“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4: ‘Walikuwa Wameimarishwa na Hawangeondolewa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Mei 25–31
Mosia 29–Alma 4
“Walikuwa Wameimarishwa na Hawangeondolewa”
Kusoma maandiko kunaalika ufunuo. Kuwa makini na jumbe ambazo Bwana anataka kukupa.
Andika Misukumo Yako
Wengine wanaweza kuonelea ya kwamba pendekezo la Mfalme Mosia la kubadilisha wafalme na nafasi yao kuchukuliwa na waamuzi waliochaguliwa kama marekebisho ya kisiasa ya busara. Lakini kwa Wanefi, hasa wale ambao waliishi chini ya utawala wa Mfalme Mwovu Nuhu, badiliko hili pia lilikuwa na umuhimu wa kiroho. Walikuwa wameshuhudia jinsi mfalme mwovu alivyokuwa amesababisha “uovu” na “mashaka makuu” miongoni mwa watu wake (Mosia 29:17), na “wakataka” kuwa huru kutokana na athari kama hiyo. Badiliko hili lingewaruhusu wao wenyewe kuwajibika kwa ajili ya haki yao wenyewe na “kuchukua wajibu wa dhambi [zao]” (Mosia 29:38; ona pia M&M 101:78).
Bila shaka, mwisho wa uongozi wa wafalme haukumaanisha mwisho wa shida katika jamii ya Wanefi. Watu wajanja kama Nehori na Amlisi waliendeleza dhana za uongo, wasioamini waliwatesa Watakatifu, na waumini wengi wa Kanisa walijawa na Kiburi na kuasi. Lakini “wafuasi wanyenyekevu wa Mungu” walisalia “imara na thabiti” licha ya yale ambayo yalifanyika karibu nao (Alma 1:25). Na kwa sababu ya mabadiliko yaliyofanywa kuwa sheria na Mosia, wangeweza “kupiga kura” kushawishi jamii yao kwa wema (Alma 2:6).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Ninaweza kuwa mshawishi kwa ajili ya wema katika jamii yangu.
Miaka mitano tu katika uongozi wa waamuzi, mgogoro uliibuka ambao ungeingiza majaribuni tangazo la Mosia kwamba sauti ya watu kwa kawaida ingalichagua kile kilicho haki (ona Mosia 29:26). Swala hili lilihusu uhuru wa kuabudu: bwana aliyejulikana kama Amlisi alitafuta “kuwanyang’anya [watu] haki zao na heshima za Kanisa” (Alma 2:4). Je, umegundua haki za kidini zikitishiwa katika taifa lako au jamii? Je, unajifunza nini kutokana na jinsi ambavyo Wanefi walijibu tishio hili? (ona Alma 2:1–7).
Kuna uwezekano kwamba kuna changamoto nyingi zinazoikabili jamii yako. Ni jinsi gani wewe, kama Wanefi, unaweza kuhakikisha kwamba sauti yako imeshirikishwa katika “sauti ya watu”? Pengine unaishi mahali ambapo sauti ya watu ina ushawishi mdogo katika serikali; ikiwa ni hivyo, je kuna njia nyingine ambazo unaweza ukawa mwenye ushawishi chanya katika jamii yako?
Ninaweza kutambua na kukataa mafundisho yasiyo ya kweli.
Ingawaje Nehori alikiri ya kwamba yale aliyofundisha hayakuwa ya kweli, mafundisho yake yaliendelea kuwaathiri Wanefi kwa kipindi cha miaka mingi (ona Alma 1:15–16; 2:1–2; 14:14–18; 15:15; 21:4; 24:28). Je, ni kwa nini watu wanaweza kuwa walivutiwa na mafundisho ya Nehori? Unaposoma Alma 1:2–4, ona ikiwa unaweza kutambua uwongo katika mafundisho ya Nehori; pengine utagundua ya kwamba unafundishwa pamoja na ukweli usio kamili.
Gideoni alimhimili Nehori “kwa maneno ya Mungu” (Alma 1:7, 9). Je, unaweza kufikiria kuhusu maandiko ambayo yanakanusha uwongo wa Nehori? Hii ni baadhi ya mifano, lakini kuna nyingine mingi zaidi: Mathayo 7:21–23; 2 Nefi 26:29–31; Mosia 18:24–26; na Helamani 12:25–26. Je, ni jinsi gani maandiko haya yanaweza kukusaidia kukanusha uwongo unaofundishwa leo?
Njia mbadala ya kufanya mafunzo yako ya Alma 1 ni kumlinganisha Nehori na wafuasi wake (mistari 3–9, 16–20) na “watu wa Mungu” (mistari 25–30; ona pia 2 Nefi 26:29–31). Je, unawezaje kuwa zaidi kama watu wa Mungu? Je, umegundua “ukuhani wa uongo” wowote katika huduma yako?
Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo hawaweki mioyo yao katika utajiri.
Sura za 1 na 4 za Alma zote zinaelezea kuhusu nyakati ambapo Kanisa lilifanikiwa, lakini waumini wa Kanisa walijibu mafanikio hayo kwa njia tofauti katika kila tukio. Umegundua tofauti zipi? Kulingana na kile utakachogundua, ni jinsi gani unaweza kuelezea mtazamo ambao ‘wafuasi wanyenyekevu wa Mungu” (Alma 4:15) wanao kwa utajiri na mafanikio? Je, ni kipi unahisi kushawishika kubadili kuhusu mtazamo wako?
“Neno la Mungu” na “ushuhuda halisi” unaweza kubadili mioyo.
Ni kipi kilimfanya Alma “kuhuzunika sana” (Alma 4:15) katika Alma 4? Wengine wanaweza wakasema ya kwamba ofisi ya muamuzi mkuu ingeweza kumuweka Alma katika nafasi nzuri zaidi ya kutatua shida ambazo aliziona miongoni mwa watu wake. Lakini Alma alihisi kwamba kulikuwa na njia nzuri zaidi. Ni kitu gani kinakuvutia kuhusu njia yake ya kuwasaidia watu wake? Kujifunza kwako kunaweza kutia msukumo mawazo kuhusu jinsi unavyoweza kuwashawishi kwa haki wale walio karibu nawe; kama ni hivyo, tenda kulingana na mawazo hayo.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.
Alma 1:19–25
Familia yako inaweza kufaidika kutokana na kutambua njia tofauti ambazo wafuasi wa Kanisa walijibu mateso katika mistari hii. Pengine waweza kufanya mazoezi ya njia za kujibu inavyofaa wakati watu wengine wanaposhambulia imani yetu. Video katika ChurchofJesusChrist.org/religious-freedom/examples zaweza kusaidia.
Alma 3:4
Ni ujumbe gani Waamlisi walitakata kutoa wakati walipokuwa “wamejiweka alama”? (ona Alma 3:4, 13). Ni ujumbe gani twaweza kutuma—kwa makusudi au bila makusudi—kwa muonekano kwetu? Huu unaweza kuwa wakati mzuri wa kufanya mapitio ya “Mavazi na Muonekano” katika For the Strength of Youth (2011), 6–8.
Alma 4:2–3
Ni vitu gani au matukio gani “yalitukumbushwa [sisi] jukumu [letu]” kwa Mungu? (Alma 4:3). Pengine inaweza kuwa yenye kufaa kushiriki mistari hii baada ya kuiamsha familia yako asubuhi. Kisha waweza kujadili jinsi changamoto za kimwili za kuamka asubuhi zinatusaidia kuelewa changamoto za kuamka kiroho.
Alma 4:10–11
Je, tunawezaje kuepuka kuwa “kikwazo kikuu kwa wale ambao [siyo] washiriki wa kanisa”? (Alma 4:10). Yaweza kuwa muhimu kuzungumza kuhusu jinsi tunavyoweza kuhakikisha vitendo vya wengine, hasa waumini wenzetu wa Kanisa, havitakuwa vikwazo dhidi ya maendeleo yetu ya kiroho.
Alma 4:19
Ili kuisaidia familia yako kuelewa nguvu ya ushuhuda, unaweza kuwaomba wafikirie kuhusu wakati ambapo kusikiliza ushuhuda wa mtu fulani kuliwaathiri kwa kina. Ni kwa nini Alma alichagua kutumia ushuhuda na neno la Mungu kuigusa mioyo ya watu? (Ona pia Alma 31:5). Ni kwa nini hii ni njia inayofaa zaidi kuliko njia zingine watu wanazoweza kutumia kuwashawishi wengine kubadilika? Je, kuna watu ambao tunaweza kuimarisha imani yao kupitia kushiriki nao ushuhuda wetu?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.