Njoo, Unifuate
Novemba 9–15. Etheri 1–5: “Pasua lile Pazia la Kutoamini”


“Novemba 9–15. Etheri 1–5: ‘Pasua Lile Pazia la Kutoamini,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 9–15. Etheri 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Wayaredi wakisafiri kupitia nyikani

Wayaredi Wakiondoka Babeli, na Albin Veselka

Novemba 9–15

Etheri 1–5

“Pasua Lile Pazia la Kutoamini”

Ni kweli zipi ulijifunza wakati wa usomaji wako binafsi wa Etheri 1–5 ambazo unaweza kushiriki na wale unaowafundisha? Ni fursa zipi unaweza kuwapa ili kushiriki kile walichojifunza?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria njia hii ya ubunifu kualika kushiriki: toa mawe 16 kwa washiriki wa darasa, na waalike baadhi yao kushiriki ukweli wanaokumbuka kutoka kwenye kujifunza kwao binafsi au kifamilia juu ya Etheri 1–5. Je, ni nini wanakwenda kukifanya kwa sababu ya kile walichojifunza?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Etheri 1–3; 4:8–19

Tunapomwita Bwana daima, atafunua mapenzi Yake.

  • Kila mmoja wetu amehangaika kutafuta jibu kwa tatizo au swali. Ni kwa jinsi gani uzoefu wa kaka wa Yaredi unawasaidia wale unaowafundisha kujifunza jinsi ya kutafuta usaidizi kutoka kwa Bwana? Pengine ungeweza kuchora jedwali ubaoni likiwa na safu zilizoandikwa Swali la kaka wa Yaredi, Tendo la kaka wa Yaredi, na Jibu la Bwana. Kisha ungeweza kuligawa darasa katika makundi matatu na kuwapangia safu moja kila kundi. Kila kundi lingeweza kufanya kazi pamoja kupekua Etheri 1:33–43 na 2:16–3:6 na kuandika kile wanachopata kwenye safu zao walizopangiwa. Baada ya hapo darasa lingeweza kujadili maswali kama haya: Ni nini tunajifunza kuhusu njia mbalimbali ambazo Bwana anaweza kuchagua kutusaidia? Ni nini tunajifunza kuhusu jukumu letu katika mchakato wa kupokea ufunuo? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano mingine kutoka kwenye maandiko ambayo hufundisha kanuni sawa na hizo. Maelezo kutoka kwa Mzee Richard G. Scott katika “Nyenzo za Zaida” hutoa umaizi zaidi kuhusu jinsi Bwana anavyojibu sala.

  • Sala ya kaka wa Yaredi katika Etheri 3:1–5 ingeweza kuwapa msukumo washiriki wa darasa kufanya tathmini ya sala zao binafsi. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kujifikiria kwamba walikua wakitoa ushauri kwa mtu ambaye anajifunza jinsi ya kusali. Ni ushauri upi wangeweza kutoa? Kisha wangeweza kupekua Etheri 3:1–5 na kufanyia ufupisho kila mstari kwa kidokezo kimoja au viwili au kanuni kuhusu jinsi ya kusali kwa usahihi. Fikiria kuwapa washiriki wa darasa dakika chache kufikiria juu ya sala zao wenyewe na jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa kaka wa Yaredi kufanya sala zao ziwe za maana zaidi.

  • Baada ya kushiriki uzoefu wa ufunuo wa kaka wa Yaredi katika Etheri 3, Moroni alitoa ushauri katika Etheri 4 kuhusu jinsi tunavyoweza kupokea ufunuo kutoka kwa Bwana. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwenye ushauri huu, ungeweza kuonesha picha ya Yesu Kristo na kuwaalika washiriki wa darasa kupekua Etheri 4:8–10 kupata mambo yanayoweza kutuzuia kupokea ufunuo au ukweli kutoka kwa Bwana. Wakati washiriki wa darasa wakishiriki kile walichopata, ungeweza taratibu kufunika picha ya Kristo kwa nguo au kipande cha karatasi. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuepuka vikwazo vya kiroho katika maisha yetu? Kisha, washiriki wa darasa wangeweza kupekua Etheri 4:7, 11–15, wakitafuta jinsi tunavyoweza kuwa na sifa za kupokea ukweli kutoka kwa Bwana. Wakati washiriki wa darasa wanashiriki kile walichopata, ondoa nguo au kipande cha karatasi. Inamaanisha nini “kuonesha imani katika … Bwana, kama kaka wa Yaredi alivyofanya”? (Etheri 4:7; ona pia Etheri 3:1–9). Inamaanisha nini “kupasua pazia la kutoamini” katika maisha yetu? (Etheri 4:15). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kufanya vivyo hivyo? Washiriki wa darasa wangeweza pia kutafuta kweli kuhusu ufunuo binafsi katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu” (Ensign au Liahona, Mei 2018, 93–96).

Etheri 2:14–15

Kupitia maonyo Yake, Bwana anatualika kutubu na kuja Kwake.

  • Hata nabii mkuu kama kaka wa Yaredi alipokea maonyo kutoka kwa Bwana. Kwa kweli, sehemu ya kile kilichomfanya mkuu ilikuwa ni jinsi alivyoitikia maonyo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwenye mfano wa kaka wa Yaredi, ungeweza kuwaalika kusoma Etheri 2:14–15 pamoja katika jozi. Kisha waombe kujifanya kwamba mmoja wao ni kaka wa Yaredi na mwingine ni mtu ambaye ametoka kupokea maonyo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa au mzazi. Waache wajadili au kuigiza kile kaka wa Yaredi angeweza kusema kuhusu uzoefu wake mwenyewe ili kumsaidia mtu huyu. Ni ushauri upi angeweza kutoa? Ni funzo gani tunapata ambalo litatusaidia kusogea karibu na Baba wa Mbinguni? Ungeweza pia kujadili jinsi maonyo ya Bwana na mwitikio wa kaka wa Yaredi vilivyosaidia kumuandaa kwa uzoefu alioupata katika Etheri 3:1–20. Hapa ni baadhi ya nyenzo ambazo zinaweza kusaidia: Ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kadiri ya Wengi Niwapendao, Huwaonya na Kuwarudi” (Ensign au Liahona, Mei 2011, 97–100) au sehemu yenye kichwa cha habari “Uadilifu” katika ujumbe wa Mzee Lynn G. Robbins “Mwamuzi wa Haki” (Ensign au Liahona, Nov. 2016, 96–97).

Etheri 5

Mashahidi watatu hushuhudia juu ya ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

  • Kujifunza zaidi kuhusu unabii wa Moroni wa Mashahidi Watatu kungeweza kuimarisha ushuhuda wa washiriki wa darasa juu ya Kitabu cha Mormoni. Pengine nusu ya darasa wangeweza kusoma Etheri 5 na nusu nyingine wangeweza kusoma “Ushahidi wa Mashahidi Watatu” (mwanzoni mwa Kitabu cha Mormoni) na kushiriki na kila mmoja kile wanachohisi lilikuwa lengo la Bwana katika kuwaruhusu Mashahidi Watatu kumuona malaika na bamba. Wangeweza pia kujadili hali zingine ambapo mashahidi wengi walifanya ukweli usimame (ona, kwa mfano, Mathayo 3:13–17; 18:15–16; Yohana 5:31–47; Mafundisho na Maagano 128:3). Ni mashahidi gani katika maisha yetu wametupa ushawishi wa kuamini? Ni kwa jinsi gani “nguvu ya Mungu na pia neno lake” “vimedhihirishwa” kwetu katika Kitabu cha Mormoni? (Etheri 5:4).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike washiriki wa darasa kufikiria kwamba viongozi wao wa siasa walikuwa daima wakitekana na kuuana. Katika Etheri 6–11, watasoma kuhusu jinsi hili lilivyotokea kwa uzao wa Yaredi na kaka yake. Watapata pia baadhi ya maonyo ambayo yatawasaidia kuepuka matatizo yaliyowakabili Wayaredi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kutambua majibu ya maswali.

Mzee Richard G. Scott alifundisha:

“Wakati tunapoelezea tatizo na suluhisho lililopendekezwa, wakati mwingine Yeye hujibu ndiyo, wakati mwingine hapana. Mara nyingi Yeye hatoi jibu kwa wakati wetu, si kwa kukosa kujali, lakini kwa sababu Yeye anatupenda—kikamilifu. Anataka tutumie kweli zile ambazo Yeye ametupatia. Ili tukue, tunahitaji kuamini uwezo wetu wa kufanya maamuzi sahihi. Tunahitaji kufanya kile ambacho tunahisi ni sahihi. Kadiri ya muda, Yeye atajibu. Yeye hatatuangusha. …

“… Yeye anatutaka sisi tutende ili tupate uzoefu unaohitajika:

“Yeye anapojibu ndiyo, ni kutufanya sisi tujiamini.

“Yeye anapojibu hapana, ni kuzuia kosa.

“Wakati Yeye hatoi jibu kwa wakati wetu, ni kutuwezesha sisi kukua kupitia imani katika Yeye, utiifu wa amri Zake, na hiari ya kutenda kwenye ukweli. Tunatarajiwa kuchukua uwajibikaji kwa kutenda juu ya maamuzi ambayo yanaambatana na mafundisho yake bila ya uthibitisho wa mapema. Sisi hatupaswi kukaa kitako tukingojea au kunung’unika kwa sababu Bwana hajazungumza. Tunapaswa kutenda” (“Kujifunza Kutambua Majibu ya Sala,” Ensign, Nov. 1989, 31–32).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Nenda kwenye Maandiko kwanza. Maandiko lazima yawe chanzo cha msingi cha maandalizi na kujifunza kwako. Usisahau kwamba maneno ya manabii wa sasa yanajaliza kwenye maandiko na ni maandiko pia (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17–18).

Chapisha