“Julai 27–Agosti 2. Alma 39–42: ‘Mpango Mkuu wa Furaha,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Julai 27–Agosti 2. Alma 39–42,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Julai 27–Agosti2
Alma 39–42
“Mpango Mkuu wa Furaha”
Baada ya kujifunza kwa sala Alma 39–42, panga shughuli za kuwasaidia watoto kujifunza. Unaweza kupata mawazo kati ya shughuli zifuatazo ambazo zinaweza kutumika kwa kundi la umri wowote.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Mwalike kila mtoto kusimama na kushiriki jambo kuhusu injili ambalo amejifunza karibuni nyumbani au kanisani.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Naweza kuwa mfano mzuri.
Alma alimsihi Koriantoni kujifunza kutokana na mfano mzuri wa kaka zake na kumuonya Koriantoni kutokuwa mfano mbaya kwa wengine.
Shughuli za Yakini
-
Elezea kwamba Shibloni na Koriantoni walikuwa ndugu na kwamba Shibloni alikuwa mfano mzuri kwa Koriantoni. Waalike watoto kurudia swali hili pamoja nawe: “Si yeye amekupatia mfano mzuri?” (Alma 39:1). Waombe watoto kumzungumzia mtu ambaye ni mfano mzuri kwao.
-
Chezeni mchezo au imbeni wimbo ambapo watoto wanakufuata au kukuiga, kama vile “Do as I’m Doing” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 276). Acha kila mtoto apate zamu kuwa kiongozi au mfano. Waulize watoto jinsi wanavyoweza kuwa mfano mzuri kwa mtu mwingine.
-
Onyesha picha za Yesu akifanya mambo mazuri, na elezea kwamba Yeye ni mfano wetu mkamilifu. Elezea kwamba tunaweza kuwa mifano mizuri, kama Yesu alivyokuwa. Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe wakiwa mifano mizuri.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kunisaidia kusahihisha makosa yangu.
Ijapokuwa watoto wadogo hawahitaji kutubu, kuwasimulia kuhusu Koriantoni kungeweza kuwasaidia kuanza kuelewa toba humaanisha nini.
Shughuli za Yakini
-
Bila kwenda kwenye maelezo ya kina kuhusu chanzo cha dhambi yake, elezea kwamba Koriantoni alifanya uchaguzi mbaya. Tunaweza kusema nini ili kumsaidia? Wasomee watoto kile Alma, baba wa Koriantoni, alichomwambia: “Utubu na kusahau dhambi zako” (Alma 39:9). Waambie kwamba “kutubu” humaanisha kwamba tunamwomba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutusamehe na kutusaidia kusahihisha makosa yetu na kwamba kisha tunajitahidi kuwa zaidi kama Wao.
-
Mpe mtoto kitu kizito akishikilie wakati ukisimulia hadithi kuhusu mtu aliyefanya jambo baya na kuhisi vibaya. Waambie watoto kwamba kitu kile ni sawa na hisia mbaya tunazoweza kuwa nazo tunapofanya kosa. Chukua kitu kizito kutoka kwa mtoto huku ukishuhudia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kuondoa hisia nzito, na mbaya na kutusaidia kusahihisha makosa yetu pale tunapotubu. Imbeni pamoja wimbo kuhusu toba, kama vile “Repentance” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 98).
Mimi nitafufuka.
Wasaidie watoto kutazamia siku wakati wao pamoja na wapendwa wao watafufuka.
Shughuli za Yakini
-
Wakati unaposoma Alma 40:23 kwa sauti, waache watoto watumie ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia kupata taswira ya nini mstari huu unafundisha. Mwalike kila mtoto kutumia ukurasa wa shughuli kumfundisha mtoto mwingine ufufuo ni nini.
-
Onyesha picha ya Mwokozi mfufuka, na wafundishe watoto wimbo kuhusu Ufufuo, kama vile “Did Jesus Really Live Again?” au “He Is Risen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64; Nyimbo za Kanisa, na. 199). Pumzika mara kwa mara kuelezea maana na umuhimu wa maneno na vifungu vya maneno.
-
Waulize watoto kama mtu wanayemfahamu aliyekufa. Shiriki ushuhuda wako kwamba mtu huyo na kila mtu atafufuka kwa sababu ya Yesu Kristo. Kama itahitajika, tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuelezea kile inachomaanisha kufufuka.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Naweza kuwa mfano mzuri.
Ushauri wa Alma kwa Koriantoni unaweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kufuata na kuwa mifano mizuri.
Shughuli za Yakini
-
Eleza kwamba mwana wa Alma Koriantoni alifanya dhambi mbaya wakati alipopaswa kuhubiri injili. Soma nusu ya mwisho ya Alma 39:11 pamoja na watoto, na waombe wasikilize jinsi dhambi ya Koriantoni ilivyowaathiri Wazoramu. Wasaidie watoto kufikiria watu ambao wanaweza kuwa wameshawishika kwa matendo yao. Ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa mifano mizuri kwa watu hawa?
-
Someni pamoja Alma 39:1. Ni kwa jinsi gani Shibloni kaka wa Koriantoni alikuwa mfano mzuri? Waombe watoto kutafuta majibu ya ziada kwa swali hili katika Alma 38:2–4. Waambie kuhusu baadhi ya mifano mizuri katika maisha yako, na waalike watoto kufanya vivyo hivyo. Onyesha video “Lessons I Learned as a Boy” (ChurchofJesusChrist.org), na waulize watoto jinsi gani mvulana mkubwa alikuwa mfano mzuri.
-
Leta tochi au picha ya jua, na linganisha mwanga na nguvu ya mfano mwema. Kama vile mwanga kutoka kwenye tochi au kwenye jua unavyoweza kutusaidia kuona njia tunayohitaji kufuata, mfano mwema hutuonyesha nini cha kufanya ili kumfuata Baba wa Mbinguni. Shiriki uzoefu ambapo mfano mzuri wa mtu mwingine ulikusaidia. Ni nini watoto wanaweza kufanya ili kuwa mfano mzuri kwa wengine? Shuhudia kwamba Yesu Kristo ni mfano wetu mkamilifu.
Naweza kutubu ninapofanya makosa.
Kama vile sisi sote, watoto unaowafundisha wanatenda dhambi na kufanya makosa. Unawezaje kuwapa msukumo wa “kusahau dhambi [zao]” na kutubu? (Alma 39:9).
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kushiriki uzoefu wakati walipoumizwa. Ni nini walifanya kusaidia jeraha lao kupona? Elezea kwamba dhambi hujeruhi roho zetu, lakini Mwokozi anaweza kutuponya tunapotubu.
-
Waombe watoto kutafuta kifungu cha maneno “utubu na kusahau dhambi zako” katika Alma 39:9, na wasaidie kuelewa nini “kutubu” na “kusahau” humaanisha. Shuhudia kwamba toba inawezekana kupitia Yesu Kristo na Upatanisho wake. Someni pamoja Alma 39:10–14 kupata mambo mengine tunayoweza kufanya ambayo yatatusaidia kutubu na kuepuka dhambi.
Baada ya kufa, roho zetu huenda kwenye ulimwengu wa roho kusubiri Ufufuo na Hukumu.
Ni kawaida kujiuliza nini hutokea kwetu baada ya kufa. Maneno ya Alma yanaweza kuwasaidia watoto kupata majibu yenye msukumo.
Shughuli za Yakini
-
Andika kifo, ulimwengu wa roho, ufufuo, na hukumu kwenye vipande tofauti vya karatasi, na viweke ubaoni katika mpangilio usio sahihi. Wasaidie watoto kuelewa maana ya maneno haya. Soma Alma 40:6–7, 11–14, na 21–23 pamoja na watoto, na waombe kuweka maneno ubaoni katika mpangilio wake sahihi.
-
Andika ubaoni orodha ya maswali yanayoweza kujibiwa na Alma 40:6–7, 11–14, na 21–23, na waalike watoto kuoanisha kila swali na mistari inayolijibu. Kwa mfano, “Mwili wangu utakuwaje nitakapofufuka?” linaweza kujibiwa na Alma 40:23. Kama inawezekana, fafanua maneno magumu kwa watoto wakati wakisoma. Wahimize watoto kushiriki kwa nini wanashukuru kwa mpango wa Baba wa Mbinguni.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kumshukuru mwanafamilia ambaye amekuwa mfano mzuri kwao na kufikiria njia moja ya jinsi wanavyoweza kuwa mifano mizuri wiki hii.