Njoo, Unifuate
Novemba 16–22. Etheri 6–11: “Kwamba Uovu Huu Uweze Kuondolewa”


“Novemba 16–22. Etheri 6–11: ‘Kwamba Uovu Huu Uweze Kuondolewa’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 16–22. Etheri 6–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Mashua za Wayaredi baharini

Nitawarudisha juu Tena kutoka kwenye Kilindi cha Bahari, na Jonathan Arthur Clarke

Novemba 16–22

Etheri 6–11

“Kwamba Uovu huu Uweze Kuondolewa”

Kumbuka kwamba kumbukumbu zilizopo katika Kitabu cha Mormoni ziliandikwa kwa ajili ya siku zetu. Wakati ukijiandaa kufundisha, pitia matukio haya kwenye maandiko kwa ajili ya kanuni ambazo zinaweza kuwaimarisha washiriki wa darasa kukabiliana na changamoto katika maisha yao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kitu fulani walichokipata katika Etheri 6–11, ungewaalika kuvuta taswira kwamba sura hizi zilikuwa zikitengenezewa filamu; Je, ni kirai gani toka Etheri 6–11 wangekipendekeza kama kichwa cha habari? Wape muda kutafakari kuhusu hili, na waalike kushiriki vichwa vyao vya habari na kufafanua kwa nini walivichagua.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Etheri 6:1–12

Bwana atatuongoza kupitia safari ya maisha yetu hapa duniani.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kulinganisha safari ya Wayaredi kuvuka bahari na safari ya maisha yetu hapa duniani. Waombe washiriki wa darasa ambao walifanya shughuli hii nyumbani kushiriki umaizi wao walioupata kutoka katika mfano huu. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kulinganisha zaidi, waalike kuangalia katika Etheri 6:1–12 kwa ajili ya maelezo kuhusu safari ambayo ingeweza kuwa na alama zenye maana (kama vile mawe yang’aayo, mashua, na upepo) na waviorodheshe ubaoni. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kutumia dakika kadhaa wakifanya kazi katika jozi au makundi madogo madogo kujifunza mistari na kujadiliana ni nini alama hizi zinaweza kuwa zinawakilisha. Kwa mfano, “Nchi yetu ya ahadi ni nini”? (mstari 8). Je,, Mungu hutuongoza vipi katika safari yetu?

  • Ungeweza kutumia Etheri 6:1–12 kuhamasisha majadiliano kuhusu jinsi gani kumgeukia Mungu hutusaidia kukua kupitia changamoto zetu. Kwa mfano, nukuu katika ‘Nyenzo za Ziada” inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kulinganisha “upepo mkali” uliosemwa katika mstari wa 5–8 na majaribu katika maisha. Je, ni kipi Wayaredi walifanya wakati “walipokuwa wamezungukwa na maji mengi”? (mstari wa 7). Washiriki wa draasa wangeweza kushiriki uzoefu ambapo majaribu yaliwasaidia kusonga mbele. Ni kwa namna gani mwitikio katika majaribu yao uliwasaidia kusonga mbele katika “nchi ya ahadi”? Je, ni kwa namna gani Bwana aliwasaidia katika majaribu yao? Wahamasishe kurejelea maneno na virai kutoka Etheri 6 wakati wakishiriki uzoefu na mawazo yao.

    Picha
    Wayaredi wakisafiri pamoja na wanyama

    Safari ya Wayaredi kupitia Asia, na Minerva Teichert

Etheri 6:7–18, 30; 9:28–35; 10:1–2

Bwana hutubariki tunapokuwa wanyenyekevu.

  • Ingawa sehemu kubwa ya hadithi ya Wayaredi inaelezea matokeo hasi ya kujivuna na uovu, pia inajumuisha nyakati za unyenyekevu na utajiri ambazo tunaweza kujifunza kutokana na zo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutokana na mifano hii chanya, ungeweza kuligawa darasa katika makundi mawili na kulipa kundi moja kusoma Etheri 6:7–18 na 30 wakati kundi lingine likisoma Etheri 9:28–35 na 10:1–2. Waombe kutafuta katika mistari hii vithibitisho kwamba Wayaredi walikuwa wamejinyenyekeza wao wenyewe—au walinyenyekezwa na hali zao—na jinsi Bwana alivyowabariki kama matokeo. Wakati washiriki wa darasa wangekuwa na muda wa kutosha, waalike kutoka katika kila kikundi kushiriki kile walichojifunza. Je, ni kwa jinsi gani kuwa mnyenyekevu hutusaidia kumkaribia Mungu? Kuimba au kusikiliza nyimbo za kanisa kuhusu unyenyekevu, kama vile “Nina Kuhitaji Kila Saa” (Nyimbo za Kanisa, namba 98), kungeweza kuongezea katika shughuli hii.

Etheri 7–11

Viongozi watakatifu huwaongoza watu kwa Mungu.

  • Hata kwa wale ambao hawakuwahi kuwa katika nafasi rasmi za uongozi wanaweza kujifunza kutoka katika mifano ya wafalme Wayaredi wenye haki na waovu; matukio haya yanaweza kutusaidia kuwa bora zaidi nyumbani kwetu, katika jamii zetu, na kanisani. Labda ungeanza majadiliano katika mada hii kwa kuwauliza washiriki wa darasa kufikiria kuhusu mtu fulani ambaye wanamchukulia kama kiongozi mzuri. Waalike kushiriki kwa ufupi baadhi ya sifa za mtu huyo, na waorodheshe ubaoni. Kisha ungeweza kuwapa kazi kila mshiriki wa darasa kujifunza kuhusu mmoja wa wafalme wa Wayaredi katika Etheri 7–11. (Orodha ya wafalme pamoja na marejeleo ya kimaandiko ambayo yanaelezea utawala wao, inapatikana katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.) Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki walichojifunza kutoka kwa wafalme hawa kuhusu uongozi, wakiongezea sifa zingine ambazo wamepata katika orodha ubaoni. Sifa chanya zingine za uongozi zimeorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.” Je, tunawezaje kupata sifa hizi na kuwa viongozi, hata kama hatuna jukumu maalum la kiuongozi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kutia hamasa matamnio ya washiriki wa darasa katika kusoma Etheri 12–15, ungeweza kusema kwamba katika sura hizi Moroni anamuelezea uwoga wake kuhusu kumbukumbu ambazo alikuwa anaweka. Jibu la Bwana linaweza kutusaidia wakati tuna hisia sawa za kuhisi kutoweza.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Majaribu tuliyonayo yanatuandaa kupokea uzima wa milele.

Akiongea katika mkutano mkuu wakati wa kipindi kigumu cha vita ya II ya dunia, Mzee Charles A. Callis wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema: “Tunaambiwa kwamba wakati wayaredi katika mashua walipoanza safari kuja nchi hii ya ahadi, tufani kali na ya kuogofya ilitawala. Upepo ulivuma na walikuwa katika hatari kubwa wakati wote katika safari hii yenye hatari. Mungu aliwasaidia. Na tunasoma kwamba ingawa pepo hizi kali na tufani vilivuma, vikibeba uharibifu, kwamba upepo daima ulivuma kuelekea Nchi ya Ahadi. Na majaribu haya ambayo tunayapitia, vita hivi vya kutisha na vitu vyote vya kuogofya ambavyo vinatawala, viko katika nguvu za Mungu. Anaweza kuvisimamisha wakati akiamua, wakati madhumuni yake matakatifu yakishatimizwa. Lakini acha tusisahau kwamba kupitia bahari hii ya matatizo, majaribu yetu, uzoefu ambao tunaupitia na ambao Mungu atafanya ufanye kazi kwa manufaa yetu, kama tutamtii Yeye—yote haya yanatupeperusha mbele kwenda mbinguni kupumzika, katika wakati mtakatifu ujao, katika uzima wa milele” (Repoti ya Mkutano, Apr. 1943, 62).

Sifa za kiongozi mwenye haki.

“Katika ufalme wa Mungu, ukuu na uongozi humaanisha kwamba kuwaona wengine kiuhalisia walivyo—kama Mungu awaonavyo—na kisha kuwafikia na kuwahudumia. Humaanisha kufurahia pamoja na wale wenye furaha, na kuomboleza na wale waombolezao, kuwainua wenye kukata tamaa, na kuwapenda majirani zetu kama Kristo atupendavyo. …

“… Uongozi katika Kanisa la Kristo si zaidi katika kuongoza wengine kama ilivyo kuhusu utayari wetu kuongozwa na Mungu” (Dieter F. Uchtdorf, “Aliye Mkuu kati Yenu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 79–80).

“Ni wale tu wenye maadili ambao wana uwezo wa kuinuana na kutiana moyo katika huduma kuu, katika mafanikio makuu, katika nguvu kuu” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson [2014], 244).

“Ulimwengu hufundisha kwamba viongozi lazima wawe wenye nguvu; Bwana Hufundisha kwamba lazima wawe wanyenyekevu. Viongozi wa dunia hupata nguvu na ushawishi kupitia vipaji vyao, ujuzi na mali. Viongozi kwa mfano wa Kristo hupata nguvu na ushawishi ‘kwa kushawishi, kwa uvumilivu, kwa upole na unyenyekevu, na kwa upendo usiokoma’ [Mafundisho na Maagano 121:41]” (Stephen W. Owen, “Viongozi Wakuu ni Wafuasi Wakuu,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 75).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza mazingira yenye heshima. Je, unahisi kwamba kila mmoja katika darasa yuko sawa kuelezea mawazo yao na hisia? “Wasaidie washiriki wa darasa lako kuelewa kwamba kila mmoja wao anaathiri roho ya darasa. Wahimize wakusaidie kujenga mazingira yaliyo wazi, ya upendo, na heshima ili kwamba kila mtu ajisikie yuko salama kushiriki uzoefu, maswali, na ushuhuda wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,15).

Chapisha