“Julai 20–26. Alma 36–38: ‘Elekeza Jicho kwa Mungu na Uishi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Julai 20–26. Alma 36–38,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Julai 20–26
Alma 36–38
“Elekeza Jicho kwa Mungu na Uishi”
Unapojifunza kwa sala Alma 36–38, misukumo inaweza kukujia kuhusu watoto unaowafundisha. Andika misukumo hii; inaweza kuchochea mawazo kwa ajili ya shughuli za kujifunza.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike watoto wote kushiriki jambo ambalo wazazi wao wamewafundisha. Waulize kama wanajua kile Alma alichowafunza wana wake.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Toba huniletea shangwe.
Kuwafundisha watoto kuhusu shangwe ya toba wakiwa bado wadogo kunaweza kuwapa msukumo wa kutubu wanapokuwa wakubwa.
Shughuli za Yakini
-
Soma Alma 36:20 kwa watoto, na waombe wasikilize jinsi Alma alivyohisi. Waalike wataje baadhi ya mambo yanayowaletea shangwe. onyesha picha ya Mwokozi, na elezea kwamba Alma alihisi shangwe kwa sababu Yesu Kristo alimsamehe dhambi zake.
-
Mpe kila mtoto kipande cha karatasi chenye uso wa furaha upande mmoja na uso wa huzuni upande wa pili. Waombe wasikilize wakati ukisoma Alma 36:6 na kuchagua uso upi wanapaswa kunyanyua. Elezea kwamba Alma alitubu na kuhisi shangwe kwa sababu Yesu Kristo alimsamehe kwa kufanya chaguzi mbaya. Waombe watoto wasikilize wakati ukisoma Alma 36:24 kuhusu chaguzi nzuri alizofanya baadaye na kunyanyua uso sahihi.
-
Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,34–35). Toa ushuhuda wako kwamba Yesu alikuja duniani kutuokoa kutoka dhambi na kutuletea shangwe.
“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”
Ni kwa jinsi unaweza kuwafundisha watoto kutambua kwamba Bwana hutumia vitu vilivyo vidogo na rahisi kufanikisha kazi Yake?
Shughuli za Yakini
-
Soma Alma 37:6–7, na waalike watoto kuinama chini kila mara unaposoma neno “vidogo.” Waonyeshe baadhi ya vitu vidogo ambavyo vinaweza kufanya vitu vikubwa vitokee au kuendesha vitu vikubwa, kama vile betri au ufunguo wa gari. Ni vitu gani vikubwa hutokea au kuendeshwa kwa sababu ya vitu hivi vidogo? Wasaidie watoto kufikiria baadhi ya vitu vidogo na rahisi Mungu anavyotaka tufanye. Ni vitu gani vikubwa vinaweza kutokea kwa sababu ya hizi amri ndogo au rahisi?
-
Onyesha picha au viwili kati ya vitu vidogo ambavyo hujikusanya na kuwa vitu vikubwa, kama vile jani na shamba, au tone la mvua na ziwa. Shuhudia kwamba hata matendo madogo, na rahisi yanaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha yetu na maisha ya wengine. Wahimize watoto kuzungumza kuhusu baadhi ya vitu rahisi, na vyema wanavyofanya kila siku, au shiriki mifano yako mwenyewe. Waalike watoto kuchagua kitu kimoja rahisi, na chema wanachoweza kufanya wiki hii na kuchora picha yao wenyewe wakifanya kitu hicho. Waalike kupeleka michoro yao nyumbani na kuishiriki na familia zao.
Maandiko yanaweza kutusaidia kila siku.
Japo watoto wengi wadogo hawawezi kusoma, unaweza kuwasaidia kupata ushuhuda wa nguvu ya maandiko ili kuongoza maisha yao ya kila siku.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya Liahona (kama vile Kitabu cha sanaa ya Injili, na. 68), au waalike watoto wachore picha wakati wakishiriki kile wanachokumbuka kuhusu picha hiyo (ona 1 Nefi 16:10, 28–29). Nyanyua juu maandiko, na waombe watoto washiriki ni kwa jinsi maandiko ni kama Liahona. Tumia Alma 37:38–47 na ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuongezea kwenye majadiliano haya.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu kusoma maandiko, kama vile “Search, Ponder, and Pray” au “As I Search the Holy Scriptures” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109; Nyimbo za Kanisa, na. 277). Ni baraka zipi za usomaji wa maandiko zimetajwa katika wimbo?
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza “kuzaliwa na Mungu” ninapomfuata Yesu na kutubu dhambi zangu.
“Uongofu … ni badiliko katika asili yetu hasa. Ni badiliko la muhimu hasa kwamba Bwana na manabii Wake wanaliita kuzaliwa upya” (“Uongofu,” Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org).
Shughuli za Yakini
-
Pitia tena pamoja na watoto hadithi ya uongofu wa Alma Mdogo katika Alma 36:6–21. Andika kwenye vipande vya karatasi maneno na vifungu vya maneno kutoka kwenye mistari hii ambavyo vinaelezea jinsi Alma alivyohisi, na uviweke ubaoni. Waombe watoto kupanga vipande vya karatasi katika makundi mawili: mambo Alma aliyohisi kabla ya kukumbuka kile baba yake alichofundisha kuhusu Mwokozi na mambo aliyohisi baada ya kukumbuka. Someni pamoja Alma 36:17–20, na shuhudia kwa watoto kwamba Yesu Kristo hutusamehe wakati tunapotubu.
-
Andika Mmezaliwa na Mungu na marejeleo yafuatayo ya maandiko ubaoni: 1 Yohana 4:7; Mosia 5:7; 27:25–26; Alma 5:14; 22:15. Wasaidie watoto kusoma mistari na kutafuta vifungu vya maneno ambavyo vinaelezea kile inachomaanisha kuzaliwa na Mungu. Ni kwa jinsi gani mtu hutenda baada ya kuzaliwa na Mungu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba tumezaliwa na Mungu?
“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”
Wasaidie watoto unaowafundisha kuona kwamba kusoma maandiko hata kwa muda mfupi kila siku kunaweza kuwaletea baraka kubwa.
Shughuli za Yakini
-
Chora au onyesha ndoo. Itachukua matone ya maji kiasi gani kujaza ndoo? Wasaidie watoto kutambua kwamba matone mengi ya maji yatahitajika kujaza ndoo. Ni kwa jinsi gani hili linahusiana na Alma 37:6–7? Ni kwa jinsi gani kusoma maandiko ni sawa na kuongeza matone madogo ya maji kwenye ndoo?
-
Waalike watoto kutazama katika Alma 37:6–9 kupata baraka zinazokuja kutokana na “kumbukumbu,” au maandiko. Kama darasa, tengenezeni orodha ya kile wanachopata. Ni kwa jinsi gani kusoma maandiko kumebariki maisha yetu? Shiriki ushuhuda wako wa maandiko, na wahimize watoto kufanya hivyo pia.
-
Onyesha picha ya Liahona (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 68), na waombe watoto kurejea kile wanachokumbuka kuhusu Liahona kutoka 1 Nefi 16:10, 28. Wasaidie watoto kusoma Alma 37:38–42. Je! Liahona ilifanya vipi kazi? Ni kwa jinsi gani hii ni sawa na vile maandiko yanavyofanya kazi? Someni pamoja mstari wa 43–47 kusaidia kujibu swali hili. Waalike watoto kumalizia ukurasa wa shughuli kama sehemu ya shughuli hii.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki sababu moja ya kuwa na shukrani kwa ajili ya maandiko na kuwaalika wanafamilia wao kufanya hivyo pia.