Njoo, Unifuate
Agosti 10–16. Alma 53–63: “Kuhifadhiwa kwa Uwezo Wake wa Ajabu”


“Agosti 10–16. Alma 53–63: ‘Kuhifadhiwa kwa Uwezo Wake wa Ajabu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 10–16. Alma 53–63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
vijana askari elfu mbili

Vijana Mashujaa Elfu Mbili, na Arnold Friberg

Agosti 10–16

Alma 53–63

“Kuhifadhiwa kwa Uwezo Wake wa Ajabu”

Maelezo katika Alma 53–63 yanaweza kukusaidia kuona matokeo ya kuishi kweli za injili au kuzikataa. Unaposoma Alma 53–63, andika misukumo na tafakari njia unazoweza kuishi kweli unazojifunza.

Andika Misukumo Yako

Wakati likilinganishwa na majeshi ya Walamani, “jeshi dogo” la Helamani (Alma 56:33) la vijana 2,000 Wanefi hawakuwa na uwezo wa kushinda. Licha ya kuwa wachache kwa idadi, wanajeshi wa Helamani “wote … walikuwa wachanga sana,” na “walikuwa hawajawahi kupigana” (Alma 56:46–47). Kwa namna fulani, hali yao yaweza kuonekana inayofahamika kwetu sisi ambao wakati mwingine tunahisi kuzidiwa na kushindwa katika vita yetu ya siku za mwisho dhidi ya Shetani na majeshi ya uovu duniani.

Lakini jeshi la Helamani lilikuwa na heri fulani kuliko Walamani ambayo haikuhusika chochote na idadi au ujuzi wa kijeshi. Walimchagua Helamani, nabii, awe kiongozi wao (Alma 53:19); “walikuwa wamefundishwa na mama zao, kwamba ikiwa hawakuwa na shaka, Mungu angewaokoa” (Alma 56:47); na walikuwa na “imani kubwa kwa yale ambayo walikuwa wamefundishwa.” Kama matokeo, walilindwa na “uwezo wa kimiujiza wa Mungu” (Alma 57:26). Hata ingawa wote walijeruhiwa katika vita, “hakukuwa na nafsi moja miongoni mwao ambaye aliangamia” (Alma 57:25). Kwa hivyo wakati maisha yanatuumiza na majeraha ya kiroho kwa kila mmoja yetu, tunaweza kuwa majasiri—ujumbe wa jeshi la Helamani ni kwamba “kuna Mungu mwenye haki, na yeyote asiyemshuku, [ata] ahifadhiwa na uwezo wake wa ajabu” (Alma 57:26).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Alma 53:10–22; 56:43–48, 55–56; 57:20–27; 58:39–40

Ninapokuwa na imani katika Mungu, Atanibariki kwa uwezo Wake wa ajabu.

Hadithi za miujiza kama vile ushindi wa vijana mashujaa wa Helamani zaweza kuwa ngumu kuhusisha kwa sababu zinaonekana si yamkini. Bali sababu moja hadithi kama hizi ziko katika maandiko ni kutuonyesha kwamba wakati tuna imani, Mungu anaweza kufanya miujiza maishani mwetu. Unaposoma kuhusu vijana mashujaa katika mistari ifuatayo, tafuta vidokezo kuhusu jinsi ambavyo walikuwa na imani katika Mungu, ni nini kilifanya imani yao iwe na nguvu sana, na nini kilifanya miujiza iwezekane: Alma 53:10–22; 56:43–48, 55–56; 57:20–27; na 58:39–40. Jedwali lifuatalo linapendekeza njia moja unayoweza kuweka kumbukumbu ya kile unachopata.

Tabia za mashujaa wa Helamani:

Kile walichofunzwa :

Kile walichofanya:

Baraka walizopokea:

Baada ya kusoma mistari hii, ni nini unahisi umetiwa msukumo kufanya ili kutumia imani yako?

Helamani alitaja wajibu wa akina mama katika kuimarisha imani ya vijana mashujaa (ona Alma 56:47–48; 57:20–27). Ni wajibu gani wanafamilia na wengine wamekuwa nao katika kujenga imani yako? Unaweza kufanya nini ili kuimarisha imani ya familia yako na marafiki?

Picha
vijana mahujaa na mama yao

Hawakuwa Na Shaka, na Joseph Brickey

Alma 58:1–12, 31–3761

Ninaweza kuchagua kufikiria mema juu ya wengine bila ya kuchukizwa.

Wote wawili Helamani na Pahorani walikuwa na sababu za kuchukizwa. Helamani hakuwa akipokea msaada wa kutosha kwa ajili ya majeshi yake, na Pahorani alilaumiwa kimakosa na Moroni kwa kuzuia msaada huo (ona Alma 58:4–9, 31–3260). Nini kinakufurahisha kuhusu majibu yao Alma 58:1–12, 31–37 na Alma 61? Unawezaje kufuata mifano yao katika hali sawa na hizo?

Mzee David A. Bednar alifundisha : “Katika njia fulani na wakati fulani, mtu fulani katika Kanisa hili atafanya au atasema kitu ambacho kinaweza kufikiriwa kuwa cha kuchukiza. Tukio kama hili bila shaka litatokea kwa kila mmoja wetu—na hakika litatokea zaidi ya mara moja. … Wewe na mimi hatuwezi kudhibiti nia au tabia za watu wengine. Hata hivyo, tunaamua jinsi ambavyo tutatenda. Tafadhali kumbuka ya kwamba wewe na mimi ni mawakala tulio na uhuru wa kuchagua , na tunaweza kuchagua kutokwazika” (“Wala Hawana La Kuwakwaza,” Ensign au Liahona, Nov. 2006, 91).

Ona pia Mithali 16:32; Moroni 7:45; David A. Bednar, “Mnyenyekevu na Mpole Katika Moyo,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 30–33.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Alma 53:10–17

Waanti-Nefi-Lehi walifanya agano kutomwaga damu. Ni maagano gani tumefanya na Mungu? Tunasoma nini katika Alma 53:10–17 ambacho kinatutia msukumo kuwa waaminifu zaidi kwa maagano yetu?

Alma 53:20–21

Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa zaidi kama wavulana wa Helamani? Yaweza kusaidia kujadili kile baadhi ya virai katika mistari hii vinamaanisha; kwa mfano, inamaanisha nini kuwa “shujaa … kwa nguvu na vitendo? Ina maana gani kutembea “wima mbele ya [Mungu]”?

Alma 58:9–11, 33, 37

Katika nyakati za mahitaji makuu, tunamgeukia Baba wa Mbinguni, jinsi walivyofanya askari? Ni kwa jinsi gani alijibu sala zao? Ni kwa jinsi gani amejibu sala zetu?

Alma 61:2, 9, 19

Tunajifunza nini kutoka kwa Pahorani kuhusu jinsi ya kujibu wakati tumelaumiwa kimakosa?

Alma 62:39–41

Hapa kuna somo la vitendo ambalo laweza kuisaidia familia yako kuelewa kwamba tunaweza tukachagua vyote viwili “kuwa wagumu” au “kulainishwa” na majaribu yetu: Weka kiazi na yai bichi ndani ya sufuria ya maji yanayochemka. Kiazi na yai vinatuwakilisha sisi, na maji yanawakilisha majaribu tunayopitia. Kiazi na yai vinapochemka, unaweza kuzungumza kuhusu baadhi ya majaribu ambayo familia yenu inapitia. Nini baadhi ya njia mbalimbali za kujibu majaribu kama haya? Kulingana na Alma 62:41, ni jinsi gani majibu yetu kwa majaribu yanatuathiri? Baada ya kiazi na yai kuiva kikamilifu, pasua kiazi na pasua yai kuonyesha kwamba “jaribu” lile moja lililainisha kiazi na kufanya yai kuwa gumu. Ni nini familia zetu zinaweza kufanya ili kuhakikisha kwamba majaribu yetu yanatunyenyekeza na kutuleta karibu na Mungu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wape watoto nafasi ya kuonyesha ubunifu wao. “Wakati unapowaalika watoto [wako] kubuni kitu kinachohusika na kanuni ya injili, unawasaidia kuelewa vyema kanuni hiyo, na unawapa kitu halisi cha kukumbuka juu ya kile walichojifunza. … Waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,25).

Picha
vijana mashujaa elfu mbili.

Ni Kweli, Bwana, Wote Wapo na Wamehesabiwa, na Clark Kelley Price

Chapisha