“Machi 16–22. Yakobo 5–7 : ‘Bwana Hufanya Kazi Pamoja na Sisi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Machi 16–22. Yakobo 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Machi 16–22.
Yakobo 5–7
Bwana Hufanya Kazi Pamoja na Sisi
Anza maandalizi yako kwa ajili ya kufundisha kwa kusoma Yakobo 5–7 binafsi na pamoja na familia yako. Ulijifunza nini ambacho kinaweza kuwa cha manufaa sana kwa wale unaowafundisha? Muhtasari huu unaweza kukupa mawazo ya ziada.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Washiriki wa darasa walipata nini katika Yakobo 5–7 ambacho kiliwavutia “kufanya kazi katika shamba la mizabibu” ambako wanaishi? (Yakobo 5:15).
Fundisha Mafundisho
Bwana huwataka watumishi Wake kufanya kazi pamoja Naye katika shamba Lake la mizabibu.
-
Kwa sababu fumbo la mti wa mizeituni ni refu na kidogo changamani, unaweza kutaka kufanya kazi pamoja kama darasa kutengeneza muhtasari wa maelezo ya jumla ya fumbo. Kwa mfano, unaweza kuchora misingi mikuu ya fumbo ubaoni au kutengeneza utaratibu wa matukio (kwa mfano, ona mchoro mwishoni mwa muhtasari huu). Washiriki wa darasa wanaweza kuongeza marejeo ya maandiko kwenye mchoro na kujadili nini baadhi za ishara zinamaanisha, kama vile miti ya mizeituni inayofugwa na ya pori, Bwana wa shamba la mizabibu, watumishi, na tunda zuri na baya. Wakati wa majadiliano, rejea mistari 61–75, ambayo inaelezea kazi ya Bwana katika siku yetu. Tunahudumia vipi katika shamba la mizabibu la Bwana? Jinsi gani mistari hii inahusiana na kazi tunayofanya?
-
Maneno ya “Bwana wa shamba la mizabibu yanaweza kutoa faraja kwa wazazi wa watoto watukutu. Kwa mfano, nini Yakobo 5:41, 46–47 inapendekeza kuhusu jinsi Baba yetu wa Mbinguni anahisi kuhusu watoto Wake wanaopotea? Je, ni kwa jinsi gani yeye anajaribu kuwaokoa? (Ona mistari 61–75).
-
Yakobo 5:61–75 inafundisha kwamba Bwana anafanya kazi sambamba na watumishi Wake katika shamba la mizabibu. Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari hii katika vikundi vidogo na kujadili uzoefu ambao umewaonesha kwamba Bwana anafanya kazi pamoja na watumishi Wake kusogeza mbele kazi Yake. Ni umaizi gani wa ziada washiriki wa darasa wanaweza kuongeza kutoka ujumbe wa Rais Henry B. Erying “Bwana Analiongoza Kanisa Lake”? (Ensign au Liahona, Nov. 2017, 81–84).
Bwana anawakumbuka watu Wake kwa upendo na huruma.
-
Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inatutaka tuchambue Yakobo 6:3–5 kwa ajili ya jumbe Yakobo alitaka kusisitiza na kisha kupata jumbe hizo katika fumbo la miti ya mizeituni (ona Yakobo 5). Pengine washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kusikiliza kutoka kwa wale waliofanya shughuli hii au kutokana na kufanya shughuli hii kama darasa. Wanaweza kuorodhesha ubaoni kweli za injili wanazozipata katika Yakobo 6. Kisha, chini ya kila ukweli, wanaweza kuorodhesha mistari kutoka fumbo katika Yakobo 5 ambayo inatoa ujumbe ule. Washiriki wa darasa wameona jumbe hizi hizi zikielezwa vipi kwa mifano katika maisha yao wenyewe?
-
Maana moja ya neno gandamana ni kushikilia kwenye kitu fulani kwa uthabiti, kwa karibu, na bila kuyumbayumba. Unaweza kutaka kushiriki ufafanuzi huu pamoja na darasa lako na kuwauliza nini umaizi unawapa kuhusu Yakobo 6:5.
Tunaweza kusimama imara wakati wengine wanapojaribu imani yetu.
-
Wengi kati yetu tuna uzoefu wa upinzani kwa imani yetu kama vile Yakobo aliokabiliana nao wakati alipokutana na Sheremu. Njia moja ya kuwasaidia washiriki wa darasa kujiandaa kwa upinzani kama huo ni kuwataka wapekue Yakobo 7:1–23 kwa kanuni ambazo zilimsaidia Yakobo kusimama imara. Ni mifano gani mingine ya kusimama imara katika imani yetu tunaweza kushiriki—kutoka kwenye maandiko, historia ya familia, au maisha yetu wenyewe? Labda kuna jumbe kutoka viongozi wa Kanisa ambazo zimetusaidia wakati wengine walitafuta kutuondoa kutoka kwenye imani yetu (ona, kwa mfano, Quentin L. Cook“Imara katika Ushuhuda wa Yesu”,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 40–43). Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki jumbe walizoziona zina msaada.
-
Wakati Yakobo alipokabiliwa na Sheremu, Sheremu alitegemea kumwondoa Yakobo kutoka kwenye imani yake, lakini imani ya Yakobo haikutetereka (ona Yakobo 7:5). Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kuigiza majadiliano kati ya Yakobo na Sheremu wakitumia Yakobo 7:1–23 kama mswada. Tunajifunza nini kutoka mistari hii kuhusu mbinu na mafundisho ya wale ambao wanapinga kazi ya Mungu? Tunajifunza nini kutoka kwa Yakobo kuhusu jinsi ya kutoyumbishwa katika imani yetu?
Tunaweza kuamini katika Mungu.
-
Wanefi waliishi daima chini ya vitisho vya kushambuliwa na Walamani. Ingawa tunaweza tusikabiliwe na vitisho vya kila siku vya vita vya kimwili, hatari gani za kiroho tunazokabiliana nazo? Tunajifunza nini kutoka mjibizo wa Wanefi kwa hali yao, ilivyoelezwa katika Yakobo 7:24–25? Mnaweza kutaka kuimba au kusoma na kisha kujadili nyimbo za Kanisa ambazo zinatumia vita kama sitiari, kama vile “Onward Christian Soldiers” au “Behold! A Royal Army” (Hymns, nos. 246, 251).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Kuwatia moyo washiriki wa darasa kusoma kitabu cha Enoshi, waambie kwamba kinaweza kuwafundisha jinsi ya kufanya sala zao ziwe za maana zaidi.