Njoo, Unifuate
Agosti 31–Septemba 6: “Habari Njema Shangwe Kuu”


“Agosti 31–Septemba 6. Helamani 13–16: ‘Habari Njema ya Shangwe Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 31–Septemba 6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Samweli Mlamani akifundisha juu ya ukuta

Samweli Mlamani Juu ya Ukuta, na Arnold Friberg

Agosti 31–Septemba 6

Helamani 13–16

“Habari Njema ya Shangwe Kuu”

Unapoandika misukumo yako wiki hii, fikiria jinsi kanuni katika Helamani 13–16 zinajenga na kuimarisha vitu vingine ambavyo umekuwa ukisoma katika maandiko.

Andika Misukumo Yako

Mara ya kwanza Samweli Mlamani alipojaribu kushiriki “habari njema” Kule Zarahemla (Helamani 13:7), alikataliwa na kufukuzwa na Wanefi wenye mioyo migumu. Unaweza kusema ilikuwa kana kwamba walikuwa wamejenga ukuta usioweza kuvunjwa kuzingira mioyo yao ambao uliwazuia kupokea ujumbe wa Samweli. Samweli alielewa umuhimu wa ujumbe alikuwa nao na akaonyesha imani kwa kufuata amri ya Mungu “kwamba anapaswa kurudi tena, na kutabiri ” (Helamani 13:3). Kama vile Samweli alivyofanya, sisi wote tunakabiliana na kuta tunapo “tayarisha njia ya Bwana” (Helamani 14:9) na kujitahidi kuwafuata manabii Wake. Na kama Samweli, sisi pia tunamshuhudia Yesu Kristo, “ambaye kwa kweli atakuja,” na tunawaalika wote ku “amini katika jina lake” (Helamani 13:6; 14:13). Sio kila mmoja atasikiliza, na wengine watatupinga kwa vitendo. Lakini wale ambao wanaamini katika ujumbe huu wakiwa na imani katika Kristo wanajua kwa kweli ni “habari njema ya shangwe kuu” (Helamani 16:14).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Helamani 13

Bwana hutoa maonyo kupitia manabii Wake.

Katika maandiko, manabii wakati mwingine wanalinganishwa na walinzi juu ya ukuta au mnara wanaoonya dhidi ya hatari Isaya 62:6; Ezekieli 33:1–7).

Rais M. Russell Ballard alifundisha: “Katika karne zilizopita, manabii wametimiza kazi zao wakati walipo waonya watu kuhusu hatari zilizo mbele yao. Mitume wa Bwana wana majukumu ya kulinda, kuonya, na kwenda kuwasaidia wale wanaotafuta majibu kwa maswali ya maisha” (“Mungu Yuko Usukani,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 25).

Unapojifunza na kutafakari Helaman 13, waweza kuwekea alama maonyo mengi Samweli aliyoyatoa. Kwa mfano, alifundisha nini kuhusu toba? kuhusu unyenyekevu na utajiri? Je, ni kwa jinsi gani maonyo haya yanatumika kwako? Ni maonyo yapi manabii wa siku zetu wametoa hivi karibuni, na unahisi unapaswa kufanya nini kuhusu maonyo hayo?

Picha
Rais Russell M. Nelson

Nabii hutuelekeza kwa Yesu Kristo.

Helamani 13–15

Bwana ni mwenye rehema kwa wale wanaotubu.

Mwanzo, Samweli alitumwa kwa Wanefi kushiriki habari ya shangwe za ujio wa Mwokozi (ona Helamani 13:7). Kwa sababu walimkataa, alirejea na maonyo makali ya hukumu za Mungu. Lakini maonyo hayo kwa uzito yalijumuisha mwaliko wa rehema wa kutubu; tafuta mialiko hii kote katika Helamani 13–15 (ona hasa Helamani 13:6, 11; 14:15–19; 15:7–8). Je, ni kwa jinsi gani mialiko hii inatumika kwako? Je, tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu toba? Ni lini umepata uzoefu wa rehema ya Mungu inayokuja kutokana na toba?

Helamani 14; 16:13–23

Ishara na maajabu vinaweza kuimarisha imani ya wale wasioshupaza mioyo yao.

Katika Helamani 14, Samweli alieleza sababu ya Bwana kutoa ishara za kuzaliwa na kufa kwa Mwokozi: “Kwa dhamira kwamba mngeamini katika jina lake” (Helamani 14:12). Unapojifunza Helamani 14, tambua ishara za kuzaliwa kwa Mwokozi mistari 1–8 na ishara za kifo chake katika mistari 20–28. Kwa nini unafikiri ishara hizi zingekuwa njia zenye ufanisi za kuonesha kuzaliwa na kifo cha Yesu Kristo?

Unaweza kufikiria ishara zozote Bwana alizotoa kukusaidia kumwamini Yeye? Kwa mfano, manabii wametabiri ishara ambazo zitatokea kabla ya Ujio wa Pili wa Mwokozi (ona “Ishara za Nyakati,” Mwongozo wa Maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Kuna ishara zozote ambazo zimetimia katika siku zetu? Ishara zingine zinazoelekeza kwenye imani katika Yesu Kristo zinaweza kuwa za kibinafsi zaidi na sio za kuvutia. Chukua muda ili kutafakari njia ulizo shuhudia Mkono Wake katika maisha yako.

Ni tahadhari gani limetolewa kuhusu ishara katika Helamani 16:13–23? Ni jinsi gani unaweza kuepuka tabia ya watu walioelezwa katika mistari hii?

Ona pia Alma 30:43–52; Ronald A. Rasband, “Kupitia Mpango Mtakatifu,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 55–57.

Helamani 16

Kufuata ushauri wa nabii kunanileta karibu na Bwana.

Mzee Neil L. Andersen alifundisha: “Nimegundua kwamba ninapojifunza kwa maombi maneno ya nabii wa Mungu na kwa uangalifu, pamoja na subira, kiroho nikiyaweka pamoja mapenzi yangu na mafundisho yake ya kutia moyo, imani yangu katika Bwana Yesu Kristo daima huongezeka. Ikiwa tutachagua kutupilia mbali ushauri wake na kuamua kwamba tunajua zaidi, imani yetu itaathirika na mtazamo wetu wa milele unafifia” (“Nabii wa Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 26–27). Ni jinsi gani maneno na vitendo vya Wanefi katika Helamani 16 vinathibitisha alichofundisha Mzee Andersen? Ni ahadi gani binafsi unahisi unapaswa kufanya kuhusu manabii wa Bwana na Ujumbe wao?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Helamani 13:3–4

Ni nini kinatia msukumo familia yako kuhusu jibu la Samweli kwa amri ya Bwana, katika Helamani 13:3–4? Wakati wa kujifunza kwenu kifamilia wiki hii, pengine ungeweza kuwatia moyo wanafamilia kushiriki mawazo ambayo “yanakuja kwenye mioyo [yao].”

Helamani 13:38

Dhana ya kuwa furaha inaweza kupatikana “kwa kutenda uovu” ni kawaida katika siku zetu. Ni kwa njia gani kuishi injili kumetuletea furaha ya kweli?

Helamani 15:3

Ni kwa jinsi gani kusahihishwa na Mungu kunaonyesha upendo Wake kwetu? Waalike wanafamilia kumuuliza Bwana kwa unyenyekevu kile wanachoweza kufanya ili wafanye vizuri zaidi.

Helamani 15:5–8

Je, tunajifunza nini kuhusu uongofu kutoka kwa Walamani walioelezwa katika aya hizi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wao?

Helamani 16:1–3

Je, familia yako inaweza kufurahia kuigiza hadithi ya Samweli Mlamani? Baada ya kusoma maelezo , pengine wanafamilia wanaweza kufanya zamu kusimama juu ya kiti na kusoma baadhi ya utabiri wa Samweli wakati wanafamilia wengine wakijifanya kurusha mishale au kutupa mawe. Hii yaweza kuisaidia familia yako kuelewa jinsi ambavyo Samweli na Wanefi yaweza kuwa walihisi. Watoto wadogo pia wanaweza kufurahi kuchora picha za hadithi. Ni jinsi gani tunaweza kuwa kama Samweli na kushiriki injili pamoja na wengine licha ya uwoga wetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Tafuta mpangilio. Mpangilio ni mpango au umbo linaloweza kutumika kama mwongozo wa kutimiza kazi. Katika maandiko, tunapata utaratibu ambao hutuonyesha jinsi ambavyo Bwana hutimiza kazi Yake, kama vile kuwatuma watumishi Wake kuwaonya watu.

Picha
Samweli Mlamani akifundisha

© The Book of Mormon for Young Readers, Samweli Mlamani, na Briana Shawcroft

Chapisha