Njoo, Unifuate
Septemba 14–20. 3 Nefi 8–11: “Inukeni na Mje Kwangu”


“Septemba 14–20. 3 Nefi 8–11: ‘Inukeni na Mje Kwangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Septemba 14–20. 3 Nefi 8–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Kristo anawatokea Wanefi

Mimi Ndimi Nuru ya Ulimwengu, na James Fullmer

Septemba 14–20

3 Nefi 8–11

“Inukeni na Mje Kwangu”

Katika 3 Nefi 8–11, watu walisikia sauti ya Mungu ikizungumza nao. Unaposoma sura hizi, tilia maanani kile ambacho sauti Yake inakuambia.

Andika Misukumo Yako

“Tazama, Mimi ni Yesu Kristo ambaye manabii walishuhudia atakuja ndani ya ulimwengu” (3 Nefi 11:10). Kwa maneno haya, Mwokozi aliyefufuka Alijitambulisha, na kutimiza unabii wa Kitabu cha Mormoni wa zaidi ya miaka 600. “Kutokea kule na tangazo lile ,” Mzee Jeffrey R. Holland aliandika, “lilijumuisha lengo kuu, wakati muhimu, katika historia yote ya Kitabu cha Mormoni. Ilikuwa ni onyesho na tangazo ambalo lilikuwa limetoa taarifa na kumtia msukumo kila nabii Mnefi. … Kila mtu alikuwa ameongea juu yake, kuimba juu yake, kuota juu yake, na kuomba kwa ujio wake—lakini hapa kwa kweli alikuwepo. Siku ya siku nyingi! Mungu ambaye anabadilisha kila usiku wa giza katika mwanga wa asubuhi alikuwa amefika” (Kristo na Agano Jipya [1997], 250–51).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

3 Nefi 8–11

Yesu Kristo ni Nuru ya Ulimwengu.

Unaweza kugundua dhamira zinazohusiana na giza na nuru—vyote kimwili na kiroho—zimerudiwa kotekote 3 Nefi 8–11. Unajifunza nini kutoka kwenye sura hizi kuhusu giza la kiroho na nuru? Nini huleta giza maishani mwako? Nini huleta nuru? Kwa nini unafikiria Yesu alichagua kujitambulisha Yeye Mwenyewe kama “nuru na uzima wa ulimwengu?? (3 Nefi 9:18; 11:11). Ni jinsi gani Yesu Kristo amekuwa nuru katika maisha yako?

3 Nefi 8–10

Kama nitatubu, Mwokozi atanikusanya, anilinde na kuniponya.

Je, unafikiria watu walihisi namna gani baada ya kushuhudia uharibifu na giza lililoelezewa katika 3 Nefi 8? Unafikiri wanaweza kuwa walihisi namna gani wakati walipoisikia sauti ya Bwana ikizungumza kuhusu nuru, rehema, na ukombozi katika sura za 9 na 10?

Ingawaje Mwokozi alitangaza kwamba ule uharibifu mkubwa ulikuwa matokeo ya dhambi za watu, Aliahidi kwamba angewaponya wale ambao wangerudi Kwake na kutubu (ona 3 Nefi 9:2, 13). Mzee Neil L. Andersen alisema: “Ninashangazwa na mikono ya Mwokozi inayozingira kwa rehema na upendo kwa wanaotubu, bila ya kujali dhambi iliyoachwa ilikuwa ya kibinafsi kiasi gani. Ninashuhudia ya kwamba Mwokozi anaweza na ana hamu ya kusamehe dhambi zetu” (“Tubu … Ili Niweze Kukuponya,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, –41).

Tafuta 3 Nefi 9–10 kwa ajili ya ushahidi wa rehema na utayari Wake kusamehe. Kwa mfano, ni nini unapata katika 3 Nefi 9:13–22 na 10:1–6 ambacho kinakusaidia kuhisi upendo na rehema ya Mwokozi? Tafakari uzoefu wakati ulipohisi “akikukusanya” na “kukulisha” wewe (ona 3 Nefi 10:4). Fikiria kuandika uzoefu huu katika shajara au kuushiriki pamoja na wapendwa wako.

3 Nefi 11:1–85

Naweza kujifunza kusikia na kuelewa sauti ya Mungu.

Je, umewahi kuhisi kana kwamba ulikuwa na wakati mgumu kuelewa ujumbe ambao Mungu alikuwa anawasilisha kwako ? Pengine uzoefu wa watu katika 3 Nefi 11:1–8 unaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya kanuni za kusikia na kuelewa sauti ya Mungu. Unaweza kugundua sifa za sauti ya Mungu ambayo watu waliisikia na kile walichofanya ili kuielewa vyema zaidi. Ni jinsi gani maelezo haya yanaweza kutumika kwenye juhudi zako za kusikia na kutambua sauti ya Mungu maishani mwako kupitia ufunuo binafsi?

3 Nefi 11:8–17

Yesu Kristo ananialika kutafuta ushuhuda binafsi juu Yake.

Kulikuwa na takriban watu 2,500 waliokusanyika kule Neema wakati Yesu Kristo alipotokea (ona 3 Nefi 17:25). Licha ya idadi hii kubwa, Mwokozi aliwaalika kila mtu “mmoja mmoja” waguse alama za misumari mikononi na miguuni Mwake (3 Nefi 11:14–15). Je hii inapendekeza nini kwako kuhusu umuhimu wa kuwa na uzoefu binafsi ambao unajenga imani katika Yesu Kristo? Ni katika njia zipi Mwokozi anakualika “kuinuka na kuja” Kwake.? (3 Nefi 11:14). Ni uzoefu upi umekuongoza kupata ushuhuda kwamba Yeye ni Mwokozi wako? Unaweza kufikiria pia jinsi mfano wa Mwokozi katika mistari hii unaweza kutia msukumo juhudi zako za kuwahudumia wengine.

Picha
Yesu akionyesha alama mikononi Mwake kwa Wanefi

Mmoja Mmoja, na Walter Rane

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

3 Nefi 8–9

Ili kuwasaidia wanafamilia wako kuhusisha uzoefu ulioelezewa katika 3 Nefi 8–9, ungeweza kusimulia au kusikiliza vipengele vilivyo rekodiwa vya sura hizi ndani ya chumba chenye giza. Jadilianeni vile ambavyo iliweza kuwa, kuwa katika giza kwa muda wa siku tatu. Kisha unaweza kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo Yesu Kristo ni “nuru … ya ulimwengu” (3 Nefi 9:18).

3 Nefi 10:1–6

Tamathali ya kuku akikusanya vifaranga vyake inaweza kuwa nyenzo yenye nguvu ya kufundushia kuwasaidia watoto kuelewa tabia na misheni ya Mwokozi. Unaweza kusoma mistari hii wakati familia yako inatazama picha ya kuku na vifaranga. Kwa nini kuku anaweza kuhitaji kukusanya vifaranga vyake? Kwa nini Mwokozi anataka kutukusanya tuwe karibu Naye? Ni nini kinaweza kutokea kama kifaranga atakaidi kukusanyika wakati anapoitwa?

3 Nefi 11:1–7

Pengine ungeweza kusoma baadhi ya aya hizi kwa ulaini, “sauti ndogo” (3 Nefi 11:3). Je, watu walihitaji kufanya nini ili waweze kuelewa sauti kutoka mbinguni? Tunajifunza nini kutokana na uzoefu wao?

3 Nefi 11:21–38

Je kuna yeyote katika familia yako anayejitayarisha kubatizwa? Kusoma 3 Nefi 11:21–38 kunaweza kusaidia kuwatayarisha. Je, ni kwa jinsi gani kutafakari mafundisho ya Mwokozi katika mistari hii kuna saidia wanafamilia ambao tayari wamebatizwa?

3 Nefi 11:29–30

Ni nini mistari hii inatufundisha kuhusu mabishano? Tunawezaje “[kuondolea] mbali” mabishano nyumbani kwetu?? (3 Nefi 11:30).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andika misukumo. Mzee Richard G. Scott alisema: “Maarifa yanayoandikwa kwa uangalifu ni maarifa unayoweza kuyatumia katika wakati wa shida. … [Kuweka kumbukumbu ya misukumo ya kiroho] zidisha uwezekano wako wa kupokea nuru zaidi” (“Kutafuta Ufahamu wa Kiroho,” Ensign, Nov. 1993, 88).

Picha
Kristo anawatokea Wanefi

Mchungaji Mmoja, na Howard Lyon

Chapisha