“Machi 23–29. Enoshi–Maneno ya Mormoni: Anafanya Kazi ndani Yangu ili Nifanye Kulingana na Mapenzi Yake”. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)
“Machi 23–29. Enoshi–Maneno ya Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Machi 23–29.
Enoshi–Maneno ya Mormoni
Anafanya Kazi ndani Yangu ili Nifanye Kulingana na Mapenzi Yake
Jitayarishe kufundisha kwa kusoma Enoshi–Maneno ya Mormoni na kutengeneza mpango wa kufundisha (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 19). Mapendekezo na mafundisho katika muhtasari huu yanaweza pia kusaidia kukupa mawazo.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kuwapa washiriki wa darasa nafasi kushiriki kile wanachojifunza nyumbani, unaweza kuwagawa katika makundi na kupangia kila kikundi kusoma mojawapo ya sura kutoka Enoshi–Maneno ya Mormoni. Waulize kupendekeza mistari kutoka sura ile wanayohisi darasa wanapaswa kujadili. Orodhesha mistari hii ubaoni, na chagua michache kuijadili.
Fundisha Mafundisho
Tunaweza kupokea msamaha wa dhambi zetu tunapofanya imani katika Yesu Kristo.
-
Haya hapa kuna baadhi ya maswali unayoweza kutaka washiriki wa darasa kutafakari na kujadili mnapojifunza Enoshi 1:1–17: Tunajifunza nini kutoka kwa uzoefu wa Enoshi kuhusu kupokea msamaha wa dhambi zetu? Enoshi alioneshaje imani yake katika Yesu Kristo? Jinsi gani uzoefu huu ulimuathiri Enoshi na jinsi gani alijiona mwenyewe na wengine?
Sala zetu za dhati zitajibiwa.
-
Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwa undani sala zao, unaweza kuwagawa katika vikundi vidogo na kiombe kila kikundi kujifunza mojawapo ya vifungu kutoka Enoshi 1: mistari 2–8, 9–11, au 12–17. Kisha uliza kila kikundi kifundishe darasa zima kitu fulani walichojifunza kuhusu sala kutoka mistari yao waliyopangiwa. Kwa mfano, unaweza kuwaalika kushiriki maneno na vishazi ambavyo vinaelezea jinsi Enoshi alivyosali.
-
Kwa nyongeza kujifunza kuhusu jinsi Enoshi alivyosali, tunaweza pia kujifunza mengi kutoka kile Enoshi alichokiomba. Pengine washiriki wa darasa wanaweza kutambua nani au nini alikiombea katika Enoshi 1:14–17. Kulingana na mistari hii, kwa nini Enoshi alitamani kusali kwa ajili ya wengine? Ni kweli gani zingine kuhusu sala tunazojifunza kutoka kwa Enoshi?
Kama tutatii amri, tutabarikiwa.
-
Yaromu na waandishi wa Omni waliandika kuhusu taifa la Wanefi lakini jumbe zao zinahusu pia watu binafsi. Tunajifunza nini kutoka vitabu vya Yaromu na Omni kuhusu jinsi uadilifu unaelekeza kwenye baraka. (Kwa mfano, ona Yoramu 1:7–12 na Omni 1:5–7, 12–18). Inaweza kuwa msaada kwa washiriki wa darasa kufafanua ustawi kwa kutumia kamusi na maandiko (kwa mfano, ona Alma 37:13; 48:15). Jinsi gani ufafanuzi wa ulimwengu unafanana na ufafanuzi wa Bwana? Jinsi gani msaada wa Bwana unasaidia watu wake kubarikiwa?
-
Wakati manabii wa Kinefi walipofanya kazi kwa bidii kufundisha amri kwa watu, manabii wetu wa siku za mwisho pia wanatufundisha kuhusu amri. Baada ya kusoma Yoramu 1:9–12, washiriki wa darasa wanaweza kujadili mafundisho ya hivi karibuni ya viongozi wa Kanisa ambayo yanawavutia kutii amri. Inaweza kuwa ya msaada kwa washiriki wa darasa kurejea jumbe za hivi karibuni za mkutano mkuu katika magazeti ya Kanisa au kwenye Gospel Library app. Wanaweza kurejelea viwango vilivyojadiliwa katika Kwa Nguvu ya Vijana. Kama inahitajika, unaweza kurejea kwenye orodha ya jumbe katika “Nyenzo za Ziada.” Utii wa amri unatusaidia vipi “kubarikiwa” katika maisha yetu?
Bwana aliwaleta watu wengi kwenye nchi ya ahadi.
-
Kitabu cha Mormoni kina historia changamani, na kufuatia makundi tofauti ya watu kinaelezea inaweza kuwa vigumu. Njia moja ya kujifunza kuhusu kila moja ya watu katika Kitabu cha Mormoni inaweza kuwa kutengeneza chati ubaoni na kulitaka darasa kuijaza na taarifa kuhusu kila kundi la watu (kama vile Wanefi, na Walamani, na watu wa Zarahemla). Kwa mfano, chati inaweza kuwa na vichwa vya habari vifuatavyo: Jina la kundi, Lini na jinsi gani walivyofika, na Nini kiliwatokea. Jadilini pamoja kwa nini inasaidia kuelewa vitu mnavyojifunza kuhusu kila kundi. Maingizo haya katika Mwongozo wa maandiko (ChurchofJesusChrist.org) yanaweza kusaidia: “Koriantumuri,” “Wayaredi,” “Walamani,” “Wamuleki,” “Wanefi,” na “Zarahemla.”
Mungu atafanya kazi kupitia sisi kama tunafuata mwongozo Wake.
-
Kama sehemu ya majadiliano ya Maneno ya Mormoni, unaweza kumwalika mshiriki wa darasa kuja amejiandaa kushiriki kwa nini Mormoni alishawishika kuweka ndani mabamba madogo (1 Nefi–Omni) katika Kitabu cha Mormoni. Mshiriki huyu wa darasa anaweza kujiandaa kwa kusoma Maneno ya Moroni na nyenzo zingine, kama vile Mafundisho na Maagano 10:8–19,39–45; muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia; na sura 5 ya Watakatifu, juzuu 1. Watie moyo washiriki wa darasa kuweka ndani kila kitu kinachohusika kuhusu kupotea kwa kurasa 116 za mswada wa Kitabu cha Mormoni na kwa nini mabamba madogo yalihitajika kuchukua nafasi ya kurasa zilizopotea. Ni kweli gani washiriki wa darasa wanajifunza kutokana na hili kuhusu jinsi Bwana anavyofanya kazi kupitia binadamu? Washiriki wa darasa wanaona nini katika Maneno ya Mormoni 1:1–8 kinachowatia moyo kufuata mwelekeo kutoka kwa Mungu hata wanapokuwa hawana uelewa kamili wa sababu?
-
Mormoni alibariki mamilioni ya watu kwa sababu alifuata ushawishi wa Roho kuhusu mabamba madogo (ona Maneno ya Mormoni 1:7). Fikiria njia unazoweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa kwamba wanaweza pia kuwabariki wengine wanapotafuta kuwa vyombo katika mikono ya Mungu na kufuata vishawishi vya Roho Mtakatifu. Jinsi gani Mungu alifanya kazi kupitia Mormoni? Nini washiriki wa darasa wameona Bwana akifanya kupitia kwao au wengine waliposikiliza ushauri wa Roho na kutafuta mapenzi ya Mungu” Hadithi kuhusu Rais Thomas S. Monson katika “Nyenzo za Ziada” inatoa mfano ambao unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiri mifano kutoka kwenye maisha yao wenyewe.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Kwa sababu vyote mkutano mkuu na Pasaka vinakuja katika wiki chache zijazo, watie moyo washiriki wa darasa kusikiliza jumbe ambazo kwazo washiriki wa Urais wa kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanashiriki ushahidi wao mahsusi wa Yesu Kristo.
Nyenzo za Ziada
Video za Kitabu cha Mormoni kuhusu Enoshi.
Tafuta video ambazo zinaonesha maelezo kutoka kitabu cha Enoshi katika Kitabu cha Mormoni lundo la video kwenye ChurchofJesusChrist.org au Gospel Library app.
Jumbe za Mkutano mkuu kuhusu kutii amri.
-
Thomas S. Monson, “Tii Amri,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 83–85.
-
Dieter F. Uchtdorf, “Kuishi Injili kwa Furaha,” Ensign au Liahona, Nov. 2014,120–23
-
Dallin H. Oaks, ““Hakuna Miungu Ingine,” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 72–75.
“Shika mkono wa kila mtoto.”
Wakati Rais Thomas S. Monson akihudumia kama mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alizungumza kwenye mkusanyiko wa watoto wa darasa la msingi katika kijiji cha Samoa. Baada ya hapo, alishawishika binafsi kumwamkia kila mmoja wa watoto 247 ambaye alihudhuria. Hata hivyo, alielewa asingekuwa na muda; alijaribu kuweka wazo la kuwaamkia watoto nje ya mawazo yake lakini hakuweza.
Mwishowe alimgeukia mwalimu wa watoto na kusema, “ningependa sana kushika mkono wa kila mvulana na kila msichana. Je, hiyo itawezekana”
Mwalimu alitabasamu na kuzungumza na watoto kwa Kisamoa. Waliashiria kwa kichwa kwa shauku kwa kujibu. Mwalimu kisha alimwambia Mzee Monson kwamba wakati alipojua kwamba mmoja wapo wa Mitume Kumi na Wawili alikuwa azuru Samoa, alikuwa amewaahidi watoto kwamba kama wangesali kiukweli na kuwa na imani, Mzee Monson angetembelea kijiji chao na atashawishiwa na Roho Mtakatifu kushika mkono wa kila mtoto (ona Thomas S. Monson, “Friend to Friend: Talofa Lava,” Friend, Mei 1072,12–13).