Njoo, Unifuate
Desemba 21–27. Krismasi: “Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake”


Desemba 21–27. Krismasi: ‘Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Desemba 21–27. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Yusufu, Mariamu, na mtoto Yesu ndani ya zizi

Tazama Mwanakondoo wa Mungu, na Walter Rane

Desemba 21–27

Krismasi

“Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake”

Unaposoma kuzaliwa kwa Yesu Kristo wiki hii, fikiria jinsi unavyoweza kusaidia darasa lako kuimarisha shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Baadhi ya mawazo katika muhtasari huu yanaweza kusaidia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kutengeneza jozi au makundi madogo madogo na kushiriki jinsi kujifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni mwaka huu kumeimarisha imani yao Kwake na kwenye mafundisho Yake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Nefi 11:13–23; Helamani 14:1–13; 3 Nefi 1:4–22

Yesu Kristo alizaliwa kuwa Mwokozi wetu.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Kitabu cha Mormoni kuwafundisha washiriki wa darasa kuhusu tukio takatifu la kuzaliwa kwa Mwokozi? Njia moja ni kuligawa darasa katika makundi matatu na kulipa kila kundi moja ya vifungu vya maandiko vifuatavyo ili kusoma: 1 Nefi 11:13–23; Helamani 14:1–13; na 3 Nefi 1:4–22. Yaombe makundi kujadili kile maandiko haya yanachowafundisha kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi. Kisha kila kundi lingeweza kushiriki na darasa kile walichojadili. Kwa nini ni ya thamani kuwa na ushahidi wa Kitabu cha Mormoni juu ya kuzaliwa kwa Mwokozi?

  • Kujua kuhusu kuzaliwa kwa Kristo ni muhimu, lakini kujua kwa nini Yeye alizaliwa ni muhimu zaidi. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kutafakari nguvu ya ukombozi ya Yesu Kristo? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki baadhi ya hadithi na vifungu vya maneno walivyojifunza wiki hii (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Wahimize kushiriki jinsi mambo waliyojifunza yalivyoongeza shukrani yao kwa kuzaliwa kwa Mwokozi na kwa nguvu yake ya kukomboa.

  • Kuanza majadiliano kuhusu zawadi ambazo Mungu ametupatia kupitia Mwanawe, ungeweza kuwaalika wanadarasa wachache kuzungumzia zawadi maalumu walizopokea wakati wa Krismasi. Ni kwa jinsi gani tunaonyesha shukrani kwa zawadi tulizopokea? Washiriki wa darasa kisha wangeweza kusoma nukuu ya Rais Thomas S. Monson inayopatikana katika “Nyenzo za Zaida” na kujadili zawadi nne ambazo Rais Monson aliorodhesha. Ni jukumu gani Mwokozi anabeba katika zawadi hizi? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa zawadi hizi?

  • Kama sehemu ya majadiliano yenu kuhusu Krismasi, fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kupiga au kuimba nyimbo za Krismasi. Mngeweza pia kupitia kwa kina baadhi ya nyenzo zilizoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.”

Ukurasa wa jina wa Kitabu cha Mormoni; dibaji ya Kitabu cha Mormoni; 2 Nefi 25:23, 26; 33:4, 10

Kitabu cha Mormoni kinashuhudia juu ya Yesu Kristo.

  • Pale kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni katika Shule ya Jumapili kunapokaribia kumalizika, ungeweza kutaka kuwapa washiriki wa darasa fursa ya kufikiria juu ya kile walichojifunza kuhusu Yesu Kristo katika Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Ili kusaidia kuanzisha mjadala, mngeweza kusoma pamoja 2 Nefi 25:23, 26 na 33:4, 10, vile vile dondoo kutoka dibaji ya Kitabu cha Mormoni na ukurasa wa jina. Ungeweza pia kushiriki hadithi au kifungu cha maneno ambacho kimekuleta karibu na Yesu Kristo na kisha wape washiriki wa darasa dakika chache kushiriki hadithi zao wenyewe au vifungu vya maneno. Shiriki ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni, na waalike washiriki wengine wa darasa kufanya vivyo hivyo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwapa msukumo washiriki wa darasa kuanza kusoma Mafundisho na Maagano, ungeweza kushiriki mstari unaoupenda au uzoefu wa kuvutia ulionao wa kujifunza Mafundisho na Maagano.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Nyenzo za Krismasi.

  • Mathayo 1:18–252; Luka 2

  • Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 28, 29, 30, 3181

  • Picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia.

  • “A Savior Is Born—Video ya Krismasi” (video, ChurchofJesusChrist.org)

  • “Good Tidings of Great Joy: The Birth of Jesus Christ” (video, ChurchofJesusChrist.org)

  • Christmas.ComeUntoChrist.org

  • Ibada za Krismasi za Urais wa Kwanza (ChurchofJesusChrist.org/broadcasts/first-presidency-christmas-devotionals)

Zawadi za Mwokozi.

Rais Thomas S. Monson alifundisha:

“Ninatafakari kwenye utofauti wa Krismasi. Zawadi za thamani ya juu, vifurushi vya ghali na vilivyofungwa kwa ustadi, vikifikia viwango vyake vya juu kwenye orodha ya vitu katika biashara mashuhuri vikibeba kichwa cha habari ‘Kwa ajili ya mtu mwenye kila kitu.’ Katika kusoma kama huko niligundua kadi ya salamu yenye kimo cha futi za mraba elfu nne iliyofungwa nyumbani kwa utepe mkubwa na ya kuweza kulinganishwa ambayo ilisema, ‘Heri ya Krismasi.’ Vitu vingine vilijumuisha rungu za almasi kwa ajili ya wachezaji wa gofu, manowari ya kasi ya Karibean kwa ajili ya wasafiri, na safari ya ghrama kubwa ya kwenda Milima ya Uswiswi kwa ajili ya wapenda safari. Hii ilionesha kufaa dhamira ya katuni ya Krismasi ambayo ilionesha Mamajusi Watatu wakisafiri kwenda Bethlehemu pamoja na masanduku ya zawadi juu ya ngamia wao. Mmoja anasema, ‘Kumbuka maneno yangu, Balthazar, tunaanzisha kitu kwa zawadi hizi ambacho kinakwenda kututoka mkononi!’ …

“Kwa dakika kadhaa, acha tuweke kando orodha ya vitu vya Krismasi, pamoja na zawadi zao za maelezo ya kutoka nchi za nje. Acha hata tugeukie kutoka kwenye maua kwa ajili ya Mama, tai maalumu kwa ajili ya Baba, mwanasesere wa kupendeza, gari moshi inayopiga kelele, baiskeli iliyosubiri kwa muda mrefu … na kuelekeza mawazo yetu kwa zile zawadi-kutoka kwa Mungu ambazo hudumu. Nimechagua kutoka kwenye orodha ndefu nne tu: …

“Kwanza, zawadi ya kuzaliwa. Imetolewa ulimwenguni kwa kila mmoja wetu. Yetu ni fursa takatifu ya kuondoka kwenye nyumba yetu ya mbinguni ili kupata makazi katika mwili na kuonyesha kupitia maisha yetu ustahili wetu na sifa za siku moja kurudi Kwake, wenye thamani wapendwao, na ufalme unaoitwa selestia. … Letu ni jukumu la kuonesha shukrani kupitia matendo ya maisha yetu. …

“Pili, zawadi ya amani. Katika ulimwengu wa kelele tunamoishi, kelele za foleni, sauti za matangazo ya vyombo vya habari, na mahitaji yenye utupu yaliyowekwa katika siku yetu— ukiachilia mbali matatizo ya ulimwengu—huleta maumivu ya kichwa, hushurutisha maumivu, na hudhoofisha nguvu yetu ya kuzoea. …

“Yeye ambaye alibeba majonzi na kuijua huzuni anazungumza na kila moyo wenye mateso na kutoa zawadi ya amani. ‘Amani nawaachieni, amani yangu nawapa: niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga’ (Yohana 14:27). …

“Tatu, zawadi ya upendo. ‘Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?’ aliuliza mwanasheria aliyezungumza na Yesu. Likaja jibu la mara moja: ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

“Na ya pili yafanana nayo, Mpende jirani yako kama nafsi yako” (Mathayo 10:36–39). …

“Nne, zawadi ya uzima—hata kutokufa. Mpango wa Baba yetu wa Mbinguni una kilele cha onyesho la upendo wa kweli. Vyote ambavyo tunavithamini, hata familia zetu, rafiki zetu, furaha yetu, ufahamu wetu, shuhuda zetu, vingepotea kama isingekuwa Baba yetu na Mwana Wake, Bwana Yesu Kristo. Kati ya mawazo na maandiko yanayothaminiwa sana katika ulimwengu huu ni maelezo matakatifu ya ukweli: ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele’ (Yohana 3:16)” (“Zawadi,” Ensign, Mei 1993, 59–62).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ni SAWA kusema, “Sijui.” Wakati unapaswa kufanya kadiri uwezavyo kujibu swali lolote washiriki wa darasa walilonalo kuhusu injili, Bwana hategemei ujue kila kitu. Wakati hujui jinsi ya kujibu jambo, fikiria kujibu kwa kulialika darasa kutafuta pamoja jibu katika maandiko na kushiriki kile wanachopata. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,24.)

Chapisha