Njoo, Unifuate
Februari 24–Machi 1. 2 Nefi 26–30: “Kazi Kuu na Maajabu”


“Februari 24–Machi 1. 2 Nefi 26–30: ‘Kazi Kuu na Maajabu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Februari 24–Machi 1. 2 Nefi 26–30,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Yesu akimyooshea mkono mwanamke

Atakuongoza wewe kwa mkono, na Sandra Rast

Februari 24–Machi 1

2 Nefi 26–30

“Kazi Kuu na Maajabu”

Kumbuka kwamba nyumbani panapaswa kuwa kitovu cha kujifunza injili. Mafunzo yako binafsi na familia ya 2 Nefi 26–30 yanapaswa kuwa msingi wa matayarisho yako ya kufundisha. Panga njia ya kujenga, kuimarisha, na kutia moyo mafunzo binafsi na familia ya watu katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Mwanzoni mwa somo, wape washiriki wa darasa nafasi ya kushiriki kitu fulani kutoka 2 Nefi 26–30 ambacho walikipata chenye maana walipojifunza nyumbani. Kwa mfano, unaweza kuwauliza kwa muhtasari kushiriki mstari ambao uliwasaidia kuelewa siku zetu na changamoto tunazokumbana nazo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

2 Nefi 26:24–28, 33

Kila kitu Bwana anachokifanya anatiwa hamasa na upendo Wake kwetu.

  • Kama unajihisi kuvutiwa kujadili mafundisho ya Nefi kuhusu upendo wa Mungu, unaweza kujaribu hii: baada ya kusoma 2 Nefi 26:24 pamoja, waombe washiriki wa darasa watengeneze orodha za vitu ambavyo Yesu Kristo amevifanya kwa ajili yao ambavyo vilihamasishwa na upendo. Jinsi gani Yeye “anawavuta wanadamu wote kwake”? Tunahisi vipi kuvutiwa kufanya katika kujibu madhihirisho Yake ya upendo?

  • Mialiko ya Bwana katika 2 Nefi 26:24–28, 33 ni yenye ushahidi wenye nguvu wa upendo Wake. Njia moja unayoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua mialiko hii ni kuwataka kufupisha ujumbe wa Bwana katika mistari hii na kuwa muhtasari wa sentensi moja. Labda washiriki wa darasa wachache watapenda kushiriki mihtasari yao. Mistari hii itaathiri vipi njia tunayowaalika wengine kuja kwa Kristo? Himiza darasa kuandika baadhi ya mawazo yao na hisia. Kualika Roho, fikiria kucheza wimbo uliorekodiwa kuhusu upendo wa Mwokozi, kama vile “Come unto Jesus” (Nyimbo, na. 117), wakati washiriki wa darasa wakitafakari.

2 Nefi 27; 29; 30:3–8

Kitabu cha Mormoni ni muhimu kwa kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

  • Watu katika darasa lako watahitaji msaada kidogo kuelewa utabiri katika 2 Nefi 27 kuhusu kitabu kilichofungwa kabisa na mtu msomi. Maelezo ya kihistoria katika “Nyenzo za ziada” zinaweza kusaidia. Je, itakubalika kwa darasa lako kama washiriki wachache wa darasa kwa ufupi waigize matukio yaliyoelezwa katika maelezo haya na katika 2 Nefi 27:15–22? Kwa nini Nefi ameweza kuoneshwa matukio haya miaka mingi sana kabla? Ni nini unabii wa Nefi unatufundisha kuhusu umuhimu wa Kitabu cha Mormoni? Wahimize washiriki wa darasa kushiriki jinsi walivyopata ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni.

  • Kuna yeyote katika darasa lako ambaye alipata uzoefu wa kumwalika mtu fulani kusoma Kitabu cha Mormoni ambacho wangeweza kishiriki? Ni baadhi ya sababu gani mtu fulani anaweza asikubali mwaliko kusoma Kitabu cha Mormoni? Jibu la Bwana kwa sababu moja kama hii linapatikana katika 2 Nefi 29:6–11. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma mistari hii na kuigiza jinsi wanavyoweza kwa upendo kumjibu mtu fulani anayesema kwamba Kitabu cha Mormoni sio muhimu. Je, ni mawazo gani mengine washiriki wa darasa wanayo kuhusu jinsi gani wanaweza kuwasaidia wengine “kujua kwamba [Kitabu cha Mormoni] ni baraka kwao kutoka mkono wa Mungu”? (2 Nefi 30:6).

2 Nefi 28

Shetani anatafuta kudanganya.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafuta uongo wa Shetani ulioelezwa katika 2 Nefi 28. Labda washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kile walichokipata, au wangeweza kukagua 2 Nefi 28 darasani na kuorodhesha uongo wa Shetani ambao wanautambua. Inaweza pia kusaidia kuwaacha wafanye kazi katika vikundi vidogo vidogo kutafuta maandiko ambayo yanakataa udanganyifu huu (kama wanahitaji msaada unaweza kushiriki mapendekezo katika “Nyenzo za Ziada”). Kisha makundi yanaweza kushiriki kile walichokipata na kujadili jinsi wanavyoweza kugundua “uongo na upuuzi na mafundisho ya kijinga” ya adui” (2 Nefi: 9).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Washiriki wa darasa wanaweza kuvutiwa kusoma 2 Nefi 31–33 kama wanajua kwamba sura hizi zina maneno ya mwisho yaliyoandikwa ya Nefi, pamoja na mojawapo ya maelezo rahisi sana na bado ya kueleweka ya mafundisho ya Kristo.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

“Kisha msomi atasema: Siwezi kukisoma” (2 Nefi 27:18).

Mnamo Februari 1828 Martin Harris, rafiki wa Joseph Smith, “alisafiri mashariki mpaka Jiji la New York pamoja na nakala za baadhi ya herufi kwenye mabamba ya [dhahabu] kuonesha kwa wanazuoni. Labda alitaka uhakika wa ziada kwamba mabamba yalikuwa ni ya halisi, au angeweza kufikiri hati ingewasaidia kukopa pesa kuchapisha tafsiri. Katika tukio lolote, alisisitiza kwamba Bwana alikuwa amemshawishi kufanya safari ile.

“Wakati ule, sio Joseph wala Martin aliyejua mengi kuahusu lugha kwenye mabamba. Walijua tu yale malaika Moroni alivyomwambia Joseph: kwamba ilikuwa kumbukumbu ya kale ya Merikani. Basi, kuliko kumtafuta msomi mwenye elimu ya Kimisri (Joseph baadae alijua kwamba lugha kwenye mabamba iliitwa ‘Kimisri kilichorekebishwa’), Martin aliwatembelea wanazuoni kadha wenye kupenda mambo ya kale, hususani mambo ya kale ya Merikani.

“… [Miongoni mwa wanazuoni Martin aliowatembelea alikuwa] profesa kijana wa sarufi na lugha kwenye Chuo cha Columbia. Anthon amekuwa akikusanya hadithi za Wahindi wa Merikani na misemo kwa ajili ya kuchapishwa na alikuwa na shauku ya kukagua hati Martin aliyomletea.

“Martin alidai kwamba Anthon alitangaza herufi ni za kweli mpaka alipoambiwa jinsi Joseph alivyozipata. Alipendekeza Martin amletee hayo mabamba. Martin alikataa, na Anthon akajibu, akifafanua mstari katika Isaya, ‘Siwezi kusoma kitabu kilichofungwa.’ Ingawa Anthon baadaye alikataa kila kitu cha maelezo ya Martin juu ya mkutano wao, tunajua hiki: Martin aliporudi kutoka matembezi yake ya wanazuoni wa mashariki akiwa amethibitisha zaidi kwamba Joseph Smith aliitwa na Mungu na kwamba mabamba na herufi zilikuwa za kale. Yeye na Joseph waliona ziara kwa Anthon kama kutimizwa kwa utabiri wa Isaya (pia imetamkwa katika Kitabu cha Mormoni chenyewe) ya ‘kitabu ambacho kimefungwa, ambacho mtu anampa mtu aliyeelimika akisema, soma hiki, ninakiomba: na anasema, siwezi; kwani kimefungwa‘ [Isaya 29:11; ona pia 2 Nefi 27:15–18]” (“Michango ya Martin Harris,” ufunuo katika muktadha [2016], 3–4, history.ChurchofJesusChrist.org).

Maandiko ambayo yanakanusha udanganyifu wa shetani.

mafundisho ya uongo

Mafundisho ya kweli

“Siku hii yeye sio Mungu wa miujiza; amefanya kazi yake” (2 Nefi 28:6).

Moroni 07:35–37

“Mungu … atatetea kutenda dhambi ndogo” (2 Nefi 28:8).

Mafundisho na Maagano 1:31;

“Yote yako salama Sayuni” (2 Nefi 28:21).

Mafundisho na Maagano 68:31; 82:14

“Mimi sio Ibilisi, kwani hakuna yeyote” (2 Nefi 29:22).

2 Nefi 2:17; Mafundisho na Maagano 76:25–27

“Hatuhitaji mengine zaidi ya neno la Mungu, kwani tuna ya kutosha” (2 Nefi 28:29).

2 Nefi 28:30; Makala ya Imani 1:9.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Usiogope ukimya. “Maswali mazuri huchukua muda kuyajibu. Wanahitaji kutafakari, kutafiti, na mwongozo. Muda unaotumia kungoja majibu kwa swali unaweza kuwa wakati mtakatifu wa kutafakari. Epukana na majaribu ya kukatiza muda huu haraka kwa kujibu swali lako mwenyewe au kwenda kwenye jambo lingine.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 31).