“Januari 7-13. 3Nefi 1-7: ‘Inua Kichwa Chako na Uchangamke,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Septemba 7–13 . 3 Nefi 1–7 Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Septemba 7–13
3 Nefi 1–7
“Inua Kichwa Chako na Uchangamke”
Roho Mtakatifu anaweza kukupa msukumo wa kufokasi katika kanuni maalum kutoka 3 Nefi 1–7 katika darasa. Hizo zinaweza kuwa kanuni tu ambazo zitambariki mtu fulani katika uhitaji.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza nyumbani, waombe waandike katika kipande cha karatasi baadhi ya kweli walizozipata katika 3 Nefi 1–7 na marejeleo ya maandiko kwa ajili ya hizo kweli. Weka vipande vya karatasi katika chombo, na toa vichache kwa ajili ya kujadiliana kama darasa. Wakati darasa likishiriki, fikiria kama kuna mawazo yanayohusiana katika muhtasari huu ambayo yanaweza kukuza kwa kina mjadala na kuwahusisha washiriki wengine wa darasa.
Fundisha Mafundisho
Uongofu ni mchakato ambao unahitaji juhudi endelevu.
-
3 Nefi 1–7 huelezea watu ambao waliongoka kwa Yesu Kristo na injili Yake na wengine ambao hawakuongoka. Ili kulisaidia darasa lako kutambua nini tofauti kati ya makundi haya , ungeweza kutengeneza chati ubaoni ikiwa na vichwa vya habari: imani na matendo ambayo hudhoofisha uongofu na imani na matendo yanayoimarisha uongofu. Gawanya marejeleo ya maandiko yafuatayo kati ya washiriki wa darasa, na waalike kujaza chati kwa kile wanachokipata (mifano imetolewa kwa ajili ya rejeleo la kwanza).
-
3 Nefi 1:4–23, 29–30: Hudhoofisha uongofu: kutoamini maneno ya manabii na kukejeli wenye haki (mstari wa 5–6). Huimarisha uongofu: kuwa na imani katika maneno ya manabii na kusali kwa ajili ya msaada (mstari 8,11).
Je, tunawezaje kuuweka uongofu wetu imara bila kujali upinzani?
-
-
Darasa lako linaweza kuvutiwa na kuchunguza jinsi ya kuimarisha kile 3 Nefi 1:27–30 hukiita “uovu wa vijana wa kizazi hiki.” Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutafuta sababu katika mistari hii kwa nini Wanefi vijana na Walamani hawakuweza kuzuia uovu uliokuwa ukiwazunguka. Hii inaweza kupelekea majadiliano kuhusu baadhi ya changamoto zinazokikabili kizazi chipukizi cha sasa na njia sahihi zaidi ya kuwasaidia kukuza imani katika Yesu Kristo. Baadhi ya mifano imetolewa katika “Nyenzo za Ziada.”
Bwana Atatimiza Ahadi Zake Zote.
-
Kusoma matukio kutoka 3 Nefi 1:4–21 na 5:1–3 kunaweza kuimarisha imani ya darasa lako katika ahadi za Bwana Labda washiriki wa darasa wangesoma kwa pamoja 3 Nefi 1:4–7 na kuorodhesha jinsi wangehisi kama wangekuwa waaminio walioelezewa katika mistari hii. Wangeweza pia kufikiria hali sawa na ambayo tungeweza kukumbana nayo hivi leo. Je, tunajifunza nini kutoka 3 Nefi 1:8–21 na 5:1–3 kuhusu Bwana na ahadi Zake? Ili kukuza majadiliano, ungeweza kurejelea wimbo kuhusu kumuamini Mungu, kama vile “Wakati Imani Inapovumilia” (Nyimbo za Kanisa, namba. 128). Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati imani yao na kumuamini Mungu vilizawadiwa, licha ya upinzani.
3 Nefi 1:4–15; 5:12–26; 6:10–15; 7:15–26
Sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo.
-
Mormoni alitamka, “Tazama, mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo” (3 Nefi 5:1). Ili kuchunguza pamoja na darasa lako nini humaanishwa kuwa mwanafunzi, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuchunguza 3 Nefi 1:4–15; 5:12–26; 6:10–15; na 7:15–26, wakitafuta sifa, imani, na matendo ya wanafunzi wa Kristo. Fikiria kuwapa washiriiki wa darasa dakika chache kutafakari na kuandika kitu ambacho wanaweza kufanya ili kuwa wanafunzi bora zaidi wa Yesu Kristo.
3 Nefi 2:11–12; 3:12–26; 5:24–26
Wakati wenye haki wanapokusanyika, Bwana anaweza kuwaimarisha na kuwalinda.
-
Sehemu ya sababu ya kwa nini Wanefi waliweza kuwashinda wezi wa Gadiantoni ilikuwa ni kwamba waliunganisha nguvu na Walamani waliokuwa kwenye agano na kufuata mwongozo wa Lakoneyo wa “kujikusanya pamoja” katika mji wa Zarahemla (3 Nefi 3:22). Je, hili linaweza kuwa limebeba somo gani kwa washiriki wa darasa? Ungeweza kuwauliza kushiriki uzoefu ambapo waliimarishwa na watu wema wanaowazunguka. Kisha ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kurejelea 3 Nefi 3:12 –26, wakitafuta sababu ya kwa nini Wanefi walikusanyika na baraka walizozipata. Je, ni kwa namna gani tunapitia baraka kama hizo wakati tunapokusanyika na wanafamilia wetu au matawi yetu au kata zetu? Je, tunaweza kujifunza nini zaidi kuhusu kukusanyika kutoka 3 Nefi 5:24–26?
-
Kusoma 3 Nefi 3 kungeweza kuwa fursa ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi gani tuna nguvu zaidi wakati tunapokusanyika pamoja katika haki. Pengine ungeweza kufikiria juu ya somo kwa vitendo ambalo huonyesha kitu fulani ambacho ni dhaifu kuwa chenye nguvu wakati kinpoungana na vitu vingine. Waalike washiriki wa darasa kujifikiria kuwa waliulizwa kuwashawishi Wanefi juu ya manufaa ya kukusanyika pamoja, kama ilivyoelezewa katika mstari wa 12–26. Labda wangefanya kazi katika makundi kujadiliana jinsi ya kufanya hili, wakizingatia juu ya kile walichosoma katika mistari hii. Wape nafasi ya kushiriki mawazo yao. Kisha kama darasa, mngeweza kujadiliana maswali kama haya: Ni changamoto zipi tunazokumbana nazo ambazo zingeweza kufananishwa na wezi wa Gadiantoni? Je, tunawezaje kuzifanya nyumba zetu na kata sehemu za kimbilio?
Hatuhitaji kumuogopa Shetani.
-
Barua iliyoandikwa na Gidiani, kiongozi wa wezi wa Gadiantoni, ilikuwa ni jaribio la kuwatishia na kuwadanganya Wanefi. Pengine washiriki wa darasa wangerejelea maneno yake katika 3 Nefi 3:2–10 na kuyalinganisha na njia Shetani anajaribu kutudanganya hivi leo. Je, tunajifunza nini kutokana na mwitikio wa Lakoneyo, mwamuzi mkuu wa Wanefi?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kulitia hamasa darasa lako kusoma 3 Nefi 8–11 kwa ajili ya darasa la wiki ijayo, waambie kwamba 3 Nefi 11 inabeba “tukio la kilele” la Kitabu cha Mormoni—huduma binafsi ya Yesu Kristo miongoni mwa Wanefi (ona dibaji ya Kitabu cha Mormoni).
Nyenzo za Ziada
Kusaidia kujenga imani katika kizazi chipukizi.
Mzee Valeri V. Cordón wa Wasabini alipendekeza njia tatu za kusaidia kizazi chipukizi kubakia wakweli katika injili:
-
“Kuwa mwenye bidii zaidi na mwenye kujali Nyumbani. … Mafundisho yenye nguvu ni muhimu sana kutunza injili katika familia zetu, na inahitaji juhudi na bidii. Tumealikwa mara nyingi kutafuta mazoea ya kujifunza maandiko binafsi na kama familia. Familia nyingi ambazo zinafanya hivi zinabarikiwa kila siku kwa umoja mkubwa na uhusiano wa karibu pamoja na Bwana.
-
“Mfano wenye nguvu nyumbani. … Haitoshi tu kuongea na watoto wetu kuhusu umuhimu wa ndoa ya hekaluni, kufunga, na kuitunza siku ya Sabato takatifu. Lazima watuone tukitenga muda katika ratiba zetu kuhudhuria hekaluni mara nyingi tuwezavyo. Wanahitaji kuona kujitolea kwetu katika kufunga kila mara na kuiweka siku nzima ya Sabato takatifu.”
-
“Desturi. … Kama familia, tunahitaji kuepuka desturi zozote ambazo zitatuzuia kuiweka siku ya Sabato takatifu au kuwa na kujifunza maandiko kila siku na kusali nyumbani. Tunahitaji kufunga milango yetu ya kidijitali ya nyumbani dhidi ya ponografia na ushawishi wowote wa mwovu. Ili kujikinga na desturi za kidunia za siku yetu, tunahitaji kutumia maandiko na sauti za manabii wetu wa leo kufundisha watoto wetu kuhusu uhalisia wa utambulisho wao mtakatifu, lengo lao katika maisha, na kazi tukufu ya Yesu Kristo”(“Lugha ya Injili,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 56–57; maneno ya mlalo yameongezwa).