Njoo, Unifuate
Agosti 17–23. Helamani 1–6: “Mwamba wa Mkombozi Wetu”


“Agosti 17–23. Helamani 1–6: ‘Mwamba wa Mkombozi Wetu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 17–23. Helamani 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
mawimbi yakipiga juu ya miamba

Agosti 17–23

Helamani 1–6

“Mwamba wa Mkombozi Wetu”

Kanuni katika muhtasari huu zinaweza kusaidia kuongoza kujifunza kwako Helamani 1–6, lakini zisikuwekee mipaka. Roho Mtakatifu atakuongoza kufikia kweli unazohitaji kujifunza.

Andika Misukumo Yako

Kitabu cha Helamani kinarekodi yote mawili ushindi na misiba miongoni mwa Wanefi na Walamani. Kinaanza na “taabu kubwa miongoni mwa watu wa Wanefi” (Helamani 1:1), na taabu hizo zinaendele kutokea kote katika kumbukumbu hii. Hapa tunasoma kuhusu njama za kisiasa, magenge ya wanyan’ganyi, kukataliwa kwa manabii, na majivuno na kutoamini kote nchini. Lakini pia tunapata mifano kama Nefi na Lehi na “sehemu kubwa ya walio wanyenyekevu” ambao sio tu waliendelea kuishi bali walistawi kiroho (Helamani 3:34). Ni kwa jinsi gani walifanya hilo? Ni kwa jinsi gani waliendelea kuwa imara wakati ustaarabu wao ulianza kupungua na kusambaratika. Kwa njia sawa na vile yeyote yule miongoni mwetu hubaki imara katika “dhoruba kali” ibilisi anatuma “[ku]piga juu [yetu]”—kwa kujenga maisha yetu “juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, … msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka” (Helamani 5:12).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Helamani 1–6

Majivuno yananitenganisha kutoka kwa Roho na nguvu za Bwana.

Unaposoma Helamani 1–6—na kote katika Kitabu cha Mormoni—unaweza kugundua mtindo katika tabia ya Wanefi: Wakati Wanefi ni wenye haki, Mungu anawabariki na wanafanikiwa. Baada ya muda, wanakuwa wenye majivuno na waovu, na kufanya chaguzi ambazo zinaongoza kwenye maangamizo na mateso. Kisha wananyenyekezwa na kutiwa msukumo ili watubu, na Mungu anawabariki tena. Mtindo huu unajirudia mara nyingi hadi watu wengine wanauita “mzunguko wa majivuno.”

Picha
mzunguko wa majivuno

“Mzunguko wa majivuno.”

Tafuta mifano ya mzunguko huu unaposoma. Unaweza hata kutaka kuwekea alama mifano wakati unapoipata. Haya ni baadhi ya maswali ya kukusaidia kuelewa mtindo huu na kuona jinsi unavyoweza kutumika kwako:

Ona pia Dieter F. Uchtdorf, “Majivuno na Ukuhani,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 55–58.

Helamani 3:24–35

Naweza kutakaswa ninapompa Mungu moyo wangu.

Katika Helamani 3, Mormoni alielezea wakati ambapo Kanisa lilikuwa na mafanikio na baraka hata viongozi wakastaajabu (ona mistari ya 24–32). Hatimaye baadhi ya watu wakawa na majivuno, wakati wengine walikua “wenye nguvu zaidi na zaidi katika unyenyekevu wao, … hata kwenye kusafishwa na utakaso wa mioyo yao” (Helamani 3:35). Angalia katika mistari ya 34–35 kile ambacho watu waliokuwa wanyenyekevu zaidi walifanya ili kutakaswa. Je, vitu hivi vinakusaidiaje kuwa mwenye kutakaswa zaidi? Inaweza kuwa yenye kusaidia kujua kwamba Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) unafafanua utakaso kama “mchakato wa kuwa huru kutokana na dhambi, halisi, msafi, na mtakatifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.” Unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kufuata mfano wa wafuasi hawa? Unafanya nini kutoa moyo wako kwa Mungu?

Helamani 5:14–52

Imani yangu imeimarishwa na “ukubwa wa ushahidi ambao [nimeu]pata.”

Mzee Jeffrey R. Holland wakati mmoja aliwaambia wale wanaopambana na imani yao : “Unaweza kuwa na imani zaidi kuliko unavyofikiri unayo kwa sababu ya kile ambacho Kitabu cha Mormoni kinaita ‘ushahidi mwingi’ [Helamani 5:50]. … Tunda la kuishi injili ni dhahiri katika maisha ya Watakatifu wa Siku za Mwisho kila mahali” (”“Bwana, Naamini,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 94). Unaposoma mistari hii, fikiria kuhusu ushahidi ambao Bwana amekupatia. Kwa mfano, pengine haujasikia sauti ya Bwana kihalisia, lakini umewahi kuhisi “mnong’ono” kutoka kwa Roho Mtakatifu ambao “ulipenya hata kwenye roho”? (Helamani 5:30; Ona Pia MM 88:66). Pengine umekuwa katika giza, umemlilia Mungu kwa ajili ya imani kubwa, na “[uka]jazwa na shangwe ile ambayo haiwezi kuzungumzwa” (Helamani 5:40–47). Ni uzoefu gani mwingine ambao umeimarisha imani yako katika Kristo na injili Yake?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Helamani 3:27–30

Wakati nabii Mormoni alikuwa akifupisha kumbukumbu takatifu, mara chache alitumia kirai “hivyo tunaona” kusisitiza kweli muhimu. Alitaka tuone nini katika Helamani 3:27–30? Wakati wa kujifunza kwenu wiki hii, waweza kupumzika mara kwa mara kuwauliza wanafamilia jinsi ambavyo wangeweza kamilisha kirai “na hivyo tunaona” kwa mujibu wa kile walichosoma. Ni kweli zipi wanazo taka kusisitiza?

Helamani 5:6–7

Babu wa Rais George Albert Smith aliyekuwa amefariki George A. Smith alimtokea katika ndoto na kuuliza, “Ningependa kujua kile ambacho umefanya na jina langu.” Rais Smith alijibu, “Kamwe sijawahi kufanya jambo lolote na jina lako ambalo ni la kuleta aibu kwako” (katika Mafundisho ya Marais wa Kanisa: George Albert Smith [2011], xxvi). Baada ya kusoma Helamani 5:6–7, pengine unaweza kuzungumza na wanafamilia wako kuhusu kukumbuka na kuheshimu majina tuliyopewa, ikiwa ni pamoja na jina la Mwokozi.

Helamani 5:12

Kusaidia familia yako kupata taswira ya maana ya “msingi imara” pengine mngeweza kujenga kiunzi kidogo pamoja na kukiweka kwenye aina ya misingi tofauti. Kisha unaweza kutengeneza “dhoruba kali” kwa kukinyunyizia maji ukitumia feni au kifaa cha kukausha nywele ili kusababisha upepo. Kilitokea nini kwa kiunzi wakati kilipokuwa kwenye misingi tofauti? Ni kwa kwa jinsi gani Yesu Kristo ni sawa na “msingi imara” katika maisha yetu?

Helamani 5:29–33

Ni uzoefu gani tumekuwa nao katika kutambua sauti ya Mungu katika maisha yetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Kuwa mvumilivu kwako mwenyewe. Msingi wa amani unajengwa kipande kimoja kwa wakati mmoja. Ukikuta kwamba mafundisho fulani ni magumu kuelewa sasa, kuwa mvumilivu. Amini kwamba uelewa utakuja unapojenga imani yako juu ya Yesu Kristo kwa kutumia imani na kujifunza kwa bidii.

Picha
Nefi na Lehi gerezani

© Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya wasomaji Wadogo, Nefi na Lehi Wamezungukwa na Nguzo za Moto, na Briana Shawcroft; ni marufuku kutoa nakala

Chapisha