Njoo, Unifuate
Juni 22–28. Alma 17–22 : “Nitawafanya Muwe Chombo”


“Juni 22–28. Alma 17–22: ‘Nitawafanya Muwe Chombo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 22–28. Alma 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Amoni Akizungumza na Mfalme Lamoni

Amoni na Mfalme Lamoni, na Scott M. Snow

Juni 22–28

Alma 17–22

“Nitawafanya Muwe Chombo”

Unaposoma Alma 17–22, andika misukumo inayokujia na utende kulingana nayo. Kufanya hivyo kutamuonyesha Bwana utayari wako wa kupokea ufunuo zaidi.

Andika Misukumo Yako

Fikiria kuhusu sababu zote ambazo watu wanaweza kutoa kuwa ndizo zinazowazuia kushiriki injili: “Sijui vya kutosha” au “Sina uhakika kwamba watakuwa na moyo wa kutaka kujua” au pengine “Itakuaje ikiwa nitawakwaza?” Pengine umejikuta wewe mwenyewe ukifikiria vitu kama hivi wakati mwingine. Wanefi walikuwa na sababu ya ziada ya kutoshiriki injili na Walamani: walikuwa “watu wakaidi na wagumu na wakali; watu ambao walifurahia kuwaua Wanefi” (Alma 17:14; ona pia Alma 26:23–25). Lakini wana wa Mosia walikuwa hata na sababu kubwa zaidi kuhisi kuwa lazima washiriki injili na Walamani: “Walitamani kwamba wokovu utangaziwe kila kiumbe, kwani hawangevumilia kwamba nafsi ya mwanadamu yoyote iangamie” (Mosia 28:3). Upendo huu ambao uliwatia msukumo Amoni na ndugu zake unaweza pia kukutia msukumo kushiriki injili na familia yako, marafiki, na watu unaowafahamu—hata wale ambao wanaoonekana kwamba huenda wasiikubali.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Alma 17:1–4

Ninapoimarisha imani yangu, ninaweza kushiriki injili kikamilifu.

Je, umewahi kukutana tena na marafiki wa zamani na kisha ukahisi jinsi Alma alivyohisi—kujawa na shangwe kwamba walikuwa imara katika imani? (ona Alma 17:1–2). Unajifunza nini kutoka kwa wana wa Mosia kuhusu jinsi ya kuweka imani yako katika injili na kujitolea kwako kwa uimara kwenye imani hiyo? Unapotafakari nguvu za kiroho za wana wa Mosia, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini?

Je, matayarisho ya kiroho ya wana wa Mosia yaliathiri vipi kazi yao miongoni mwa Walamani? Pengine ungeweza kutumia nafasi hii kutathmini juhudi zako za kufundisha injili “kwa uwezo na mamlaka ya Mungu” (Alma 17:3).

Alma 17:6–12

Ninaweza kuwa chombo katika mikono ya Mungu kuleta wokovu kwa watoto Wake.

Rais Thomas S. Monson alisema, “Daima nataka Bwana ajue kwamba kama anahitaji kutoa mwito, Tom Monson atatimiza mwito huo kwa niaba Yake” (“Katika Mwito wa Bwana: Maisha ya Thomas S. Monson,” video, ChurchofJesusChrist.org). Unaposoma Alma 17:6–12, tafuta kile ambacho wana wa Mosia walifanya ili waweze kuwa vyombo katika mikono ya Mungu. Unawezaje kuwa chombo katika mikono ya Mungu kuwabariki wengine? Unajifunza nini kutokana na mfano wao ambacho kinakupatia ujasiri wa kufanya kile ambacho Bwana anahitaji ufanye?

Ona pia Dallin H. Oaks, “Kushiriki Injili ya Urejesho,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 57–60.

Alma 17–18

Naweza kuwasaidia wengine kujiandaa kupokea injili.

Lamoni alikuwa kiongozi wa “watu wakaidi na wagumu na wakali” (Alma 17:14), lakini alishinda miaka mingi ya desturi na akaikubali injili ya Yesu Kristo. Unaposoma kuhusu miingiliano baina ya Amoni na Lamoni, tambua kile alichofanya Amoni ambacho chaweza kuwa kilichangia wepesi wa Lamoni kukubali ujumbe wake. Kama mawazo yanakujia kuhusu kile unachoweza kufanya kushiriki injili na wengine, andika misukumo hii.

Yaweza pia kuwa yenye kusaidia kuwekea alama au kuandika kweli ambazo Amoni alimfundisha Lamoni (ona Alma 18:24–39), na kweli ambazo Haruni alimfundisha baba yake Lamoni (ona Alma 22:1–16). Mistari hii inapendekeza nini kwako kuhusu kweli ambazo unaweza kushiriki na wengine ili kuwasaidia kutafuta ushuhuda wa injili?

Picha
Amoni akiokoa kondoo wa mfalme

Minerva K. Teichert (1888–1976), Amoni Anaokoa makundi ya Mifugo ya Mfalme, 1935–1945, mafuta juu ya ubao, inchi 35 x 48. Jumba la Makumbusho ya Sanaa la Chuo Kikuu cha Brigham Young

Alma 18–22

Ushuhuda wangu unaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana.

Ingawaje historia za kuongoka tunazozisoma katika maandiko mara nyingi huusisha matukio ya ajabu, kwenye kiini chake ni kawaida kupata watu ambao walikuwa na ujasiri wa kuzungumza na kushiriki ushahidi wao na wengine. Njia moja ya kujifunza matukio katika Alma 18–22 ni kutafuta athari kubwa za mtu mmoja kushiriki ushuhuda wake. Pengine ungeweza kuandika kile ambacho umegundua katika mchoro kama huu:

Amoni alishiriki injili na , ambaye alishiriki injili na , na matokeo yalikuwa ni .

Alma 19:36

Bwana ananinyoshea mkono wakati ninapotubu.

Katika hitimisho la historia ya kuongoka kwa Lamoni, Mormoni alifundisha jambo muhimu kuhusu tabia ya Bwana. Ni nini Alma 19:36 inapendekeza kuhusu tabia ya Bwana? Ni wakati gani umehisi Bwana akikunyooshea mkono Wake? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale uwapendao kuhisi rehema Yake?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Alma 17–19

Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya historia katika sura hizi kuwa za kiuhalisia kwa ajili ya familia yako? Mngeweza kuigiza hadithi ya Amoni akilinda kondoo au hadithi ya Abishi akikusanya umati kushuhudia uwezo wa Mungu. Pengine wanafamilia wangeweza kuchora picha za sehemu tofauti za hadithi na kutumia picha hizo kusimulia hadithi hiyo. Ni nini familia yako itafanya ili kufuata mfano wa Amoni na Abishi?

Alma 18:24–39

Pengine wanafamilia wako wangeweza kusoma Alma 18:24–39 pamoja na kutambua kweli ambazo Amoni alimfunza Lamoni. Kwa nini tunadhani Amoni alimfundisha Lamoni kweli hizi kwanza? Kwa nini ni muhimu kwetu sisi kuwa na ushuhuda kuhusu kweli hizi?

Alma 20:8–15

Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Lamoni alivyomjibu Baba yake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuiga mfano wa Lamoni katika kutetea haki? (Kwa ajili ya baadhi ya mifano, tazama video “Dare to Stand Alone” katika ChurchofJesusChrist.org.)

Alma 22:15–18

Fanya mapitio ya Alma 20:23 kuona kile ambacho Baba yake Lamoni alikuwa tayari kuacha ili kuokoa maisha yake. Kisha fanya mapitio ya Alma 22:15 kuona kile alichokuwa tayari kuacha ili aweze kupokea shangwe ya injili. Je, alikuwa radhi kuacha nini ili kumjua Mungu? (ona mstari wa 18). Pengine kila mmoja wa wanafamilia angeweza kuandika mpango wa kuacha kitu fulani ili aweze kumjua Mungu kikamilifu zaidi.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Tambua na tumia kanuni. Ingawa maelezo ya hadithi za maandiko yanaweza kuonekana kana kwamba hayakufai, kanuni katika historia hizi mara nyingi zinakufaa. Unaposoma kuhusu Amoni na Haruni, ni kanuni zipi kuhusu kushiriki injili unazopata?

Picha
Mke wa Mfalme Lamoni akipoteza fahamu

Mke wa Mfalme Lamoni aliinuka kutoka chini, akimsifu Yesu. Ee, Yesu Uliyebarikiwa, na Walter Rane

Chapisha