Njoo, Unifuate
Aprili 13–19 Mosia 1–3: “Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Watu Wote”


“April 13–19. Mosia 1–3: ‘Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Wanadamu Wote,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“April 13–19. Mosia 1–3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Mfalme Benyamini akiwafundisha watu wake

Minerva K. Teichert (1888-1976), Hotuba ya kuaga ya Mfalme Benjamini, 1935, oil on masonite, 36 x 48 inchi. Chuo Kikuu cha Sanaa cha Brigham Young

Aprili 13–19

Mosia 1–3

“Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Watu Wote”

Unaposoma Mosia 1–3, sali kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kweli za muhimu Mfalme Benyamini alizofundisha. Andika umaizi unaokujia kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya Mfalme Benyamini akifundisha, inayopatikana kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu picha hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mosia 2–3

Ninapowatumikia wengine, Ninamtumikia pia Mungu.

Je, ni nini utafanya kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kuwatumikia wengine ni njia pia ya kumtumikia Mungu?

Shughuli za Yakini

  • Acha watoto wafanye zamu kuvaa taji la mfalme (ukurasa wa shughuli ya wiki hii una mfano) na kusimama juu ya kiti au stuli kujifanya kuwa Mfalme Benyamini. Wanaweza kufanya hivi wakati ukishiriki baadhi ya mambo ambayo Mfalme Benyamini alifundisha watu wake, yanayopatikana katika Mosia 2–3. Ona pia “Mlango wa 12: Mfalme Benyamini” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 32–35, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org).

  • Waalike watoto kurudia sentensi ifuatayo maneno machache kwa wakati pale wanapopiga makofi kwa kila silabi pamoja nawe: “Mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu” (Mosia 2:17). Rudia hili mpaka watoto wamejifunza baadhi au maneno yote. Shuhudia kwamba tunapowasaidia wengine, tunamsaidia pia Baba wa Mbinguni na Yesu na kuwafanya Wao wawe na furaha. Waombe watoto kushiriki jinsi wanavyoweza kuwasaidia wengine.

  • Wasaidie watoto kufuatisha mikono yao juu ya karatasi na kuchora kitu wanachoweza kufanya kuzitumikia familia zao. Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu huduma, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198).

Picha
Watoto wakikunja kipande cha kitambaa

Mfalme Benyamini alifundisha kwamba tunaweza kumtumikia Mungu kwa kuwatumikia wengine.

Mosia 2:19–25

Baraka zangu zote hutoka kwa Baba wa Mbinguni.

Pale watoto wanapomtambua Mungu kama chanzo cha baraka zao, watakuwa wanyenyekevu na wenye shukrani.

Shughuli za Yakini

  • Elezea kwamba Mfalme Benyamini alifundisha kwamba baraka zetu zote hutoka kwa Baba wa Mbinguni. Waalike watoto kusikiliza baraka Baba wa Mbinguni alizotupatia unaposoma Mosia 2:21. Je, Ni baraka zipi zingine Baba wa Mbinguni ametupatia? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba tuna shukuru kwa vitu hivi? (Ona Mosia 2:22).

  • Chezeni mchezo ambapo watoto wanapitisha kitu kwa mzunguko wanapoimba wimbo kuhusu shukurani au kusikiliza wimbo huo (ona “Shukurani” kwenye kielezo cha Kitabu cha Nyimbo za Watoto). Acheni kuimba au simamisha muziki kila baada ya muda fulani, na mwalike yeyote aliyeshikilia kitu kile kushiriki baraka anayoshukuru kwayo.

Mosia 3:1–20

Ninaamini katika Yesu Kristo.

Malaika alimwambia Mfalme Benyamini kweli za muhimu kuhusu maisha na huduma ya Yesu Kristo. Tafuta katika mistari hii kweli kuhusu Yesu ambazo unahisi ni muhimu kwa watoto kujifunza.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha za baadhi ya matukio yaliyotajwa katika Mosia 3:5–10 (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 30, 41, 42, 5759). Waulize watoto ni nini kinatendeka katika picha, na wasaidie kama inavyohitajika. Taratibu soma Mosia 3:5–10, na waalike watoto kuinua mikono yao unaposoma kuhusu jambo katika moja ya picha. Waalike watoto kushiriki mambo mengine ambayo wanajua Yesu alifanya wakati alipokuwa duniani.

  • Chora jua upande wa juu wa ubao kuwakilisha mbingu. Chora njia kadhaa zinazoelekea sehemu tofauti kote ubaoni lakini njia moja tu ambayo huelekea mbinguni. Waombe watoto kutafuta njia hiyo na kuweka picha ya Yesu hapo. Soma Mosia 3:17, na shuhudia kwamba kumfuata Yesu Kristo ni njia pekee ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mosia 2:11–18

Ninapowatumikia wengine, Ninamtumikia pia Mungu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutokana na mfano wa Mfalme Benyamini wa huduma?

Shughuli za Yakini

  • Waonyeshe watoto picha ya Mfalme Benyamini akiwafundisha watu wake (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 74). Wasaidie watoto kutafuta Mosia 2:11–18 ili kupata kile Mfalme Benyamini alichofanya kutumikia. Ni kwa nini aliwatumikia watu wake? Je, ni kwa nini tunapaswa kutumikiana?

  • Andika ubaoni vifungu vya maneno kutoka Mosia 2:16–17 vikiwa havina baadhi ya maneno. Waalike watoto kutafuta kwenye maandiko maneno yanayokosekana. Waombe kueleza kile mistari hii inachomaanisha kwao. Waalike kushiriki uzoefu ambapo wengine wamewatumikia au wao wamewatumikia wengine. Ni kwa jinsi gani uzoefu huu unawafanya wajihisi?

  • Wape watoto vipande vya karatasi kuandika jinsi wanavyoweza kuwatumikia wanafamilia wao, na mpe kila mtoto mfuko aweke karatasi ndani yake. Wahimize watoto kuchukua kipande cha karatasi kutoka kwenye mfuko kila siku na kufanya tendo lile la huduma kwa mtu mwingine.

Mosia 2:15–25

Sipaswi kujisifu kuhusu huduma yangu na matendo mema.

Fikiria kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba huduma yetu inapaswa kuchochewa na upendo wetu kwa wengine na kwa Mungu.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kushiriki jinsi ambavyo wangeweza kutoa maana ya neno jisifu, au wasaidie kutafuta maana kwenye kamusi. Wasaidie kutafuta Mosia 2:15–24, wakitafuta sababu kwa nini Mfalme Benyamini hakujisifu kuhusu huduma yake kwa wengine. Kwa nini tunapaswa kuwatumikia wengine? Baada ya watoto kushiriki mawazo yao, wasaidie kuelewa kwamba tunapaswa kutafuta kuwatumikia wengine kwa sababu tunawapenda wao na Mungu, si kwamba ili tuonekane wema kwa wengine.

  • Waombe watoto kushiriki hali ambazo mtu angeweza kujisifu au kujivuna kuhusu jambo fulani. Kwa nini ni vibaya kujisifu katika hali hizo? Waalike kutumia ushauri kutoka kwenye hotuba ya Mfalme Benyamini katika Mosia 2:15–24 kuwasaidia kwenye majibu yao.

Mosia 3:19

Yesu Kristo hunisafisha kutokana na dhambi na kunisaidia kuwa mtakatifu.

Ili kuwa zaidi kama Baba yetu wa Mbinguni, tunahitaji zaidi ya kusafishwa kutoka dhambi zetu—mioyo yetu lazima ibadilishwe. Kama Mfalme Benyamini alivyofundisha, tunahitaji kushinda tamaa zetu za kufanya dhambi na kuwa watakatifu kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

Shughuli za Yakini

  • Chora watu wawili ubaoni—mmoja kuwakilisha “mwanadamu wa asili” na mwingine kuwakilisha “mtakatifu.” (Unaweza kuhitaji kutoa maana ya maneno haya.) Someni pamoja Mosia 3:19, na waalike watoto kutafuta mabadiliko ambayo mwanadamu wa asili anahitaji kufanya ili kuwa mtakatifu. Ni maneno yapi mengine na vifungu vya maneno watoto wangeweza kuhitaji msaada kuelewa?

  • Je, watoto unaowafundisha wamewahi kuwasaidia wazazi wao kuandaa chakula kwa kutumia maelezo ya upishi? Kama ndivyo, ungeweza kuwaalika kutumia Mosia 3:19 kutengeneza “maelezo” ya jinsi tunavyoweza kuwa kama Yesu Kristo. Kwa nini Upatanisho wa Yesu Kristo ni “kiambato”muhimu zaidi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kushiriki na familia zao au marafiki jinsi watakavyofuata mfano wa Mfalme Benyamini na kuwatumikia wengine.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wananufaika kutokana na marudio. Usiogope kurudia shughuli mara nyingi, hususani na watoto wadogo. Marudio yatawasaidia watoto kukumbuka kile wanachojifunza.

Chapisha