Njoo, Unifuate
Desemba 21–27. Krismasi: “Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake”


“Desemba 21–27. Krismasi: ‘Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Desemba 21–27. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Yusufu, Mariamu, na mtoto Yesu ndani ya zizi

Tazama Mwanakondoo wa Mungu, na Walter Rane

Desemba 21–27

Krismasi

“Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake”

Msimu wa Krismasi ni wakati wa kutafakari juu ya na kutoa shukrani kwa kuzaliwa kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Unaposoma na kutafakari wiki hii kuhusu kuzaliwa na maisha Yake, fikiria jinsi kujifunza kwako Kitabu cha Mormoni kumeimarisha ushuhuda wako kwamba Yeye ni Mwokozi wa ulimwengu. Andika misukumo inayokujia.

Andika Misukumo Yako

Kutoka kwa Nefi mpaka kufikia Moroni, kila nabii katika Kitabu cha Mormoni alijitolea kwa kusudi takatifu lililofanyiwa muhtasari katika ukurasa wa jina: wa kitabu hiki: “Kuwathibitishia [watu wote] kwamba Yesu ndiye Kristo.” Nabii mmoja alimuona kama roho kabla ya maisha ya sasa, na mwingine aliona kuzaliwa kwake na huduma yake katika ono. Mmoja alisimama juu ya ukuta kutangaza ishara za kuzaliwa na kifo chake, na mwingine akapiga magoti mbele ya mwili wake uliofufuka, akigusa vidonda kwenye mikono, miguu, na ubavuni Mwake. Wote walijua ukweli huu muhimu: “Hakuna njia nyingine wala jinsi ambayo kwayo binadamu anaweza kuokolewa isipokuwa kupitia kwa upatanisho wa damu ya Yesu Kristo, ambaye … anakuja kuukomboa ulimwengu” (Helamani 5:9).

Kwa hivyo wakati wa msimu huu wa Krismasi, wakati waaminifu kote duniani wanasherehekea wema na upendo wa Mungu kwa kumtuma Mwana Wake, tafakari jinsi ambavyo Kitabu cha Mormoni kimeimarisha imani yako katika Kristo. Unapofikiria kuhusu kuzaliwa Kwake, tafakari ni kwa nini Alikuja na jinsi kuja Kwake kulivyobadili maisha yako. Kisha unaweza kupata uzoefu wa furaha ya kweli ya Krismasi—zawadi ambayo Yesu Kristo anakupatia.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

1 Nefi 11:13–36; Mosia 3:5–10; Helamani 14:1–13; 3 Nefi 1:4–22

Yesu Kristo alikuja duniani kuwa Mwokozi wangu.

Ni desturi kusoma hadithi ya kuzaliwa kwa Mwokozi katika Agano Jipya wakati wa Krismasi, lakini pia waweza kupata unabii wa nguvu wa tukio hili takatifu katika Kitabu cha Mormoni. Kwa mfano, unabii wa kuzaliwa kwa Mwokozi na huduma Yake vinapatikana katika 1 Nefi 11:13–36; Mosia 3:5–10; Helamani 14:1–13; na 3 Nefi 1:4–22. Ni mawazo gani kuhusu Yesu Kristo yanakujia unaposoma vifungu hivi na kutafakari maana zinazo wezekana za ishara za kuzaliwa Kwake? Je, ni kwa namna gani ushuhuda wa manabii wa Amerika ya kale umeimarisha ushuhuda wako juu ya Kristo na Misheni Yake?

Ona Pia Mathayo 1:18–252; Luka 2.

2 Nefi 2:6; Alma 7:7–13; 11:40; Helamani 5:9; 14:16–17

Yesu Kristo ndiye Mkombozi wa wanadamu wote.

Hatungekuwa na sababu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo kama dhabihu Yake ya Upatanisho haingefanyika, ambayo kupitia kwayo Anatuokoa kutoka dhambi na kifo, anatufariji katika mateso, na anatusaidia “kukamilishwa ndani Yake” (Moroni 10:32). Umejifunza nini kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni mwaka huu kuhusu uwezo wa Mwokozi wa kukukomboa? Kuna hadithi zozote au mafundisho yanayojitokeza kwako ? Fikiria kile mifano ifuatayo inakufundisha kuhusu misheni ya ukombozi wa Mwokozi: 2 Nefi 2:6; Alma 7:7–13; 11:40; na Helamani 5:9; 14:16–17. Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kumwonyesha shukrani zako?? (Christmas.ComeUntoChrist.org ina mawazo ambayo yanayoweza kukusaidia kuanza.)

1 Nefi 6:4; 19:18; 2 Nefi 25:23, 26; 33:4, 10

Kitabu cha Mormoni kinashuhudia juu ya Yesu Kristo.

“Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo” ni zaidi ya kichwa kidogo cha habari cha Kitabu cha Mormoni; ni kauli ya lengo lake takatifu. Tafakari kile unachojifunza kutokana na maandiko yafutayo kuhusu misheni ya Kitabu cha Mormoni kushuhudia kuhusu Kristo: 1 Nefi 6:4; 19:18; na 2 Nefi 25:23, 26; 33:4, 10.

Fikiria kuandika katika shajara jinsi kujifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu kulivyokuleta karibu zaidi na Kristo. Mapendekezo yafuatayo yanaweza kukushawishi:

  • Kitu kipya ambacho nilijifunza kuhusu Mwokozi mwaka huu kilikuwa ni …”

  • “Kusoma [aya kuhusu Mwokozi] kulibadili jinsi nilivyo …”

  • “Mtu ninayempenda sana [au hadithi] katika Kitabu cha Mormoni ilinifundisha kwamba Mwokozi …”

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

1 Nefi 11:13–23; Mosia 3:5–10; Helamani 14:1–13; 3 Nefi 1:4–22

Watoto wanaweza kufurahia kuchora picha za kile wanachosikia unaposoma hadithi za kuzaliwa kwa Kristo na misheni Yake katika 1 Nefi 11:13–23; Mosia 3:5–10; Helamani 14:1–13; na 3 Nefi 1:4–22. Kisha watoto wenu wanaweza kukariri tena hadithi hizo wakitumia picha ambazo wamechora.

“Yeye Ndiye Zawadi”

Ili kuisaidia familia yako kufokasi juu ya zawadi ambayo Baba wa Mbinguni alitupatia kwa kumtuma Mwana Wake, unaweza kuifunga picha ya Yesu Kristo kama Zawadi ya Krismasi. Wanafamilia wanaweza kuzungumza kuhusu zawadi za Krismasi walizozipenda zaidi ambazo wamepokea au wanazotumaini kupokea. Kisha wanaweza kuifungua picha ya Kristo na kujadiliana jinsi ambavyo Amekua zawadi ya thamani kubwa kwetu sisi. Video “He Is the Gift” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kuwasaidia kujadili jinsi mnavyoweza kugundua, kukubali, na kushiriki zawadi ya Mwokozi kama familia Krismasi hii.

Familia yako pia inaweza kunufaika kutokana na kufikiria kuhusu “zawadi” ambayo wangependa kumpa Mwokozi, kama vile kufanya juhudi kuwa mpole kwa wengine au kufanya juhudi kushinda tabia mbaya . Fikiria kuwaalika wanafamilia kuandika mawazo yao, wayafunge kama zawadi, na kuziweka zawadi zao kuzunguka picha ya Mwokozi.

Roho ya Krismasi

Inaweza kufurahisha mno kupanga shughuli ambazo familia yako inaweza kufanya katika siku zinazoelekea kufikia Krismasi ili kuhisi Roho wa Kristo, kama vile kumhudumia mtu fulani au kuimba nyimbo za Krismasi pamoja. (Kwa ajili ya mawazo, ona christmas.ComeUntoChrist.org.)

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia Mialiko ya Kutenda. Wakati unapofuatilia mwaliko wa kutenda, wewe unawaonyesha [wanafamilia wako] kwamba unawajali na jinsi gani injili inabariki maisha yao. Pia unawapa wao nafasi ya kuelezea uzoefu wao, ambao huimarisha kujitolea kwao na huwapa fursa ya kusaidiana katika kuishi injili” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,35).

Picha
malaika akimuonyesha Nefi Bikira Mariamu katika ono

Ono la Nefi Juu ya Bikira Mariamu, na Judith A. Mehr

Chapisha