Njoo, Unifuate
Julai 13–19. Alma 32–35: “Pandeni Neno Hili Ndani ya Mioyo Yenu”


“Julai 13–19. Alma 32–35: ‘Pandeni Neno Hili Ndani ya Mioyo Yenu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Julai 13–19. Alma 32–35,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Mbegu kwenye mkono wa mtoto

Julai 13–19

Alma 32–35

“Pandeni Neno Hili Ndani ya Mioyo Yenu”

Waweke watoto unaowafundisha akilini mwako wakati kwa sala unaposoma Alma 32–35. Unapofanya hivyo, mawazo na misukumo vitakuja kuhusu jinsi ya kuwafundisha. Andika na fanyia kazi misukumo hii.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Weka jina la kila mtoto ndani ya chombo. Muombe mtoto mmoja kuchagua moja ya majina, na kumwalika mtoto huyo kushiriki kitu alichojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni hivi karibuni. Endelea mpaka kila mmoja amepata fursa, lakini usimlazimishe yeyote kushiriki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 32:28–43

Ninaweza kusaidia imani yangu katika Yesu Kristo kukua.

Mbegu, miti, na matunda ni vitu vinavyojulikana ambavyo vinaweza kuwasaidia watoto kuelewa kanuni za dhahania kama imani na ushuhuda. Tafakari jinsi unavyoweza kutumia analojia ya Alma kufundisha watoto.

Shughuli za Yakini

  • Fanyia ufupisho Alma 32:28–43; ungeweza kutumia “Mlango wa 29: Alma Anafundisha kuhusu Imani na Neno la Mungu” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 81, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Onyesha picha za mmea katika hatua tofauti za ukuaji, na waombe watoto wakusaidie kuweka picha katika mpangilio sahihi (ona picha katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Elezea kwamba tunapoishi injili, ushuhuda wetu unakua—unaanza mdogo kama mbegu lakini unakua mkubwa kama mti.

  • Waonyeshe watoto mbegu, na wasomee mistari michache ya kwanza ya Alma 32:28. Waambie watoto kwamba neno la Mungu ni kama mbegu. Uliza jinsi tunavyoweza kusaidia mbegu kukua. Waache watoto wajifanye kupanda mbegu, kuimwagilia, na kuisaidia kukua. Onyesha kwamba hatuwezi kuiona mbegu baada ya kuipanda, lakini tunajua iko pale na inakua; hatuwezi pia kumwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, lakini tunajua Wao ni halisi na Wanatupenda. Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo wanayoweza kufanya kusaidia imani yao katika Yesu Kristo kukua.

  • Chora mti ubaoni, na waache watoto waongeze jani au tunda kila wakati wanapofikiria juu ya jambo wanaloweza kufanya kusaidia imani yao katika Yesu Kristo kukua. Waalike kufanya matendo rahisi kuwakilisha mambo waliyoyafikiria.

Alma 33:2–11; 34:17–27

Baba wa Mbinguni hunisikia ninaposali.

Wazoramu walisali mara moja kwa wiki, wakitumia maneno yaleyale kila mara (ona Alma 31:22–23). Alma na Amuleki walifundisha kwamba tunaweza kusali muda wowote kuhusu mahitaji yetu yoyote ya kiroho au kimwili.

Shughuli za Yakini

  • Soma vifungu vya maneno ulivyochagua kutoka Alma 33:4–11 ambavyo vinaelezea mahali tunapoweza kusali, na wasaidie watoto kufikiria mahali wanapoweza kusali. Kisha waalike wachore picha zao wenyewe wakisali mahali hapo. Shuhudia kwamba wanaweza kusali mahala popote, hata kama wanasali kimyakimya.

  • Chagua vifungu vya maneno kutoka Alma 34:17–27 ambavyo huelezea mambo tunayoweza kuyaombea, na yasome kwa watoto. Wasaidie kufikiria juu ya mambo wanayoweza kusema kwa Baba wa Mbinguni wakati wanaposali, na waalike kuchora picha za mambo haya. Shuhudia kwamba wanaweza kuzungumza na Baba wa Mbinguni kuhusu kitu chochote wanachofikiria au kuhisi. Shiriki uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni alisikia sala zako.

  • Imba wimbo unaowafundisha watoto kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” au We Bow Our Heads” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13, 25). Wasaidie kugundua kile wimbo unachofundisha kuhusu sala.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 32:1–16, 27–28

Nikiwa mnyenyekevu, Bwana anaweza kunifundisha.

Alma na Amuleki walifanikiwa kuwafundisha Wazoramu waliokuwa wanyenyekevu na wenye utayari kusikia neno la Mungu. Fikiria jinsi gani unaweza kuwahimiza watoto kuchagua kuwa wanyenyekevu.

Shughuli za Yakini

  • Waulize watoto kile wanachokumbuka kujifunza wiki iliyopita kuhusu Wazoramu (ona Alma 31:8–24). Wakumbushe kwamba sababu moja Alma alikuwa na hofu kuhusu wao ilikuwa ni kiburi chao (ona Alma 31:24–28). Someni pamoja Alma 32:1–5, na waulize watoto nini kilikuwa kimewapata Wazoramu waliokuwa masikini. Kisha waalike watoto kusoma mstari wa 12–13 kutafuta kwa nini Alma alihisi kwamba kutupwa nje ya masinagogi yao (au makanisa) lilikuwa ni jambo zuri kwa Wazoramu hawa. Ni zipi baadhi ya baraka zinazokuja kwa kuwa mnyenyekevu?

  • Wasaidie watoto kutafuta maana ya nyenyekevu au unyenyekevu katika Mwongozo wa Maandiko au kamusi. Ni dokezo zipi zingine kuhusu maana ya maneno haya wanaweza kupata katika Alma 32:13–16? Waalike kufikiria njia kadhaa za kukamilisha sentensi kama “ninakuwa mnyenyekevu ninapo .”

Alma 32:26–43.

Ushuhuda wangu wa Yesu Kristo unakua ninapoutunza.

Wasaidie watoto unaowafundisha kugundua kile wanachoweza kufanya “kupanda” neno la Mungu katika mioyo yao.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha kitu kigumu, na imara (kama jiwe) kuwakilisha moyo mgumu au wenye kiburi na kitu laini (kama udongo) kuwakilisha moyo laini au mnyenyekevu. Waache watoto waguse vitu vyote viwili. Kisha waonyeshe watoto mbegu kuwakilisha neno la Mungu. Waalike wajaribu kusukuma mbegu ndani ya kitu kigumu na kitu laini. Someni pamoja Alma 32:27–28, na mzungumze kuhusu ingemaanisha nini “kutoa nafasi” (mstari wa 27) kwa neno la Mungu katika mioyo yetu.

  • Mnaposoma Alma 32:26–43 kwa pamoja, simama mara kadhaa na waalike watoto kuchora picha ya mbegu au mmea ulioelezewa—kwa mfano, mbegu na mche (mstari wa 28), mmea unaokua (mstari wa 30), na mmea mkubwa unaotoa matunda (mstari wa 37). Wahimize kuweka majina kwenye picha zao kwa kutumia marejeleo kutoka Alma 32. Ni kwa jinsi gani kutunza mbegu ni kama kutunza shuhuda zetu za Yesu Kristo? Tunatunzaje shuhuda zetu? Waalike watoto kwa utulivu kufikiria kuhusu jinsi shuhuda zao zinavyokua na kile watakachofanya kuzitunza.

Alma 33:2–11; 34:17–27

Baba wa Mbinguni hunisikia ninaposali.

Wazoramu walikuwa na uelewa mbaya kuhusu sala, uelewa ambao bado tunauona leo. Alma na Amuleki walifundisha kweli zenye nguvu ili kukinza uelewa huu mbaya.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kutafuta Alma 33:2–11 ili kupata maneno muhimu au vifungu vya maneno vinavyohusiana na sala ambavyo vimejirudia. Maneno na vifungu hivi vya maneno vinatufundisha nini kuhusu sala?

  • Wasaidie watoto kutengeneza orodha ya mazingira ambapo wanaweza kusali, yakijumuisha yale yaliyotajwa katika Alma 33:4–10 na 34:17–27 pamoja na mazingira katika maisha yao. Waalike watoto kufikiria au kushiriki uzoefu wakati waliposali na kuhisi kwamba Mungu amejibu sala zao.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ikiwezekana, mpe kila mtoto mbegu aende nayo nyumbani na kuipanda ili kuwakumbusha kusaidia shuhuda zao za Yesu Kristo kukua. Wahimeze wawaambie familia zao kile walichojifunza kuhusu kufanyia kazi imani yao katika Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya baraka zilizoahidiwa. Unapowaalika watoto kuishi kanuni ya injili, shiriki ahadi ambazo Mungu ameahidi kwa wale wanaoishi kanuni hiyo (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).