni mfano mzuri kwa watoto wa jinsi wanavyoweza kuwapenda na kuwatumikia wengine.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtoto mmoja kujifanya kuwa Amuleki na mtoto mwingine ajifanye kuwa Alma pale unaposimulia hadithi katika Alma 8:18–22. Acha watoto wakusaidie kusimulia hadithi, na waalike watoto tofauti kuwa Alma na Amuleki. Ni kwa jinsi gani Amuleki alikuwa rafiki mzuri wa Alma? Waombe watoto kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo mtu fulani amekuwa rafiki kwao. Ni jinsi gani uzoefu huo uliwafanya wajihisi? Je, ni kwa nini Mungu anatutaka tuwe marafiki wazuri kwa wengine?

  • Tafuta au chora picha inayowakilisha urafiki (kama vile watu wawili wakikumbatiana au moyo), na ikate katika vipande vya fumbo. Nyuma ya kila kipande cha fumbo, andika kitu ambacho Alma na Amuleki walifanya kuwa marafiki wazuri au mambo tunayoweza kufanya kuwa rafiki mzuri. Waalike watoto kufanya zamu kuchagua kipande na kukiongeza kwenye fumbo wakati unasoma kile kilichoandikwa nyuma yake. Wasaidie kufikiria watu wanaoweza kufanya nao urafiki. Shuhudia kuwa Yesu Kristo ni rafiki mkuu tunayeweza kuwa naye.

wasichana wawili wakicheka

Tunaweza kuwa marafiki wazuri kwa wengine.

Alma 11:43–44

Baada ya kifo, nitafufuka.

Amuleki aliwafundisha watu wa Amoniha kuhusu ufufuo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa inamaanisha nini kufufuka?

Shughuli za Yakini

  • Tumia mkono wako kuwakilisha roho, na tumia glavu kuwakilisha mwili. Toa mkono wako nje ya glavu kuwaonyesha watoto kwamba roho na miili yetu vitatenganishwa kwenye kifo. Kisha weka mkono wako ndani ya glavu tena kuonyesha kwamba roho na miili yetu itaunganishwa tena kwenye ufufuo. Acha watoto wafanye zamu kuvaa na kuvua glavu wakati unasoma Alma 11:43 kwao. Onyesha picha ya Maria na Yesu Kristo Mfufuka (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 59), na shuhudia kwamba Yesu Kristo alifanya iwezekane kwa kila mtu kufufuka.

  • Waalike watoto kuchora picha za rafiki zao au wanafamilia, ikijumuisha jamaa zao. Watoto wanaposhiriki picha zao, onyesha kwa kidole kila rafiki au mwanafamilia waliyemchora na elezea kwamba mtu yule atafufuka. Shuhudia kwamba Yesu alifanya iwezekane kwetu sisi kuwa na familia zetu milele.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 8–10

Ninaweza kushiriki injili.

Alma na Amuleki walishiriki injili, hata wakati ilipokuwa si rahisi kufanya hivyo. Ni kwa jinsi gani ujasiri na imani yao vingeweza kuwashawishi watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Kwa maneno yako mwenyewe, fanya ufupisho wa matukio katika Alma 8–10. Chagua kanuni kadhaa kutoka kwenye matukio haya ambazo zingeweza kuwasaidia watoto kushiriki injili, kama vile uvumilivu (ona Alma 8:8–13), kushuhudia juu ya Kristo (ona Alma 9:26–27), na kuwa na mwenza (ona Alma 10:7–11). Waalike watoto kusoma mistari iliyochaguliwa na kusimulia kile walichojifunza kuhusu kushiriki injili. Kwa nini ni muhimu kuwaambia wengine kuhusu injili?

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu wakati waliposhiriki injili na mtu fulani, au shiriki uzoefu wako mwenyewe. Waalike watoto kusikiliza jinsi wanavyoweza kujiandaa kushiriki injili wakati wakiimba wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “We’ll Bring the World His Truth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172). Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka sisi kushiriki injili? Wasaidie watoto kupanga jinsi ya kushiriki injili na rafiki zao, kama vile kuwapa nakala ya Kitabu cha Mormoni au kuwaalika kwenye shughuli ya Kanisa. Wape muda wa kuigiza kile ambacho wangeweza kusema au kufanya katika hali hizi.

Alma 11–12

Mpango wa Mungu ni mpango wa wokovu.

Ni kwa jinsi gani utatumia Alma 11–12 ku “[fanya] ufahamike kwa [watoto] mpango wa ukombozi”? (Alma 12:30).

Shughuli za Yakini

  • Andika ubaoni baadhi ya kanuni zinazohusiana na mpango wa ukombozi zinazopatikana katika Alma 11–12, kama vile Anguko la Adamu na Hawa, Upatanisho wa Yesu Kristo, toba, kifo, ufufuo, na hukumu. Soma mistari michache kutoka Alma 11 au 12 ambayo inafundisha kuhusu kanuni hizo, na wape watoto muda wa kuchora picha inayowakilisha kila kanuni. Ni nini wajibu wa Mwokozi katika mpango huu? Kisha waalike watoto kutumia picha zao kuigiza kumfundisha rafiki kuhusu mpango wa Mungu.

Alma 12:10

Kama sitashupaza moyo wangu, ninaweza kupokea zaidi kutoka kwenye maneno ya Mungu.

Linapokuja suala la kujifunza kweli za kiroho, hali ya mioyo yetu ni muhimu kama vile uwezo wa akili zetu.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Alma 12:10, na kujadili inamaanisha nini “kushupaza” mioyo yetu. Ni kwa nini moyo ulioshupazwa hufanya iwe vigumu zaidi kujifunza kutoka kwa Mungu?

  • Kuelezea kwa mfano kanuni hii, waonyeshe watoto sponji na jiwe na waulize kipi kitafyonza maji vizuri. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwonyesha Bwana kwamba tunataka mioyo yetu iwe laini kama sponji?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutafuta fursa za kushiriki injili au kumsaidia mtu mwingine wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda darasani kwako. Ushuhuda unaweza kuwa rahisi kama “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wenu” au “Ninahisi vizuri ndani ninapojifunza kuhusu Yesu Kristo.” (Ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11.)