Njoo, Unifuate
Aprili 20–26. Mosia 4–6: “Mabadiliko Makuu”


“Aprili 20–26. Mosia 4–6: ‘Mabadiliko Makuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Aprili 20–26. Mosia 4–6,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Mfalme Benyamini akiwafundisha watu wake

Mnamtumikia tu Mungu Wenu, na Walter Rane

Aprili 20–26

Mosia 4–6

“Mabadiliko Makuu”

Unaposoma na kutafakari Mosia 4–6, kuwa mwangalifu kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu. Je, unashawishika kufanya nini kizuri? (ona Mosia 5:2).

Andika Misukumo Yako

Je, umewahi kumsikiliza mtu akizungumza na kuhisi umeshawishika kubadilisha maisha yako? Pengine uliamua, kwa sababu ya kile ulichokisikia, kuishi tofauti kidogo—au hata tofauti kabisa. Hotuba ya Mfalme Benyamini ilikuwa hotuba ya aina hiyo, na kweli alizofundisha zilikuwa na athari ya aina hiyo juu ya wale watu ambao walizisikiliza. Mfalme Benyamini alishiriki na watu wake kile ambacho malaika alikuwa amemfundisha—kwamba baraka za ajabu zinapatikana kupitia “damu ya upatanisho wa Kristo”(Mosia 4:2). Ujumbe wake ulibadilisha mtazamo wao wote kuwahusu wao wenyewe (ona Mosia 4:2), ulibadili tamaa zao (ona Mosia 5:2), na kuwatia msukumo kuagana na Mungu kwamba daima wangetenda mapenzi yake (ona Mosia 5:5). Hivi ndivyo maneno ya Mfalme Benyamini yalivyowaathiri watu wake. Yatakuathiri vipi wewe?

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mosia 4

Kupitia Yesu Kristo, ninaweza kupokea na kuhifadhi msamaha wa dhambi zangu.

Kumvua mtu wa kawaida siyo rahisi. Inahitaji juhudi kubwa ya kuwa “mtakatifu kupitia upatanisho wa Kristo aliye Bwana” (Mosia 3:19). Mara nyingine, hata unapohisi kuwa umesamehewa dhambi zako, unaweza ukapambana kuhifadhi hiyo hisia na kusalia katika njia ya haki. Mfalme Benyamini alifundisha watu wake jinsi ya kupokea na kuhifadhi msamaha wa dhambi na kuishi daima kama mtakatifu. Unaposoma sura ya 4 ya Mosia, unaweza kujiuliza maswali kama haya:

Mistari 1–12:Ni baraka zipi msamaha wa dhambi uliwaletea watu wa Mfalme Benyamini? Ni nini Mfalme Benyamini alifundisha ili kuwasaidia kuhifadhi msamaha wa dhambi zao? Alifundisha nini kuhusu jinsi tunavyopokea wokovu? Tilia maanani kile Mfalme Benyamini alisema tunapaswa “kila wakati [tu]kishikilie ukumbusho” (mstari 11). Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kuvikumbuka vitu hivi?

Mistari 12–16:Kulingana na mistari hii, nini kinafanyika maishani mwetu kama tutafanya vitu ambavyo vimeelezewa katika mstari wa 11? Umeshuhudia mabadiliko haya katika maisha yako? Yanahusiana kwa njia gani na mabadiliko yaliyoelezewa katika Mosia 3:19?

Mistari 16–30:Ni jinsi gani kushiriki na maskini kunatusaidia kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu? Namna gani waweza kutumia mstari wa 27 kwenye juhudi zako kuwa kama Kristo?

Ona pia David A. Bednar, “Daima Kuhifadhi Msamaha wa Dhambi Zenu,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 59–62; Dale G. Renlund, “Kuhifadhi Mabadiliko Makuu ya Moyo,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 97–99.

Mosia 5:1–7

Roho wa Bwana anaweza kusababisha mabadiliko makuu moyoni mwangu.

Ni kawaida kwa watu kusema ya kwamba, “Siwezi nikabadilika. Hivyo ndivyo nilivyo.” Kinyume na hayo, uzoefu wa watu wa Mfalme Benyamini unatuonyesha jinsi Roho wa Bwana anavyoweza kweli kubadili mioyo yetu. Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Tunaweza kubadili tabia zetu. Tamaa zetu zinaweza kubadilika. … Mabadiliko ya kweli—mabadiliko ya kudumu—yanaweza kuja tu kupitia uponyaji, usafishaji, na uwezo wa nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo. … Injili ya Yesu Kristo ni injili ya mabadiliko!” (“Maamuzi ya Milele,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 108).

Unaposoma kuhusu mabadiliko ya uzoefu wa watu wa Mfalme Benyamini, fikiria kuhusu jinsi “mabadiliko makuu” yanayoelekeza kwenye uongofu wa kweli yamefanyika—au yanaweza kufanyika—katika maisha yako. Je, ni matukio machache “makuu” yaliyosababisha kubadilika kwa moyo wako, au uongofu wako ulifanyika kwa kipindi cha muda mrefu?

Ona Pia Ezekieli 36:26–27; Alma 5:14; David A. Bednar, “Kumgeukia Bwana,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 106–9.

Picha
Kristo akimponya mwanamke mgonjwa

Mwokozi anaweza kubadili mioyo yetu na maisha yetu. Mikono ya Uponyaji, na Adam Abram

Mosia 5:5–15

Ninajichukulia juu yangu jina la Kristo ninapofanya maagano.

Sababu moja ambayo Mfalme Benyamini alitaka kuwahutubia watu wake ni kuwa alitaka “kuwapatia watu hawa jina.” Baadhi walikuwa Wanefi na wengine walikuwa wa ukoo wa Muleki, lakini haya siyo majina ambayo alitazamia. Aliwaalika watu kujichukulia juu yao “jina la Kristo” kama sehemu ya agano lao la utiifu kwa Mungu (Mosia 1:11; 5:10). Unajifunza nini kutoka Mosia 5:7–9 kuhusu maana ya kujichukulia juu yako jina la Kristo?

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha, “Chanzo [cha nguvu za kimaadili na kiroho] ni Mungu. Kushiriki kwetu kwenye nguvu hizo ni kupitia maagano baina yetu Naye” (“Nguvu za Maagano,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 20). Unaposoma Mosia 5:5–15, tengeneza orodha ya baraka ambazo zitakuja maishani mwako unapotunza maagano uliyofanya na Mungu. Je, ni jinsi gani kutunza maagano yako kutakusaidia kuhifadhi “mabadiliko makuu” yaliyofanyika ndani yako kupitia Yesu Kristo na Upatanisho Wake?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Mosia 4:9–12

Ni jinsi gani familia yako inaweza kikamilifu “kumwamini Mungu” (Mosia 4:9) na “kila wakati kushikilia ukumbusho, wa ukuu wa Mungu”? (Mosia 4:11). Pengine wanafamilia wanaweza wakasoma Mosia 4:9–12 na kutambua vifungu ambavyo vinasaidia kujenga imani yao kwa Mungu. Kisha wanaweza kuandika vifungu hivi na kuviweka kote nyumbani kama ukumbusho. Je, ni jinsi gani kuvikumbuka vitu hivi kutatusaidia “kufurahi daima” na “kuhifadhi msamaha wa dhambi [zetu]”? (Mosia 4:12).

Mosia 4:14–15

Tunajifunza nini kuhusu kupigana na kutetanisha kutoka kwenye mistari hii?

Mosia 4:16–26

Ni katika hali gani sisi wote ni waombaji? Kulingana na mistari hii, ni jinsi gani tunapaswa kuwatendea watoto wote wa Mungu? (Mosia 4:26). Ni nani anahitaji usaidizi wetu?

Mosia 4:27

Je, familia yako inakimbia zaidi kuliko nguvu zake? Pengine unaweza ukawaalika wanafamilia kufanya tathmini ya shughuli zao kuhakikisha ya kwamba wanafanya bidii lakini wanakuwa wenye busara pia.

Mosia 5:5–15

Je, kujichukulia jina la Kristo juu yetu kunapendekeza nini kuhusu uhusiano wetu na Yeye? Inaweza kuwa na manufaa kuzungumza kuhusu ni kwa nini watu mara nyingine huandika majina yao kwenye mali zao binafsi. Jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba “tunamilikiwa” na Mwokozi?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuza mazingira ya upendo. Jinsi wanafamilia wanavyotendeana kunaweza kushawishi kwa kina roho ya nyumbani kwako. Wasaidie wanafamilia wote kufanya sehemu yao ili kustawisha nyumba yenye upendo, heshima ili kwamba kila mmoja ajisikie yu salama kushiriki uzoefu, maswali, na shuhuda zao. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 15.)

Picha
Kristo akiwapa ndege chakula katika uga

Daima Katika Utunzaji Wake, na Greg K. Olsen

Chapisha