Njoo, Unifuate
Septemba 7–13. 3 Nefi 1–7: “Inua Kichwa Chako na Uchangamke”


“Septemba 7–13. 3 Nefi 1–7: ‘Inua Kichwa Chako na Uchangamke,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Septemba 7–13. 3 Nefi 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Wanefi wanashuhudia mchana bila usiku

Mchana Mmoja, Usiku Mmoja, na Siku Moja, na Jorge Cocco

Septemba 7–13

3 Nefi 1–7

“Inua Kichwa Chako na Uchangamke”

Wanefi walishuhudia ishara za ajabu, lakini baada ya muda walisahau kile walichokuwa wameshuhudia (ona 3 Nefi 2:1). Kuandika misukumo yako ya kiroho kutakuwezesha kukumbuka uzoefu wako wakati unapojifunza maandiko 3 Nefi 1–7.

Andika Misukumo Yako

Kwa namna fulani, ulikuwa wakati wa kusisimua kuwa mwaminifu katika Yesu Kristo. Unabii ulikuwa ukitimizwa—ishara kubwa na miujiza miongoni mwa watu iliashiria kuwa Mwokozi alikuwa karibu kuzaliwa. Kwa upande mwingine, ulikuwa ni wakati wa wasiwasi kwa waumini kwa sababu, licha ya miujiza yote, wasioamini walisisitiza kwamba “wakati umepita” wa kuzaliwa kwa Mwokozi (3 Nefi 1:5). Watu hawa walisababisha “makelele mengi kote nchini” (3 Nefi 1:7) na hata wakapanga siku ya kuwaua waumini wote kama ishara iliyotabiriwa na Samweli Mlamani—usiku bila giza—haingetokea.

Katika hali hizi za majaribu, nabii Nefi “aliomba kwa nguvu kwa Mungu wake kwa niaba ya watu wake” (3 Nefi 1:11). Jibu la Bwana ni la kutia msukumo kwa yeyote anayekabiliwa na mateso au wasiwasi na anahitaji kujua kwamba nuru itashinda giza: “Inua kichwa chako na uchangamke; … nitatimiza yote ambayo nimesababisha kuzungumzwa kwa midomo ya manabii wangu” (3 Nefi 1:13).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

3 Nefi 1:4–21; 5:1–3

Bwana atatimiza maneno Yake yote.

Unafikiri ungejihisi vipi kama ungekuwa mmojawapo wa waumini katika kipindi kilichoelezwa katika 3 Nefi 1–7? Je, inaweza kuwa ilihisiwa namna gani, kwa mfano, kusubiri kuja kwa usiku bila giza ambao ungetangaza kuzaliwa kwa Mwokozi, ukijua ya kwamba ungeuawa kama hilo halingetokea? Unaposoma 3 Nefi 1:4–21 na 5:1–3, angalia kile ambacho Nefi na waumini wengine walifanya kudumisha imani yao wakati wa nyakati hizi ngumu. Ni kwa namna gani Bwana aliwabariki? Ni nini unajifunza ambacho kinaweza kukusaidia wakati unajikuta ukisubiri kwa ajili ya baraka zilizoahidiwa na Mungu?

3 Nefi 1:22; 2:1–3

Kusahau uzoefu wa kiroho kunanifanya niwe hatarini dhidi ya majaribu ya Shetani.

Waweza kufikiria kwamba kushuhudia kitu cha kimiujiza sana kama usiku bila giza kungebakia nawe kwa muda mrefu na kuwa nanga ya ushuhuda wako. Lakini kumbukumbu za ishara na maajabu Wanefi walizoshuhudia vilionekana kupotea baada ya muda. Nini kiliwasababisha kusahau, na nini kilikuwa matokeo ya kusahau? (ona 3 Nefi 1:22; 2:1–3).

Je, unafanya nini ili kukumbuka na kufanya upya ushuhuda wako wa vitu vya kiroho? Kwa mfano, fikiria jinsi kuandika uzoefu wako wa kiroho kunavyoweza kukusaidia. Jinsi gani utashiriki ushahidi wako pamoja na wale walio karibu nawe ili kuwasaidia waamini?

Ona pia Alma 5:6; Henry B. Eyring, “Ee Kumbuka Kumbuka,” Ensign au Liahona, Nov. 2007, 66–69; Neil L. Andersen, “Imani Haiji kwa Bahati, ila kwa Kuchagua,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 65–68.

3 Nefi 2:11–12; 3:1–26; 5:24–26

Bwana huwaimarisha Watakatifu Wake dhidi ya hatari za kiroho.

Katika siku zetu, kwa kawaida hatukabiliani na magenge ya wanya’ganyi ambao wanatulazimisha kutoka manyumbani mwetu na kukusanyika mahali pamoja. Lakini tunakabiliana na hatari za kiroho, na uzoefu wa Wanefi waweza kuwa na mafunzo yanayoweza kutusaidia. Tafuta mafunzo haya unaposoma 3 Nefi 2:11–12 na 3:1–26.

Katika 3 Nefi 5:24–26 tunasoma kuhusu kukusanywa kwa watu wa Bwana katika siku za mwisho. Ni nini mistari hii inafundisha kuhusu jinsi Bwana anawakusanya watu Wake leo hii?

Ona pia “Worldwide Devotional for Youth: Messages from President Russell M. Nelson na Sister Wendy W. Nelson,” Juni 3, 2018, ChurchofJesusChrist.org; “Israel—The gathering of Israel,” Mwongozo wa Maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org.

3 Nefi 5:12–26; 7:15–26

Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo.

Unafikiri inamaanisha nini kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo? (ona MM 41:5). Katika 3 Nefi 5:12–26, Mormoni alikatiza ufupisho wake wa kumbukumbu za Wanefi na kutangaza kwamba alikuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo. Kisha, katika 3 Nefi 7:15–26, alielezea huduma ya mwanafunzi mwingine—nabii Nefi. Ni nini unapata katika vifungu hivi viwili ambacho kinakusaidia kuelewa maana ya kuwa mwanafunzi wa Mwokozi?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

3 Nefi 3:13–14, 25–26

Wanefi walifanya nini ili kujilinda dhidi ya adui waliye mkabili? Je, tunafanya nini ili kufanya nyumba zetu kuwa mahali pa usalama na ulinzi kutokana na maovu duniani?

3 Nefi 2:1–3; 6:15–17

Kuisaidia familia yako kuelewa jinsi Shetani anavyoweza kutudanganya, chora mwili, na wakati familia yako inaposoma 3 Nefi 2:1–3 na 6:15–17, weka alama sehemu tofauti za mwili zilizotajwa. Kulingana na mistari hii, ni baadhi ya njia zipi Shetani hutujaribu tumsahau Mungu na kugeukia dhambi?

3 Nefi 4:7–12, 30–33

Wanefi walifanya nini walipowaona wanyang’anyi wa Gadiantoni wakija? Je, familia yetu inaweza kujifunza nini kutoka kwa Wanefi wakati tunakumbana na hali ngumu? Tunaweza kujifunza nini kutokana na maneno ya Wanefi baada ya Bwana kuwasaidia wakati wa kipindi chao kigumu?

3 Nefi 5:13; Mafundisho na Maagano 41:5

Soma 3 Nefi 5:13 na Mafundisho na Maagano 41:5, na mjadiliane maana ya kuwa mwanafunzi wa Kristo. Pengine wanafamilia wanaweza kuzungumza kuhusu nyakati ambapo walitambuana kila mmoja akiwa mwanafunzi. Kama una watoto wadogo, unaweza kutengeneza beji inayosema, “Mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo,” na waruhusu waivae beji hiyo wakati wowote unapowatambua wanamfuata Mwokozi.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie familia yako wayalinganishe maandiko na wao wenyewe. Nefi alisema, “nililinganisha maandiko yote nasi, ili yatufundishe na kutuelimisha” (1 Nefi 19:23). Ili kuisaidia familia yako kulinganisha maandiko kwao wenyewe, unaweza kuwaalika watafakari kile ambacho wangefanya kama wangekuwa miongoni mwa waumini walioelezwa katika 3 Nefi 1:4–9. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21.)

Picha
Wanefi wanashuhudia mchana bila usiku

Mchana, Usiku, na Mchana, na Walter Rane

Chapisha