Njoo, Unifuate
Oktoba 26–Novemba 1. Mormoni 1–6: “Ningeweza Kwamba Ningewashawishi Wote … Kutubu”


“Oktoba 26–November 1. Mormoni 1–6: ‘Ningeweza Kwamba Ningewashawishi Wote … Kutubu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

‘Oktoba 26–November 1. Mormoni 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Mormoni akiandika kwenye bamba za dhahabu

Mormon Akifupisha Maandishi kwenye Mabamba, na Tom Lovell

Oktoba 26–Novemba1

Mormoni 1–6

“Ningeweza Kwamba Ningewashawishi Wote … Kutubu”

Wakati ukisoma Mormoni 1–6, tafuta kweli ambazo zinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kubakia waaminifu katika nyakati za uovu, kama Mormoni alivyofanya.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati mwingine washiriki wa darasa wanasita kushiriki umaizi wao kwa sababu hawajawahi kuwa na muda wa kupangilia mawazo yao. Ili kuwasaidia katika hili, wape dakika chache kuandika umaizi wao walioupata kutoka katika kujifunza Mormoni 1–6 nyumbani; kisha waombe kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mormoni 1–6

Tunaweza kuishi kwa haki bila kujali uovu unaotuzunguka.

  • Wengi wa washiriki wa darasa lako wanaweza kuelewa uzoefu wa Mormoni katika kujitahidi kuishi kwa haki katika ulimwengu wenye uovu. Labda wangeweza kushiriki kile wanachojifunza kutoka katika uzoefu wa Mormoni. Ili kusaidia katika mjadala huu, ungeweza kuwaalika washirki wa darasa kutafuta mistari ambayo inaonyesha tabia za Mormoni na watengeneze orodha ya tabia hizo ubaoni (ona, kwa mfano, Mormoni 1:2–3, 15–16; 2:1, 23–24; 3:1–3, 12, 17–22). Je, ni kwa namna gani sifa hizi zimemsaidia Mormoni kubakia imara kiroho? Je, zinawezaje kutusaidia sisi kuwa kama Mormoni?

    Picha
    Wanefi na Walamani wakipigana vita wao kwa wao.

    Vita, na Jorge Cocco

  • Mormoni mara nyingi aliandika moja kwa moja kwa watu wa siku zetu. Je, tunawezaje kujifunza kutoka katika maneno yake kwetu katika Mormoni 3:17–22 and 5:10–24? Mpe kila mshiriki wa darasa kipande cha karatasi kikiwa na kirai “ushauri wa Mormoni kwetu” kikiwa kimeandikwa juu, na wahamasishe kutafuta jumbe katika mistari hii ambayo ina manufaa katika siku zetu. Je, tunawezaje kutumia ushauri wa Mormoni kutusaidia kubakia imara kiroho katika ulimwengu wa leo?

  • Kama unawafundisha vijana, ungeweza kutumia mfano wa Mormoni kuwasaidia kuelewa kwamba wanaweza kuwa viongozi wenye haki wakati bado wakiwa wadogo. Kama unawafundisha watu wazima, ungeweza kutumia mfano huu kuhamasiha majadiliano kuhusu fursa za kuwasaidia vijana kuwa viongozi wazuri. Kwa kuanza majadiliano, ungeweza kuwaomba baadhi ya washiriki wa darasa kurejelea Mormoni 1 na wengine kurejelea Mormoni 2, wakitilia maanani fursa ambazo Mormoni alipewa kuongoza katika kipindi cha miaka yake ya mwanzo. Ni sifa zipi alikuwa nazo ambazo zilimfanya kuwa kiongozi mkuu? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano ambayo wameiona ya ushawishi wenye nguvu wa watoto na vijana watakatifu. Wangeweza pia kujadiliana juu ya fursa ambazo wao—au vijana wanaowajua—wanazo ili kuwa viongozi wenye sifa kama alizokuwa nazo Mormoni

Mormoni 2:10–15

Toba huitaji moyo uliovunjika na roho iliyopondeka.

  • Ili kujifunza kuhusu tofauti kati ya huzuni ambayo hupelekea toba na huzuni ambayo haipelekei hilo, fikiria kusoma Mormoni 2:10–15 kwa pamoja na kujadiliana maswali kama haya: Je, “huzuni” ina kazi gani katika toba? Je, kuna tofauti gani kati ya “huzuni ipelekeayo toba” na “huzuni ya aliyelaaniwa”? Je, ni mtazamo gani na tabia zipi zinaweza kutusaidia kuwa na “moyo uliovunjika na roho iliyopondeka”?

Mormoni 3:12

Tunaweza kuwapenda wengine, hata kama hatukubaliani na chaguzi zao.

  • Kama Mormoni, wengi wa washiriki wa darasa lako wanahusiana kwa ukaribu na watu ambao hawashiriki imani yao. Je, ni kwa namna gani ungeweza kutumia uzoefu wa Mormoni kufundisha washiriki wa darasa kuhusu kuwapenda wengine bila kujali tofauti zao? Fikiria kusoma Mormoni 3:12 kwa pamoja na kujadiliana nyakati ambapo Mormoni alionyesha upendo kwa wale ambao walikataa ujumbe wake na kwa kujua kuasi dhidi ya Mungu (ona, kwa mfano, Mormoni 1:16–17; 2:12). Je, ni uzoefu upi wshiriki wa darasa wanaweza kuushiriki kutoka katika maisha yao wenyewe wa kuwapenda wale ambao hawakushiriki imani yao au maadili? Maelezo ya Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” yanatoa ushauri wa ziada.

Mormoni 6:17

Yesu Kristo amesimama na mikono iliyokunjuliwa kutupokea.

  • Kwa wale ambao wanaweza kutokuwa na tumaini kwamba wanaweza kusamehewa dhambi zao, maelezo ya Mormoni kuhusu Mwokozi akisimama “na mikono iliyokunjuliwa kutupokea” yangeweza kutoa uhakika. Fikiria kusoma Mormoni 6:17 kwa pamoja na onyesha picha ya Yesu Kristo akiwa amekunjua mikono (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili namba. 66). Je, mstari huu unafundisha nini kuhusu hamu ya Mwokozi kutusaidia? Ungeweza pia kufikiria kuimba wimbo wa kanisa kwa pamoja ambao unafundisha ujumbe sawa na huo kama “Njoo kwa Yesu” (Nyimbo za Kanisa, namba 117). Pia ungeweza kushiriki uzoefu wa Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Zaida” na waombe washiriki wa darasa kujadiliana jinsi tunavyoweza kuwasaidia wengine kutambua kwamba toba inawezekana.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kuhusu nini wangeweza kukiandika katika barua kwa watu katika siku sijazo. Katika Mormoni 7–9 tunasoma kile Mormoni na Moroni walikiandika, miongo mingi iliyopita, kwa watu katika siku zetu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuwapenda wengine wenye imani tofauti.

Rais DallinH. Oaks alifafanua:

“Sote hatuna budi kufuata mafundisho ya injili ya kuwapenda jirani zetu na kuepuka mabishano. Wafuasi wa Kristo hawana budi kuwa mfano wa ustaarabu. Tunapaswa kuwapenda watu wote, kuwa wasikilizaji wazuri, na kuonyesha kujali imani yao ya dhati. Ingawa tunaweza kutofautiana, tusiwe wasiokubaliana. Msimamo wetu na maongezi yetu katika mada zenye utata hakutakiwi kuwa kwa mabishano. Hatuna budi kuwa wenye busara katika kufafanua na kutafuta msimamo wetu na katika kutumia ushawishi wetu. Kwa kufanya hivyo, tunaomba kwamba wengine wasichukizwe na imani za kweli za dini yetu na uhuru wa kutumia dini yetu. Tunawahimiza wote kutekeleza Sheria Muhimu ya Mwokozi. ‘Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo’ (Mathayo 7:12).

“Wakati misimamo yetu hauchukuliwi, hatuna budi kukubali matokeo yasiyopendeza kwa ukarimu na kutumia ustaarabu kwa wajaribu wetu” (“Kuwapenda wengine na Kuishi na Utofauti,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 27).

Toba inawezekana.

Rais Russell M. Nelson alishiriki uzoefu ufuatao:

“Mwaka jana wakati Mzee David S. Baxter pamoja nami tulipokuwa tukiendesha kwenda katika mkutano wa kigingi, tulisimama katika mgahawa. Baade wakati tukirudi katika gari yetu, tulifuatwa na mwanamke ambaye alituita kwa nguvu. … Alituuliza kama tulikuwa wazee katika kanisa. Tukasema ndio. Karibu bila kujizuia, alituambia hadithi ya maisha yake ya kutisha, akimezwa na dhambi. Sasa, miaka 28 tu, alikuwa hajisikii vizuri. Alihisi kutokuwa na thamani, bila sababu yoyote ya kuishi. Wakati akiongea, uzuri wa nafsi yake ukaanza kutokeza. Akiomba kwa dhati kwa machozi, aliuliza kama kulikuwa na tumaini lolote kwa ajili yake, na njia ya kutoka katika kukosa kwake matumaini.

“‘Ndio,’ tulijibu, ‘kuna tumaini. Tumaini limeunganishwa katika toba. Unaweza kubadilika. Unaweza “njoo kwa Kristo, na ukamilishwe ndani yake”’[Moroni 10:32]. Tulimuomba kwamba asihairishe [ona Alma 13:27; 34:33]. Alilia kwa nguvu na kutushukuru kwa dhati.

“Wakati Mzee Baxter pamoja nami tulipoendelea na safari yetu, tulitafakari uzoefu ule. Tulikumbuka ushauri ulitolewa na Haruni kwa nafsi isiyo na tumaini, ambaye alisema ‘ ikiwa utatubu dhambi zako zote, na umsujudie Mungu, na umlingane kwa imani, … ukiamini kwamba utapokea, ndipo utakapopokea matumaini ambayo unatamani’ [Alma 22:16]. …

“… Kwa mwanamke wa miaka 28 aliyenaswa katika dimbwi la dhambi, na kwa kila mmoja wetu, ninatangaza kwamba baraka tamu za toba zinawezekana. Huja kupitia uongofu wa kweli kwa Bwana na kazi Yake takatifu.”

Kwa kuongezea, Rais Nelson aliona: “Pia tunakumbuka watu wenye dhambi chini ya uongozi wa kiongozi mwenye kujali, Mormoni, ambaye aliandika ‘Lakini tazama, sikuwa na tumaini, kwani nilijua hukumu ya Bwana ambayo ingewajia; kwani hawakutubu uovu wao, lakini walipigania maisha yao bila kumlingana yule ambaye Aliwaumba’ (Mormoni 5:2)” (“Toba na Uongofu,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 102, 104).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ukuaji wa kiroho hutokea nyumbani. Washiriki wa darasa lako wanatumia masaa 165 kila wiki nje ya kanisa. Katika wakati huo, wana uzoefu wao wenyewe wa kiroho ambao unawafundisha kuhusu injili. Uliza maswali ambayo yanawahamasisha wanafunzi kushiriki vitu ambavyo wamejifunza katika wiki na pamoja na familia zao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,18).

Chapisha