Njoo, Unifuate
Juni 29–Julai 5. Alma 23–29: Hawakuwahi “Kuanguka Kamwe”


“Juni 29–Julai 5. Alma 23–29: Hawakuwahi ‘Kuanguka Kamwe,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 29–Julai 5. Alma 23–29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Waanti-Nefi-Lehi wanazika silaha zao

Waanti-Nefi-Lehi Wanazika Silaha Zao za Vita, na Jody Livingston

Juni 29–Julai 5

Alma 23–29

Hawakuwahi “Kuanguka Kamwe”

Kwa sala soma Alma 23–29, ukitafuta mwongozo wa kiungu kuhusu kile watoto wanachohitaji na jinsi gani ya kuwasaidia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Chora uso wa furaha kwenye kipande cha karatasi, na mruhusu kila mtoto kukishikilia. Wanaposhikilia karatasi, waalike kutaja kitu fulani wanachojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambacho kinawaletea furaha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 24:6–24

Ninabarikiwa pale ninapotunza ahadi zangu.

Ulijifunza nini katika kujifunza kwako Alma 24:6–24 ambacho kinaweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kutunza ahadi takatifu?

Shughuli za Yakini

  • Soma baadhi ya mistari au vifungu vya maneno kutoka Alma 24:6–24 ili kuwafundisha watoto kuhusu Waanti-Nefi-Lehi , ahadi waliyoweka, na jinsi walivyotunza ahadi. Ungeweza pia kutumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia au “Mlango wa 26: Watu wa Amoni” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 73–74, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org).

  • Elezea ni kwa jinsi gani Waanti-Nefi-Lehi walivyotunza ahadi yao kwa kuzika silaha zao. Waalike watoto kuchora upanga na kisha kujifanya wanachimba shimo na kuzika upanga wao. Wasaidie watoto kufikiria juu ya ahadi wanazofanya. Kwa nini ni muhimu kutunza ahadi? Eleza kwamba wakati tunapobatizwa, tunafanya ahadi na Mungu na Yeye hufanya ahadi na sisi. Haya yanaitwa maagano. Shuhudia kwamba tunabarikiwa pale tunapotunza ahadi zetu na Mungu.

Alma 2629

Injili hunipa shangwe, na ninaweza kushiriki shangwe hii na wengine.

Amoni, ambaye alisaidia kufundisha injili kwa Waanti-Nefi-Lehi, alipokea shangwe kubwa kutokana na kuhubiri injili. Alma, ambaye pia alifundisha injili kwa watu wengi, alipokea shangwe kama hii. Tunaweza kupata shangwe sawa na hii pale tunaposhiriki shuhuda zetu pamoja na wengine.

Shughuli za Yakini

  • Chagua vifungu vichache vya maneno kutoka Alma 26 au 29 ambavyo huzungumza kuhusu shangwe, na visome kwa watoto (ona, kwa mfano, Alma 26:11, 13 au Alma 29:13–14). Waalike watoto wasimame kila mara wanaposikia maneno “shangwe” au “shangilia.” Wasaidie watoto kuelewa kwamba kushiriki injili kulimfanya Alma na Amoni kuwa na furaha. Shiriki uzoefu ambapo kushiriki injili kulikuletea shangwe.

  • Waalike watoto kuchora picha za mambo yanayowaletea furaha. Mwalike kila mtoto kutoa mchoro wake kwa mwenzake darasani na kuuelezea. Elezea kwamba wakati kitu fulani kinapotuletea shangwe—kama vile injili—shangwe yetu inakua pale tunapoishiriki.

  • Mpe mtoto mmoja nakala ya Kitabu cha Mormoni, na mpe nafasi ajaribu kukishiriki na mwana darasa mwingine. Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Kitabu cha Mormoni. Kwa nini tunashiriki Kitabu cha Mormoni na wengine?

Alma 27:20–30

Naweza kuwasaidia wengine kuishi injili.

Wanefi waliwalinda Waanti-Nefi-Lehi kutokana na adui zao na kuwasaidia kutunza maagano waliyokuwa wameyafanya na Bwana.

Shughuli za Yakini

  • Wasimulie watoto hadithi ya Waanti-Nefi-Lehi wakifanya ahadi ya kutopigana tena (ona Alma 27:20–30). Elezea kwamba kwa sababu ya ahadi ya Waanti-Nefi-Lehi, hawangeweza kujilinda kutokana na adui zao. Soma Alma 27:23, na elezea kwamba rafiki zao kati ya Wanefi walichagua kuwalinda Waanti-Nefi-Lehi ili waweze kutunza ahadi yao. Jinsi gani tunaweza kuwasaidia rafiki zetu kutunza ahadi zao? Simulia kuhusu wakati ambapo rafiki alikusaidia kutunza ahadi yako na Mungu.

  • Igiza na watoto hali ambapo wanaweza, katika njia ya ukarimu, kuwasaidia wengine kuchagua mema. Kwa mfano, ni nini tunaweza kumwambia rafiki anayetaka kudanganya au kuwa mkatili?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma24

Maagano ni ahadi ninazofanya na Mungu na Yeye hufanya na mimi.

Waanti-Nefi-Lehi Walizika silaha zao na kuahidi kutoua tena. Kadhalika, watoto unaowafundisha wanaweza kutunza maagano yao.

Shughuli za Yakini

  • Wape watoto wote mawe madogo, na waalike kuandika neno agano juu ya mawe yao. Elezea kwamba agano ni ahadi kati ya Baba wa Mbinguni na watoto Wake. Ni kwa jinsi gani maagano yetu hutufanya wenye nguvu au “imara” kama jiwe? (Alma 24:19). Someni pamoja Alma 24:16–25 kujifunza agano lipi watu wa Amoni walifanya na jinsi walivyoheshimu agano lao. Waalike watoto kwenda na mawe nyumbani kama ukumbusho wa kutunza maagano.

  • Soma pamoja na watoto Alma 24:16–19, na kujadili kile Waanti-Nefi-Lehi walichofanya kumwonyesha Mungu wametubu. Je, waliweka agano kutofanya nini? Elezea kwamba maagano tunayofanya ni “ushuhuda kwa Mungu” kwamba tunataka kufuata amri za Mungu (mstari wa 18). Ni maagano yapi watoto wamefanya?

  • Waalike watoto kuchora picha za silaha za Waanti-Nefi-Lehi. Kisha waalike kuandika, nyuma ya silaha zao, kitu wanachohisi wanapaswa kubadilisha ili kumfuata Yesu Kristo kikamilifu zaidi. Waache wajifanye kana kwamba wanazika silaha zao na kuweka mpango wa kutenda kwenye kile walichoandika.

Alma 24:7–10; 26:23–34; 27:27–30

Kwa sababu Baba wa Mbinguni ni mwenye huruma, tunaweza kutubu na kubadilika.

Hivi karibuni watoto wamekuwa wakijifunza kuhusu Alma, Amoni, na Waanti-Nefi-Lehi. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia matukio haya kuonyesha kwamba Baba wa Mbinguni ana huruma kwa wale wanaotubu kwa dhati?

Shughuli za Yakini

  • Andika Kabla na Baada ubaoni. Waombe baadhi ya watoto kusoma mistari ifuatayo kutafuta vile Walamani walivyokuwa kabla ya Amoni na kaka zake kuwafundisha: Alma 17:14–15; 26:23–24. Waombe watoto wengine kusoma mistari ifuatayo kutafuta ni kwa jinsi gani Walamani walibadilika: Alma 26:31–34; 27:27–30. Waalike watoto kuorodhesha chini ya vichwa vya habari kile walichopata. Kisha waalike kugundua, katika Alma 24:7–10, ni kwa jinsi gani Walamani hawa waliweza kubadilika kikamilifu. Toa ushuhuda wako wa nguvu ya Mungu kutusamehe na kutusaidia kutubu na kubadilika.

  • Waalike watoto wasome pamoja Alma 26:21–22, ukitafuta baraka zinazokuja kwa wale wanaotubu. Waalike watoto kuelezea baadhi ya baraka hizi kwa maneno yao wenyewe.

Alma 2629

Injili hunipa shangwe, na ninaweza kushiriki shangwe hii na wengine.

Sura hizi zina mifano tele ya shangwe ambayo huja kutokana na kuishi na kushiriki injili. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Alma 26 na 29 kuwatia msukumo watoto kutafuta shangwe hii?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kupata maneno “shangwe” na “shangilia” katika Alma 26 na 29. Someni pamoja baadhi ya mistari wanayopata, na kujadili kile mistari hii inachofundisha kuhusu shangwe. Nini kiliwaletea Amoni na Alma shangwe? Shiriki uzoefu ambapo ulihisi shangwe kutokana na kuishi au kushiriki injili, au waalike watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe.

  • Waalike watoto wawili kuangaliana, na kuona nani anaweza kumfanya mwenzake kutabasamu kwanza. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kusambaza shangwe kwa wengine? Ni kwa jinsi gani kushiriki injili husambaza shangwe? Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kushiriki shangwe ya injili na rafiki na familia zao?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutunza ahadi zao kama Waanti-Nefi-Lehi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jifunze maandiko. Chagua dondoo ya maandiko au kifungu kifupi ambacho unafikiri kingeweza kuwasaidia watoto katika darasa lako, na wasaidie kukikariri. Misaada ya kuona na ishara za mikono zinaweza pia kusaidia.

Chapisha