Njoo, Unifuate
Agosti 24–30. Helamani 7–12: “Mkumbuke Bwana”


“Agosti 24–30. Helamani 7–12: ‘Mkumbuke Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 24–30. Helamani 7–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Nefi akisali katika mnara wa bustani

Kielelezo cha Nefi katika mnara wa bustani na Jerry Thompson

Agosti 24–30

Helamani 7–12

“Mkumbuke Bwana”

Unaposoma Helamani 7–12, tafakari jinsi hadithi na kanuni katika milango hii zinaweza kuwabariki watoto unaowafundisha. Mawazo yaliyoko katika muhtasari huu yanaweza kuongezea msukumo unaopokea.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waulize watoto kile wanachojua kuhusu nabii Nefi, mwana wa Helamani (ona Helamani 7–12). Kama itahitajika, elezea tofauti kati ya nabii aliyeitwa Nefi na nabii aliyeitwa Nefi mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Helamani 7:20

Bwana anataka mimi nimkumbuke Yeye.

Nefi alishangazwa na jinsi watu wake walivyogeuka kutoka kwa Mungu na Kumsahau. Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifunza jinsi wanavyoweza kumkumbuka Baba wa Mbinguni na Yesu?

Shughuli za Yakini

  • Shiriki na watoto uzoefu ambapo ulisahau kitu cha muhimu. Waulize kama wamewahi kusahau kitu. Wasomee Helamani 7:20, na elezea kwamba Wanefi walichagua kumsahau Mungu. Nabii Nefi aliwataka wamkumbuke Mungu. Leta picha ndani ya begi ambazo zinawakilisha njia ambazo watoto wanaweza kumkumbuka Baba wa Mbinguni na Yesu. Waache watoto wafanye zamu kuchagua picha na kushiriki jinsi tunavyoweza kumkumbuka Mungu kila siku.

  • Wasaidie watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

Helamani 8:13–23

Manabii wanashuhudia juu ya Yesu Kristo.

Nefi alishuhudia kwamba Yesu Kristo angekuja, na aliwaalika watu wake kutubu na Kumfuata. Tumia milango hii kuwafundisha watoto kwamba manabii hushuhudia juu ya Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo na waambie watoto kwamba manabii kama Nefi wanatualika kumfuata Yesu. Soma maneno yafuatayo kuhusu manabii kutoka Helamani 8:22: “wameshuhudia kuja kwa Kristo, na wamengojea, na wamefurahia siku yake ambayo itakuja.” Shiriki pamoja na watoto jambo ambalo nabii wetu aliye hai amelisema kuhusu Mwokozi.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu manabii, kama vile “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110). Chagua kifungu cha maneno cha muhimu kutoka kwenye wimbo, na andika neno moja kutoka kwenye kifungu cha maneno kwenye kila moja ya karatasi zenye alama za nyayo. Tandaza nyayo sakafuni zikielekea kwenye picha ya Mwokozi. Waalike watoto kufuata njia ya nyayo, na wasaidie kusoma maneno.

Helamani 10:11–12

Nitamtii Baba wa Mbinguni.

Mfano wa Nefi wa utiifu unaweza kuwapa msukumo watoto unaowafundisha kumtii Bwana.

Shughuli za Yakini

  • Soma Helamani 10:2, 11–12, na wasaidie watoto kuelewa kwamba Nefi alimtii Mungu. Waalike watoto kuigiza kile Nefi alichofanya. Kwa mfano, waombe watembee kuelekea upande mmoja wa chumba (kama vile wanaenda nyumbani), wasimame, wageuke na kutembea kuelekea upande mwingine wa chumba (kama vile wanarudi kufundisha watu). Wasaidie kuona kwamba Nefi alitaka kumtii Bwana hata kama alitakiwa kufanya jambo gumu.

  • Wasaidie watoto kuelewa kwamba wakati mwingine Baba wa Mbinguni anatutaka kufanya jambo ambalo ni tofauti na kile tunachotaka kufanya, lakini tunaweza kumtii kama Nefi alivyofanya. Shiriki maelezo kama “Wakati mwingine ninataka kukasirika, lakini Baba wa Mbinguni anataka niwe … ,” na waruhusu watoto kumalizia maelezo. Wahimize watoto kukumbuka kusimama na kutafakari kuhusu kile Baba wa Mbinguni anawataka wafanye na kisha kukifanya.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Helamani 7–11

Nitakuwa salama kiroho pale ninapomfuata nabii.

Rais James E. Faust alifundisha: “Usalama wetu upo kwenye kusikiliza kile ambacho [Rais wa Kanisa] husema na kufuata ushauri wake” (“Ufunuo Endelevu,” Ensign, Nov. 1989, 10).

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ubaoni ya mambo ambayo nabii hufanya (ona “Nabii,” Mwongozo kwenye maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie kupekua Helamani 7:1–2, 27–29; 8:22–23; na 10:3–4, 6–7 kuona jinsi Nefi alivyofanya baadhi ya mambo katika orodha yao. Ni lini tumemuona nabii wetu wa leo akifanya mambo haya? Toa ushuhuda wako wa nabii aliye hai. Ili kuonyesha kwa mfano umuhimu wa manabii, onyesha dakika ya kwanza ya video “Watchman on the Tower” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Someni pamoja Helamani 11:3–7 (au rejea “Mlango wa 39: Nefi anapokea Nguvu Kubwa,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 108–10, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto kusikiliza nini kilitokea kwa watu ambao hawakumsikiliza nabii. Ni nini kinaweza kutokea wakati hatumsikilizi nabii? Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapomfuata Yeye? Shiriki jambo ambalo nabii wetu amefundisha, na wahimize watoto kufuata mafundisho yake.

Helamani 7:20–21

Bwana anataka mimi nimkumbuke Yeye.

Watoto unaowafundisha watapata mvuto wa mawazo ambao ungeweza kuwasababisha kumsahau Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwapa msukumo watoto kutoa muda kwenye mambo ya kiroho?

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Helamani 7:20–21, na waulize watoto kile wanachofikiria inamaanisha kumsahau Mungu. Elezea kwamba neno sahau linaweza pia kumaanisha “kuacha” au “kupuuzia.” Onyesha picha ya Mwokozi, na waalike watoto kuchora vitu ambavyo wangeweza kutumia muda mrefu kuvifanya ambavyo vingeweza kuwafanya wamsahau Bwana. Weka michoro yao mbele ya picha ya Yesu. Waombe watoto kufikiria vitu wanavyoweza kufanya kila siku ili kumkumbuka Baba wa Mbinguni na Yesu. Wanaposhiriki mawazo yao, ondoa michoro mmoja baada ya mwingine mpaka picha ya Mwokozi ijionyeshe.

  • Waalike watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

Helamani 10

Ninapotafakari maneno ya Mungu, ninaweza kupokea ufunuo.

Je, watoto unaowafundisha wanajua maana ya kutafakari? Wasaidie kuelewa kwamba Nefi alibarikiwa kwa ufunuo wakati alipotafakari mambo ambayo Bwana alimwonyesha.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kuelewa kutafakari kunamaanisha nini (ona “Tafakari,” Mwongozo kwenye maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waalike kufikiria maneno mengine ambayo yanaelezea maana ya kutafakari. Kisha waombe wasome Helamani 10:1–3 na kubadilisha neno tafakari kwa maneno waliyofikiria. Nini kilitokea wakati Nefi alipotafakari maandiko? (ona Helamani 10:3–7). Shiriki wakati ambapo ulipokea ufunuo baada ya kutafakari andiko au ufunuo wa siku za leo au uzoefu wa kiroho.

  • Wape watoto muda wa kusoma Helamani 10, au someni pamoja, na wahimize kutafuta mstari ambao wangependa kuutafakari kipindi cha wiki inayokuja. Waalike kuandika mstari wanaochagua kwenye karatasi au kadi na kuiweka mahali pa kuwakumbusha kutafakari mstari ule kipindi cha wiki inayokuja. Katika darasa lijalo, wape muda wa kushiriki kile walichojifunza pale walipotafakari mstari.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao kile wanachopanga kufanya ili kumkumbuka Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kila siku. Wangeweza pia kuwaalika familia zao kujiunga nao katika lengo lao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa Mialiko ambayo inaheshimu haki ya kujiamulia. Unapowaalika watoto kutenda juu ya kile ambacho umewafundisha, fikiria jinsi ya kuheshimu haki yao ya kujiamulia pale wanapotumia kile walichojifunza. Kwa mfano, baada ya somo kuhusu Mwokozi, ungeweza kuuliza, “Ni nini utafanya ili kumkumbuka Mwokozi wiki hii?”

Chapisha