Njoo, Unifuate
Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4: “Hakungekuwepo na Watu Wenye Furaha Zaidi”


“Oktoba 19–25. 3 Nefi 27–4: ‘Hakungekuwepo na Watu Wenye Furaha Zaidi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Oktoba 19–25. 3Nefi 27–4,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Yesu Akisali pamoja na Wanefi

Sala ya Kristo na Derek Hegsted

Oktoba 19–25.

3 Nefi 274 Nefi

“Hakungekuwepo na Watu Wenye Furaha Zaidi”

Kujifunza binafsi 3 Nefi 274 Nefi ni njia nzuri zaidi ya kujiandaa kufundisha. Mafundisho na mawazo katika muhtasari huu yanaweza kukusaidia kuitikia misukumo ya kiroho unayoipokea wakati ukijifunza.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia mojawapo ya kuwahamasisha washiriki wa darasa kushiriki umaizi kutoka katika kujifunza kwao ni kwa kuwaalika kutafuta wimbo wa kanisa unaohusiana na ukweli waliojifunza katika 3 Nefi 274 Nefi. Kisha wangeweza kushiriki nyimbo za kanisa walizozipata na jinsi nyimbo hizi zinavyohusiana na kweli katika maandiko.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

3 Nefi 27:1–22.

Kanisa la Yesu Kristo linaitwa kwa jina Lake na limejengwa juu ya injili Yake.

  • Kujadili kuhusu jina la Kanisa kunaweza kuongeza kwa kina shukrani ya washiriki wa darasa lako kwa uumini wao katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha majina ya taasisi tofauti tofauti na kuelezea kile majina hutuambia kuhusu taasisi hizo. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kusoma 3 Nefi 27:1–12, wakitafuta kile Mwokozi alikifundisha kuhusu jina la Kanisa Lake. Pia wangeweza kushiriki kile inachomaanisha kwa kuwa waumini wa Kanisa la Kristo. Je, humaanisha nini kwa sisi kujichukulia jina Lake juu yetu?

  • Hapai kuna njia njyingine ya kujadiliana umuhimu wa jina la Kanisa la Mwokozi. Baada ya kujadiliana kweli zipatikanazo katika 3 Nefi 27: 1–22, ungeweza kuandika jina kamili la Kanisa ubaoni. Kisha washiriki wa darasa wangechagua maneno katika jina na kupendekeza jinsi kila neno hutusaidia kujua sisi ni akina nani au nini tunachokiamini. Kauli ya Rais M. Russell Ballard katika “Nyenzo za Zaida” ingeweza kusaidia. Je, kwa nini ni muhimu kutumia jina la Kanisa wakati tunaposhiriki imani yetu na wengine?

  • Baada ya kufafanua kwama Kanisa Lake lazima “lijengwe juu ya injili [Yake]” (3 Nefi 271:10), Mwokozi alielezea injili Yake ni nini. Labda ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi wangeweza kufafanua kwa rafiki injili ni nini. Kisha ungeweza kuwaalika kuchunguza 3 Nefi 27:13–22, wakitafuta jinsi Mwokozi alivyoilezea injili Yake. Je, ungeweza kufupisha vipi kile Mwokozi alikisema? Wakati tukijifunza maana ya injili aliyotoa Mwokozi, Je, ni umaizi gani tunaoupata kuhusu jinsi ya kuishi injili katika maisha yetu ya kila siku?

3 Nefi 29–30

Kitabu cha Mormoni ni ishara kwamba kazi ya siku za mwisho ya Mungu inatimizwa.

  • Pengine ungeweza kuanza majadiloiano kuhusu 3 Nefi 29–30 kwa kuzungumzia kuhusu ishara. Kwa mfano, washiriki wa darasa wangeweza kusema ishara ambazo zinatufanya kujua kwamba tufani inakuja au kwamba majira yanabadilika. Wangeweza kusoma 3 Nefi 29:1–3 kujifunza nini kinamaanishwa kwa ujio wa Kitabu cha Mormoni, ambao Mormoni aliuita “maneno haya” (ona pia 3 Nefi 21:1–7). Je, ni ujumbe gani Bwana aliutoa katika 3 Nefi 29:4–9 kwa wale ambao “wanapinga” na “kukataa” kazi ya Mungu katika siku za mwisho? Je, ni kwa namna gani kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku huimarisha imani yetu katika vitu vile ambavyo watu wengine “huvipinga” na “kuvikataa” katika siku zetu? Ungeweza kutaka kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mwaliko wa Bwana katika 3 Nefi 30 na kushiriki jinsi Kitabu cha Mormoni kinawasaidia wao kuukubali mwaliko huu.

4 Nefi

Uongofu katika Yesu Kristo na injili Yake hupelekea umoja na furaha.

  • Tukio katika 4 Nefi linaelezea shangwe ambayo huweza kuja katika maisha yetu—kama watu binafsi, na kama familia, na kama kata au kigingi—wakati tukijaribu kuwa waongofu zaidi katika Yesu Kristo. Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kuchunguza 4 Nefi 1:1–18 na waandike ubaoni baraka ambazo huja kwa watu wakati wote walipokuwa wameongoka katika Bwana. Je, ni kwa namna gani uongofu wao unaathiri jinsi wanavyowachukulia wengine? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi injili imeleta baraka sawa kwa familia zao au kata yao. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi kila mmoja wetu anaweza kuishi kama watu katika 4 Nefi na jinsi tunavyoweza kuhamasiha umoja wenye nguvu na furaha kati ya wale wanotuzunguka, ungeweza kusoma maelezo ya Mzee D. Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa wangeweza kujifanyia uchunguzi juhudi zao binafsi katika maeneo matatu aliyoyaelezea Mzee Christofferson.

  • Watu katika Kitabu cha Mormoni walijitofautisha kama Wanefi na Walamani—na wengine kama wa “uzao mwingine”—kwa karne nyingi, lakini huduma ya Mwokozi kati yao, ilitoa tofauti hizi. Baada ya kusoma 4 Nefi 1:17 kwa pamoja, pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mawazo yao kuhusu aina ya “vizazi tofauti” au makundi yaliyopo katika jamii yetu. Je, tunaweza kufanya nini kushinda mgawanyiko huo na kweli kuwa “ wamoja, watoto wa Kristo”? (mstari wa 17).

  • Je, washiriki wa darasa wanajifunza nini kutokana na anguko la jumuiya ya Sayuni lilioelezewa katika 4 Nefi? Ungeweza kuwaalika wao kuchunguza 4 Nefi 1: 19–34, wakitafuta kile kilichositisha furaha na umoja wa watu walioupata takribani miaka 200 baada ya kutembelewa na Mwokozi. Je, ni kweli zipi katika mistari hii zinaweza kutusaidia kutambua mitazamo na tabia ambazo zinahitajika kubadlishwa katika maisha yetu na katika jamii yetu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Mormoni 1–6 inaelezea matukio ya kuhuzunisha ambayo yalipekea kuharibiwa kwa Wanefi. Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma sura hizi, waalike kutafuta vitu ambavyo wanaviona kuhusu Wanefi ambavyo tunaviona vikitokea katika siku zetu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Jina la Kanisa la Kristo.

Mzee M. Russell Ballard alisema:

“Nimetafakari sana kuhusu Mwokozi kutoa jina kwa maneno tisa kwa Kanisa Lake lililorejeshwa. linaweza kuonekana ni refu, lakini kama tutalitafakari kama ufafanuzi wa jinsi Kanisa lilivyo, mara moja huwa ufupisho wa kupendeza, wa kuvutia na, na wa moja kwa moja. Inawezekanaje ufafanuzi wowote uweze kuwa wa moja kwa moja na wa kueleweka lakini uliolezewa kwa maneno machache?

“Kila neno linafafanua na ni la lazima. Neno Kanisa huonyesha nafasi ya kipekee ya Kanisa la urejesho kati ya dini zilizopo ulimwenguni.

“Maneno Kanisa la Yesu kristo hutoa tamko kwamba ni Kanisa Lake. [ona 3 Nefi 27:8]. …

La Watakatifu wa Siku za Mwisho yanaeleze kuwa ni Kanisa sawa ni lile Kanisa Yesu Kristo alianzisha wakati wa huduma Yake duniani lakini limerejeshwa katika siku hizi za mwisho. Tunajua kulikuwa na kuanguka, au ukengeufu, uliolazimu Urejeshwaji wa Kanisa Lake la kweli na lililokamilika katika nyakati zetu.

Watakatifu humaanisha kwamba waumini wake wanamfuata Yeye na kujitahidi kufanya mapenzi Yake, kushika amri Zake, na kujiandaa tena kuishi na Yeye na Baba yetu wa Mbinguni katika wakati ujao. Watakatifu kiurahisi humaanisha wale wanaotafuta kufanya maisha yao kuwa matakatifu kwa kuweka maagano na kumfuata Kristo” (“Umuhimu wa Jina,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 80).

Je, nini kinahitajika ili kuijenga Sayuni?

Mzee D. Todd Christopherson alifundisha: Sayuni ni Sayuni kwa sababu ya sifa, mtazamo, na uaminifu wa wakazi wake [ona Musa 7:18]. … Kama tungeanzisha Sayuni katika nyumba zetu, matawi, kata, na vigingi, lazima tuinuke katika kiwango hiki. Itakuwa muhimu (1) kuunganika katika moyo mmoja na wazo moja; (2) kuwa binafsi na kwa umoja, watu watakatifu; na (3) kuwatunza maskini na wenye mahitaji kwa juhudi kubwa kwamba tuondoe umasikini kati yetu. Hatuwezi kusubiri mpaka Sayuni iJe, ili vitu hivi vifanyike—Sayuni itakuja tu ikiwa vitafanyika” (“Njoo Sayuni,” Ensign au Liahona Nov. 2008,38).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia njia mbali mbali. Inaweza kuwa rahisi kuridhika na aina fulani ya ufundishaji, lakini njia mbali mbali za ufundishaji huwafikia washiriki tofauti wa darasa. Fikiria kuhusu njia ambazo umetumia hivi karibuni—Je, umetumia hadithi, masomo kwa vitendo, picha, na vinginevyo? (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,7).

Chapisha