“Novemba 23–29. Mosia 12–15 : ‘Kwa Imani Mambo Yote Yanatimizwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Novemba 23–29. Etheri 12–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Novemba 23-29
Etheri 12–15
“Kwa Imani Mambo Yote Yanatimizwa”
Lengo la muhtasari huu si kuamrisha nini kinatakiwa kufanyika darasani. Ni nyongeza ya—na si kuchukua nafasi kwa ajili ya—ufunuo binafsi. Acha Roho aongoze kujifunza kwako binafsi na maandalizi, na kisha angalia kama shughuli katika muhtasari huu zingeweza kuwasiadia washirikiwa darasa kugundua na kushiriki kanuni muhimu katika Etheri 12–15
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia washirikiwa darasa kushiriki kile walichojifunza kutoka katika kusoma kwao binafsi maandiko na kama familia, ungeweza kuandika ubaoni virai kama “nimejifunza kwamba …” “nina ushuhuda wa …” na “nimepata uzoefu wa …” waalike washiriki wa darasa kushiriki kitu fulani kutoka Etheri 12–15 ambacho kingekamilisha moja ya virai katika ubao.
Fundisha Mafundisho
Tunaweza kupokea msamaha wa dhambi zetu tunapofanya imani katika Yesu Kristo.
-
Ili kuwasidia washiriki wa darasa kutafakari nini kinamaanishwa kutumia imani katika Yesu Kristo, ungeweza kuwauliza ni taswira ipi au maneno yanayokuja mawazoni wakati wakisikia neno tumia. (Ungeweza hata kuangalia maneno kwenye kamusi.) Ni matokeo gani mazoezi ya viungo yanayo katika miili yetu? Je, tunawezaje kutumia kanuni hii kwenye imani? Ni katika njia zipi tunaweza “kutumia imani” katika Kristo? Washirikiwa darasa wangeweza kuchunguza Etheri 12:2–22 na kujadili jinsi watu waliosemwa katika mistari hii walitumia imani. Je, tunawezaje kufuata mifano yao? Kulingana na mistari hii, kutumia imani katika Yesu Kristo kuna matokeo gani?
-
Mifano hiyo ya imani katika Etheri 12:7–22 inatoa marejeleo mazuri ya hadithi zenye msukumo wa kiungu ambazo mmeshajifunza kwa pamoja katika Kitabu cha Mormoni. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano mingine ya imani na nini wanajifunza kutokana nayo (mingine inaweza kupatikana katika Waebrania 11). Wangeweza pia kushiriki mifano ya imani toka historia zao za familia au maisha yao wenyewe. Je, ni kwa namna ipi mifano hii iliimarisha imani yao katika Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni?
-
Etheri 12 imejaa umaizi na kweli kuhusu imani. Washiriki wa darasa wangeweza kupata mistari katika sura hii ambayo inawafundisha kuhusu imani. Kisha wangeweza kuandika ubaoni kile walichogundua.
Imani hupelekea “Tumaini kwa ajili ya ulimwengu bora zaidi.”
-
Je, kuna yoyote katika darasa lako anaweza kuelezea kwa nini nanga ni muhimu katika boti? Ungeweza kuonyesha picha ya boti na nanga (au chora picha ubaoni) na jadili nini hutokea kwenye boti ambayo haina nanga. Je, hutokea kwetu wakati hatuna tumaini? Kisha washirikiwa darasa wangeweza kusoma Etheri 12:4 na kuzungumzia kuhusu jinsi tumaini ni kama “nanga kwa nafsi [zetu]” Pia wangeweza kusoma Etheri 12:1–9, 28 na 32 na kushiriki umaizi wanaoupata kuhusu tumaini. Je, ni nini tunatakiwa kutumainia? (Ona Etheri 12:4; Moroni 7:41; ona pia Yohana 16:33).
Kupitia neema ya Yesu Kristo, vitu dhaifu vinaweza kuwa imara.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia binafsi kweli ambazo Moroni alijifunza kuhusu udhaifu na nguvu katika Etheri 12, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kumfikiria mtu fulani ambaye anaweza kuwa anahisi kuvunjika moyo kwa sababu ya udhaifu wao. Kisha wahamasishe washiriki wa darasa kuchunguza Etheri 12:23–29 ili kupata jumbe ambazo zingeweza kumsaidia mtu huyo. Kama Moroni angekuwepo leo hii, Je, nini angesema kumtia moyo mtu huyo? Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki uzoefu kutoka katika maisha yao wenyewe ambapo Mwokozi amesaidia “vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu kwao” (Etheri 12:27). Je, badiliko hili ni la tofauti kwa namna gani na juhudi binafsi za kuwa bora ambazo mtu angeweza kufanya bila kumtegemea Mwokozi? Kwa mengi zaidi juu ya mada hii, ona maelezo ya Rais Henry B. Eyring katika “Nyenzo za Zaida”
-
Uzoefu wa Moroni ni kati ya matukio mengi katika maandiko ambayo huonyesha jinsi neema ya Mwokozi inavyoweza kugeuza madahaifu yetu kuwa nguvu. Inaweza kusaidia kama utaligawanya darasa katika makundi na lipe kazi kila kundi kumchagua mtu fulani toka katika maandiko ambaye alikuwa na udhaifu, na jadili jinsi Bwana alivyomfanya mtu huyo kuwa mwenye nguvu. Baadhi ya mifano inapendekezwa katika “Nyenzo za ziada.” Pia ungeweza kupendekeza kwamba washirikiwa darasa warejelee maana ya neema katika Kamusi ya Biblia au Kweli katika Imani (ukurasa wa 77–78). Je, ni kwa namna gani mifano ya kimaandiko waliyojifunza inaelezea nguvu ya neema ya Mwokozi? Je, tunaalikaje nguvu hii katika maisha yetu?
-
Ni kawaida kulinganisha madhaifu yetu na nguvu ya wengine inayodhaniwa, hata Moroni alihisi kutokuwa sawa kwa kulinganishwa na kaka wa Yaredi (ona Etheri 12:24). Je, kwa nini ni hatari kwetu kujilinganisha na wengine? Kulingana na Etheri 12:26–27, Je, ni kwa namna gani Bwana anatutaka kuona madahaifu yetu? (ona pia maelezo ya Rais Henry B. Eyring katika “Nyenzo za Ziada”). Je, ni kwa namna ipi anataka tuyachukulie madhaifu ya wengine? (ona Etheri 12:26).
Kuwakataa manabii huleta hatari ya kiroho.
-
Kwa kupewa ukweli muhimu uliofundishwa katika Etheri 12, ungeweza kuchagua kutotumia muda sana darasani kwenye sura ya 13–15. Hata hivyo, inaweza kusaidia kwa kuwauliza maswali washiriki wa darasa kwa ufupi kutoa muhtasari wa kinachotokea katika sura hizi. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata ujumbe wenye maana katika tukio hili, ungeweza kuwaomba kumalizia virai kama vile “hivyo tunaona …” kwa somo ambalo wanajifunza kutoka katika anguko la Wayaredi. Je, ni kwa jinsi gani anguko lao ni sawa na la Wanefi? (ona, kwa mfano, Etheri 15:19 na Moroni 8:28). Je, Bwana anatutaka tujifunze nini kutoka katika matukio haya, na tunaweza kufanya nini ili kuepuka hatma kama la Wayaredi Washiriki wa darasa wangeweza kurejelea jinsi mwisho wa kitabu cha Etheri unavyounganishwa na Omni 1:19–22; Mosia 8:8; na Mosia 28:11–18.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wiki ijayo washirikiwa darasa wataanza kujifunza kutoka kitabu cha Moroni. Wanaweza kukuta kwamba inavutia kujua kwamba Moroni hakuwa mwanzoni amepanga kuandika chochote zaidi baada ya kitabu cha Etheri, lakini alibakia akiishi kwa muda mrefu kuliko alivyotegemea. Wiki hii wataanza kusoma jumbe za mwisho ambazo Moroni alipata msukumo wa kiungu kuandika kabla hajafa.
Nyenzo za Ziada
Uendelevu wa kiroho huitaji kuona madhaifu yetu.
Rais Henry B. Eyring, akitoa maoni juu ya Etheri 12:27, alifundisha “Moroni alisema kwamba wakati ‘aliposikia maneno haya,’ ali ‘farijika’ (Etheri 12:29). Yanaweza kuwa faraja kwetu pia. Wale ambao hawaoni madahaifu yao hawaendelei. Utambuzi wako wa madhaifu yako ni baraka kwa kuwa inakusaidia kubakia mnyenyekevu na kukufanya kumgeukia Mwokozi. Roho si tu anakufariji, lakini Yeye pia ni wakala ambapo Upatanisho hufanya kazi kuleta kubadilishwa kwa asili yako. Kisha vitu dhaifu huwa vyenye nguvu” (“Amani Yangu Nawaachieni Ninyi,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 16).
Mifano: Vitu dhaifu vikifanywa vyenye nguvu
-
Enoki (Musa 6:31–34; 7:13)
-
Musa (Kutoka 4:10–12; 14:31)
-
Gidioni (Waamuzi 6:12–16; 8:22–23)
-
Petro (Luka 5:8–10; 22:55–62; Matendo ya Mitume 4:13–21)
-
Moroni (Etheri 12:23–29)
-
Joseph Smith (Joseph Smith—Historia 1:28; DC 35:17; 135:3)