Njoo, Unifuate
Agosti 10–16. Alma 53–63: “Kuhifadhiwa na Uwezo Wake wa Ajabu”


“Agosti 10–16. Alma 53–63: ‘Kuhifadhiwa na Uwezo Wake wa Ajabu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 10–16. Alma 53–63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
vijana askari mashujaa elfu mbili

Vijana Askari Mashujaa Elfu Mbili, na Arnold Friberg

Agosti 10–16

Alma 53–63

“Kuhifadhiwa na Uwezo Wake wa Ajabu”

Unaposoma Alma 53–63, fikiria jinsi gani ungeweza kuleta hadithi katika sura hizi kwenye maisha kwa ajili ya watoto na wasaidie kujifunza kanuni za injili ambazo hadithi hufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwaandaa watoto kujifunza kutoka Alma 53–63, waalike kushiriki kile wanachokumbuka kuhusu Wa Anti-Nefi-Lehi (ona Alma 23–24). Ili kusaidia, onyesha picha uliyotumia kusimulia hadithi, au wakumbushe shughuli waliyofanya darasani.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Alma 53:20–21; 56:27, 47–48

Ninaweza kuwa mwaminifu kwa Mungu kama walivyokuwa vijana askari mashujaa.

Vijana wa Helamani (ikimaanisha “wadogo”) askari mashujaa wanaweza kuwa mfano mkubwa kwa watoto katika darasa lako. Wahimize watoto kujaribu kuwa kama wao.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtoto kunyanyua picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapofanya ufupisho wa hadithi ya vijana askari mashujaa wa Helamani. Ungeweza pia kutumia “Mlango wa 34: Helamani na Vijana Askari Mashujaa 2,000” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 93–94, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Waruhusu watoto washiriki kile wanachofahamu na kupenda kuhusu hadithi ya vijana askari mashujaa 2,000.

  • Waalike msichana na mvulana kuwakilisha akina mama na akina baba wa vijana askari mashujaa. Unaposoma Alma 56:27 na 47–48, wape watoto hawa vitu vya kushikilia ambavyo vinawakilisha jinsi akina mama na akina baba walivyowasaidia askari mashujaa, kama vile gunia la chakula kuwakilisha “vyakula” walivyopeleka akina baba na maandiko kuwakilisha mafundisho ya akina mama. Waombe watoto kushiriki vitu wazazi wao wanavyowapatia au kuwafundisha.

  • Soma Alma 53:20–21, na wasaidie watoto kuelewa kile maneno kama hodari, jasiri, nguvu, na kweli humaanisha. Elezea jinsi askari mashujaa walivyoonyesha sifa hizi. Tengeneza beji rahisi kwa ajili ya watoto ambazo zinasomeka, “Ninapo , ninakuwa kama askari mashujaa!” Wasaidie watoto kujaza nafasi zilizo wazi kwa kiwango wanachochagua kutoka Alma 53:20–21.

  • Waalike watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waalike wafikirie jinsi wanavyoweza kuwa kama jeshi la Helamani. Imbeni pamoja “We’ll Bring the World His Truth” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172–73).

Alma 58:32–41.

Ninapokuwa na hofu, ninaweza kumtumaini Mungu.

Wakati yeye na jeshi lake walipopata wakati mgumu, Helamani alimtumaini Bwana. Ni nini watoto unaowafundisha wanaweza kujifunza kutokana na mfano huu?

Shughuli za Yakini

  • Chora uso wenye hofu ubaoni, na zungumza kuhusu jinsi Helamani alivyopata hofu kwa sababu jeshi lake halikuwa na chakula cha kutosha au wanaume wa kutosha kuendelea kupigana (ona Alma 58:32–41). Waombe watoto kushiriki wakati ambapo walipata hofu. Soma Alma 58:37 (au msaidie mtoto kusoma), na wasaidie watoto kubadilisha uso ubaoni kuwa uso wenye tabasamu kuonyesha jinsi Helamani alivyohisi kwa sababu alimtumaini Mungu. Tunaweza kufanya nini tunapohisi hofu? Imbeni pamoja “Smiles” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,267).

  • Andika katika vipande vya karatasi mambo machache ambayo watoto wanaweza kuyahofia. Waruhusu watoto kufanya zamu kuchagua karatasi kwa ajili yako kusoma, na waalike watoto kushiriki jinsi ambavyo Mungu angeweza kuwasaidia kwa kila moja ya hofu hizi. Shiriki uzoefu ambapo Mungu alikusaidia ulipokuwa na hofu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Alma 56:45–48; 57:21, 25–27; 58:39–40

Ninaweza kuwa mwaminifu kwa Mungu kama walivyokuwa vijana askari mashujaa.

Ni kweli zipi kutoka kwenye hadithi ya vijana askari (ikimaanisha “wadogo”) mashujaa zinaweza kuwasaidia watoto katika changamoto wanazopitia?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusiana na vijana askari mashujaa. Ungeweza pia kutumia “Mlango wa 34: Helamani na Vijana Askari Mashujaa 2,000 (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 93–94, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Waache watoto washiriki kile wanachovutiwa nacho kuhusu mashujaa.

  • Someni pamoja Alma 56:45–48; 57: 21, 25–27; 58:39–40. Waalike watoto kutafuta maneno na vifungu vya maneno kutoka kwenye mistari hii ambavyo huwaelezea vijana askari mashujaa. Maneno na vifungu hivi vya maneno vinamaanisha nini? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama vijana askari mashujaa?

  • Soma Alma 56: 46–48 kwa watoto, na waalike wasikilize kile ambacho akina mama wa vijana askari mashujaa waliwafundisha watoto wao kuhusu imani. Ni kwa jinsi gani wazazi leo huwasaidia watoto wao kuwa na imani? Kwa nini ni muhimu kwa watoto kufuata mafundisho ya haki ya wazazi wao na viongozi wa Kanisa kwa “usahihi”? (Alma 57:21).

Picha
Mama akimfundisha mwanaye

Mbegu ya Imani, na Jay Ward

Alma 53:10–17; 56:27

Ninaweza kuyashika maagano yangu.

Vijana askari mashujaa na wazazi wao walifanya agano ambalo walilitimiza kwa uaminifu. Ungeweza kutumia maelezo haya kuwafundisha watoto kuhusu umuhimu wa maagano.

Shughuli za Yakini

  • Wagawe watoto katika makundi matatu: moja kuwakilisha Helamani, lingine kuwakilisha watu wa Amoni, na la tatu kuwakilisha wana wa watu wa Amoni. Someni Alma 53:10–17 pamoja, na ruhusu makundi kushiriki ni kwa jinsi gani watu wanaowawakilisha walifanya na kutunza maagano. Shiriki ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni hutubariki sisi pale tunapotunza maagano.

  • Andika ubaoni vifungu vya maneno kutoka Mosia 18:8–10 au Mafundisho na Maagano 20:37 ambavyo vinaelezea mambo tunayoahidi kufanya wakati tunapobatizwa. Pia andika baadhi ya vifungu vya maneno ambavyo havihusiani na maagano. Waombe watoto wazungushie mambo tunayoahidi kufanya (waruhusu watumie maandiko kama itahitajika). Je, tunabarikiwa vipi tuaposhika maagano yetu? Wahimize watoto kuandika kile walichomuahidi Mungu kufanya na weka orodha yao mahali ambapo wanaweza kuiona mara kwa mara.

  • Mwalike mtoto asome Alma 56:27. Ni kwa jinsi gani akina baba waliwasaidia wana wao bila kuvunja agano lao la kutopigana? Nani anatusaidia sisi katika kutunza maagano yetu?

Alma 61:3–14

Ninaweza kuchagua kutokasirika.

Moroni kwa makosa alimtuhumu Pahorani, lakini badala ya kukasirika, Pahorani alisema, “Nina … furaha kwa ujasiri wa moyo wako” (Alma 61:9).

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufikiria kuhusu wakati ambapo walituhumiwa kwa kufanya jambo ambalo hawakulifanya. Waambie kuhusu jinsi hili lilivyotokea kwa Pahorani (ona Alma 60–61). Ungeweza kutumia “Mlango wa 35: Kapteni Moroni na Pahorani” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 95–97, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Ili kujifunza kuhusu jinsi Pahorani alivyojibu, fanyeni zamu kusoma mistari kutoka Alma 61:3–14. Pahorani alifanya nini pale Moroni alipomtuhumu? Tunajifunza nini kuhusu msamaha kutoka kwenye mfano wa Pahorani? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama yeye?

  • Andika ubaoni Ninapaswa kufanya nini wakati mtu anaponikasirikia? Waalike watoto kufanya zamu kuandika baadhi ya majibu ubaoni. Ni kwa jinsi gani Pahorani angeweza kujibu swali hili? Waombe watoto kuandika majibu haya katika barua kwao wenyewe ambayo wanaweza kuisoma wakati mtu anapowakasirikia.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao njia moja wanayotaka kuwa kama vijana askari mashujaa. Wangeweza pia kuwashukuru wazazi wao kwa kuwafunza kama walivyofanya mama wa vijana askari mashujaa.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Washirikishe watoto katika majadiliano ya injili. Kubadili mpangilio wa darasa kunaweza wakati mwingine kusaidia watoto kushiriki vizuri katika majadiliano ya injili. Kwa mfano, ungeweza mara kadhaa kuwaaalika watoto kukaa kwenye duara sakafuni badala ya kwenye viti vyao.

Chapisha