Njoo, Unifuate
Novemba 30–Desemba 6 Moroni 1–6: “Kuwaweka katika Njia Sahihi”


Novemba 30–Desemba 6. moroni 1–6: ‘Kuwaweka katika Njia Sahihi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Novemba 30–Desemba 6. Moroni 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Alma akibatiza watu katika Maji ya Mormoni

Minerva Teichert (1888–1976), Alma Akibatiza katika Maji ya Mormoni, 1949–1951, mchoro wa mafuta kwenye ubao, inchi 35⅞ x 48. Jumba la Makumbusho la sanaa la Chuo kikuu cha Brigham Young, 1969

Novemba 30–Desemba 6

Moroni 1–6

“Kuwaweka katika Njia Sahihi”

Moroni alitamani kwamba mambo aliyoandika yangekuwa “yenye thamani” kwa wale wanaoishi katika siku za mwisho (Moroni 1:4). Unaposoma Moroni 1–6, kwa sala fikiria mambo ambayo yatakuwa yenye thamani kubwa wale unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati mwingine washiriki wa darasa wanaweza kushiriki umaizi vizuri kutoka kwenye kujifunza kwao binafsi wakati wanapokuwa na muda kidogo kukumbuka kile walichosoma. Ungeweza kuchukua dakika chache mwanzoni mwa darasa kurejelea vichwa vya habari vya sura vya Moroni 1–6. (Hii ingeweza pia kuwasaidia washiriki wa darasa ambao hawakusoma nyumbani.) Kisha waalike washiriki wa darasa watafute sura kwa ajili ya mstari wanaoona una maana na wangependa kuushiriki na darasa lote.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Moroni 2–6

Ibada za ukuhani lazima zisimamiwe kulingana na Bwana anavyoagiza.

  • Ikiwa washiriki wa darasa lako (au wapendwa wao) wanajiandaa kupokea ibada za ukuhani, ingeweza kuwa yenye thamani kurejea kile Moroni alichofundisha kuhusu ibada katika Moroni 2–6. Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi katika jozi kuigiza mpangilio wa matukio kama ufuatao. (1) Kaka yako punde atatawazwa kwenye ukuhani. Ni ushauri gani ungempa kutoka kwenye Moroni 3? (2) Rafiki wa imani nyingine anajiuliza kwa nini ni muhimu kupokea sakramenti kila wiki. Ni nini ungesema? (ona Moroni 4–5). (3) Ubatizo wa binti yako unakaribia, lakini hana uhakika kama yuko tayari. Ni kwa jinsi gani ungeweza kumsaidia? (ona Moroni 6:1–3). Baada ya kuigiza, darasa lingeweza kujadili kile walichojifunza kutoka kwa kila mmoja. Wangeweza pia kushiriki shuhuda zao kuhusu jinsi ibada kama hizi zilivyowasogeza karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Ili kutambulisha majadiliano kuhusu kujiandaa kwa ajili ya ubatizo, ungeweza kumuomba mshiriki wa darasa kuelezea jinsi walivyojiandaa kwa majukumu muhimu katika maisha yao, kama vile misheni, ndoa, kuwa mzazi, au kazi mpya. Ni kwa jinsi gani maandalizi hayo yanafananishwa na maandalizi ya kustahili kwa ajili ya ubatizo, kama ilivyoelezewa katika Moroni 6:1–3? (ona pia Mosia 18:8–10; Mafundisho na Maagano 20:37). Kwa nini sifa zilizoorodheshwa katika vifungu hivi vya maneno ni muhimu kwa ajili ya ubatizo? Tunajuaje kuwa tumejiandaa kwa ibada hii? Wahimize washiriki wa darasa kutafakari ni vyema kwa kiasi gani wamekuwa wakiishi viwango hivi tangu ubatizo wao na kile ambacho wangefanya kujiboresha. Ungeweza pia kuwaalika kuandika misukumo yoyote wanayopokea na kuirejelea mara kwa mara.

    msichana akipokea baraka

    Ibada hufanywa kwa uwezo wa ukuhani.

Moroni 4–5

Kupokea sakramenti hutusaidia kusogea karibu na Yesu Kristo.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza shughuli za kujifunza zinazohusiana na sakramenti. Pengine ungeweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa kukamilisha shughuli hizi nyumbani na kuja darasani wakiwa wamejiandaa kushiriki kile walichojifunza. Ungeweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki wao kwa wao kile wanachofanya kujiandaa wenyewe na familia zao ili kuwa na uzoefu mtakatifu wa sakramenti.

  • Wengi wetu tumesikia sala za sakramenti mara nyingi, lakini Je, tunafikiria zaidi kuhusu nini maneno humaanisha? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari sala hizi, ungeweza kuwapa dakika kadhaa waandike sala mbili za sakramenti kutoka kwenye kumbukumbu yao. Kisha waalike kulinganisha kile walichoandika na Moroni 4:3 na 5:2. Ni nini walikumbuka kwa urahisi? Ni kipi waliacha? Je, wamegundua chochote kuhusu sala hizi ambacho hawakuwa wamegkiundua hapo awali? Waalike washiriki wa darasa kushiriki maneno na vifungu vya maneno kutoka kwenye sala ya sakramenti ambacho kinajionyesha kwao au ambacho kinawasaidia kuhisi utakatifu wa ibada hii. Ili kuongeza shukrani ya washiriki wa darasa kwa ajili ya sakramenti, fikiria kumwalika mshiriki wa darasa kuimba au kupiga wimbo wa kanisa wa sakramemnti. Ungeweza pia kuonesha video “Always Remember Him” (ChurchofJesusChrist.org).

Moroni 6:4–9

Wafuasi wa Yesu Kristo wanahudumiana.

  • Fikiria kutumia analojia ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa “kulishwa na neno zuri la Mungu” (Moroni 6:4). Kwa mfano, ni aina ipi ya kirutubisho kinahitajika kwa ajili ya mche au mtoto? Nini kitatokea ikiwa utaacha kitu kinachohitaji kurutubishwa? Ni kwa jinsi gani waumini wapya na wanaorudi ni sawa na mmea au mtoto mchanga katika hitaji la kurutubishwa? Washiriki wa darasa wangeweza kupekua Moroni 6:4–9 kwa ajili ya mawazo kuhusu jinsi wanavyoweza “kurutubishana” kiroho. Wangeweza pia kupata mawazo katika “Nyenzo za Ziada.” Ungeweza kushiriki uzoefu ambapo mfuasi mwenza alikuhudumia. Pengine washiriki wa darasa wangekuwa tayari kushiriki uzoefu sawa na huo.

  • Moroni 6:4–9 ingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi tunavyobarikiwa wakati “tunapohesabiwa kama watu wa kanisa la Kristo” na kuhudhuria mikutano ya kanisa. Ni kwa jinsi gani tungeweza kuelezea mambo haya kwa mtu anayetilia shaka uhitaji wa kanisa lenye mpangilio? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kutafuta mistari hii kupata jambo ambalo wangeweza kushiriki. Au wangeweza kuorodhesha baadhi ya baraka walizopokea kama waumini wa Kanisa (ona D. Todd Christofferson, “Kwa nini Kanisa,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 108–11). Nini tunaweza kufanya kuhakikisha kwamba wafuasi wenzetu “wanakumbukwa na kulishwa na neno zuri la Mungu” pale “tunapokutana pamoja mara kwa mara”? (Moroni 6:4–5).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Washiriki wa darasa wanaweza kuwa na shauku ya kusoma Moroni 7–9 wiki ijayo ikiwa utaelezea kwamba inajumuisha barua mbili zilizoandikwa na Mormoni kumsaidia mwana wake kubakia mwaminifu katika nyakati ngumu.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kulishwa na neno zuri la Mungu.

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha: “Watu wengi hawaji Kanisani kutafuta tu kweli chache za injili ama kuwaona marafiki wa zamani, ingawa hayo yote ni muhimu. Wanakuja wakitafuta uzoefu wa kiroho. Wanataka amani. Wanataka imani yao iimarishwe na tumaini lao kufanywa upya. Wanataka, kwa ufupi, kulishwa na neno zuri la Mungu, kuimarishwa na nguvu za mbinguni” (“Mwalimu Anatoka kwa Mungu,” Ensign, Mei 1998, 26).

Rais Gordon B. Hinckley alieleza kuwa kuwalisha waongofu kwa neno zuri la Mungu “ni kazi ya kila mmoja. Ni kazi ya walimu wa nyumbani na walimu watembelezi [sasa ni akina kaka na akina dada wahudumiaji]. Ni kazi ya uaskofu, ya akidi za ukuhani, ya Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, wavulana na wasichana, hata darasa la Msingi.

“Nilikuwa katika mkutano wa kufunga na ushuhuda Jumapili iliyopita. Mvulana mwenye miaka 15 ama 16 alisimama mbele ya mkusanyiko na kusema kuwa alikuwa ameamua kubatizwa.

“Kisha mmoja baada ya mwingine, wavulana wa akidi ya walimu walisimama mbele ya kipaza sauti ili kuonyesha upendo wao kwake, kumwambia kuwa alikuwa anafanya jambo lililo sahihi, na kumhakikishia kuwa wangesimama naye na kumsaidia. Ilikuwa ni tukio la ajabu kuwasikia wavulana hao wakizungumza maneno ya shukrani na ya kuhimiza kwa rafiki yao. Nimeridhika kwamba wote kati ya wavulana wale, ikiwa ni pamoja na aliyebatizwa wiki iliyopita, watakwenda misheni.

“Katika mahojiano ya habari hivi karibuni niliulizwa, ‘nini kinakupa kuridhika kwa kiasi kikubwa pale unapoona kazi ya Kanisa leo?’

“Jibu langu: ‘Uzoefu wa kuridhisha wa kiasi kikubwa zaidi nilionao ni kuona kile injili hii inachofanya kwa ajili ya watu. Inawapa mtazamo mpya juu ya maisha. Inawapa mtazamo ambao hawakuwahi kuuhisi kabla. Inainua uoni wao kwenye mambo ya kawaida na matakatifu. Jambo fulani hutokea kwao ambalo ni la kimuujiza kutazama. Wanamtazama Kristo na kuja wakiwa hai.’

“… Ninamuomba kila mmoja wenu kusaidia katika shughuli hii” (“Waongofu na Wavulana,” Ensign, Mei 1997, 48).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo wako mwenyewe. Badala ya kuichukulia mihutasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima uyafuate, itumie kama chanzo cha mawazo kuanzisha mwongozo wako wa kiungu unapotafakari mahitaji ya wale unaowafundisha.