“Desemba 21–27. Krismasi: Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Desemba 21–27. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Desemba 21–27
Krismasi
“Atakuja Duniani Kuwakomboa Watu Wake”
Watoto kwa kawaida wana hamu ya kuzungumza kuhusu jinsi wanavyosherehekea Krismasi. Tafakari nini unachoweza kufanya kuwasaidia kufokasi kwa Yesu Kristo na shukrani zao kwa kuzaliwa Kwake.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike watoto kusimulia au kuchora picha ya jambo ambalo familia zao hufanya wakati wa Krismasi ili kuwasaidia kumkumbuka Yesu Kristo.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
1 Nefi 11:13–22; Mosia 3:5–8; Alma 7:9–13; Helamani 14:1–6; 3 Nefi 1:15, 19–21
Yesu Kristo alizaliwa kuwa Mwokozi wangu.
Je, watoto unaowafundisha wanajua kwa nini tunasherehekea Krismasi? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuelewa kwa nini kuzaliwa kwa Yesu ni sababu ya kusherehekea kwetu?
Shughuli za Yakini
-
Simulia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu, ukionyesha picha wakati ukisimulia (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 28, 29, 30, 31). Waruhusu watoto washiriki kile wanachokijua. Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwafundisha watoto kwamba watu walioishi nyakati za Kitabu cha Mormoni walijua kuhusu kuzaliwa kwa Yesu.
-
Soma vifungu vya maneno muhimu kutoka Alma 7:11–12 ili kuwafundisha watoto kile Yesu Kristo alichotufanyia. Shiriki kwa nini una shukrani kwamba Yesu Kristo alizaliwa, na elezea hisia zako kuhusu dhabihu ya upatanisho Wake.
-
Onyesha picha zinazoelezea dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi—kama vile mateso Yake katika Gethsemane, kifo Chake msalabani, na Ufufuo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56, 57, 58, 59). Waombe watoto wakuambie kile wanachoona katika picha. Wasaidie kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni alimtuma Yesu Kristo duniani kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu, kufa kwa ajili yetu, na kufufuka ili kwamba tuweze kurudi kuishi pamoja Naye.
-
Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu kuzaliwa kwa Yesu, kama vile “He Sent His Son” au “Away in a Manger” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35, 42–43). Waonyeshe watoto vifungu vya maneno katika wimbo ambavyo vinaelezea baraka tulizonazo kwa sababu ya kuzaliwa kwa Yesu.
Kitabu cha Mormoni kinashuhudia juu ya Yesu Kristo.
Unapohitimisha usomaji wako wa Kitabu cha Mormoni mwaka huu, wakumbushe watoto kwamba kitabu hiki ni “Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo,” ulioandikwa kutusaidia kuja Kwake.
Shughuli za Yakini
-
Inua juu nakala ya Kitabu cha Mormoni, kwa ajili ya watoto kukiona. Soma kichwa cha habari na onyesha maneno “Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo.” Waruhusu watoto wafanye zamu kukishikilia kitabu, na wasaidie kutafuta jina la Mwokozi juu ya jalada. Waambie watoto jinsi unavyohisi kuhusu Kitabu cha Mormoni na jinsi kilivyokusaidia kujifunza kuhusu Yesu Kristo.
-
Mpe kila mtoto picha ya Yesu, au waache wachore picha zao wenyewe za Yesu. Waalike kunyanyua juu picha zao kila mara wanaposikia jina la Kristo wakati unaposoma 2 Nefi 25:23, 26. Shuhudia kwamba Kitabu cha Mormoni kiliandikwa ili kutusaidia “kumwamini Kristo” (2 Nefi 25:23).
-
Shiriki na watoto moja ya aya unazozipenda au hadithi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambayo inakusaidia kujifunza kuhusu Yesu Kristo. Waulize watoto kuhusu hadithi wanazozipenda ndani ya Kitabu cha Mormoni, na wasaidie kuona jinsi hadithi hizi zinavyotusaidia kujifunza kuhusu Mwokozi na kuja karibu Naye. Kuangalia baadhi ya picha katika Hadithi za Kitabu cha Mormoni kungeweza kuwasaidia kukumbuka hadithi.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
1 Nefi 11:13–22; Mosia 3:5–8; Alma 7:10–13; Helamani 14:1–6; 3 Nefi 1:15, 19–21
Yesu Kristo alizaliwa kuwa Mwokozi wangu.
Tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia vizuri zaidi watoto kuelewa umuhimu wa kuzaliwa kwa Kristo na kile inachomaanisha kwao.
Shughuli za Yakini
-
Mpe kila mtoto moja ya rejeleo la maandiko linalopatikana kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waalike kila mmoja kusoma maandiko yao, kutambulisha nabii aliyekuwa akizungumza, na kushiriki jambo moja ambalo nabii huyu alijua kuhusu Yesu Kristo. Wape msaada au waruhusu kushirikiana kama itahitajika.
-
Orodhesha ubaoni baadhi ya matukio yanayozunguka kuzaliwa kwa Yesu, kama ilivyoelezewa katika Luka 2:4–14; Mathayo 2:1–2; na 3 Nefi 1:15, 19–21. Wasaidie watoto kutafuta maandiko haya ili kubainisha ikiwa matukio yalitukia Bethlehemu, Amerika, au kote. Kwa nini tuna shukrani kuwa na Kitabu cha Mormoni kama ushahidi wa pili wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo na kazi yake kama Mwokozi?
-
Soma Alma 7:10–13 pamoja na watoto. Je, tunajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu? Kuhusu utakatifu Wake? Kuhusu kazi Yake duniani? Waalike watoto washiriki ni kwa nini wana shukrani kwa ajili ya Yesu Kristo, na shiriki ushuhuda wako kuhusu Yeye.
Kitabu cha Mormoni kinashuhudia juu ya Yesu Kristo.
Akizungumzia kuhusu Kitabu cha Mormoni, Nabii Joseph Smith alisema kwamba “mwanadamu angemkaribia Mungu zaidi kwa kufuata mafunzo yake, zaidi ya kitabu kingine” (dibaji ya Kitabu cha Mormoni). Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa ahadi hii?
Shughuli za Yakini
-
Toa moja ya mistari ifuatayo kwa kila mtoto: 2 Nefi 25:23, 26; 33:4, 10. Waalike watoto kusoma mstari wao na kuonyesha kile ambacho nabii wa Kitabu cha Mormoni Nefi alitaka sisi tujue. Waombe waandike kile wanachokipata ubaoni. Elezea kwamba mambo haya yanaelezea lengo muhimu la Kitabu cha Mormoni. Waruhusu watoto waigize wao kwa wao jinsi ambavyo wangeelezea kwa rafiki lengo muhimu la Kitabu cha Mormoni.
-
Shiriki na watoto moja ya aya unazozipenda au hadithi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambayo inakusaidia kujifunza kuhusu Yesu Kristo. Waulize watoto kuhusu hadithi wanazozipenda ndani ya Kitabu cha Mormoni, na wasaidie kuona jinsi hadithi hizi zinavyotusaidia kujifunza kuhusu Mwokozi na kuja karibu Naye. Shiriki na watoto jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyokusaidia kujua kwamba Yesu ndiye Kristo. Wahimize watoto kufikiria mstari au hadithi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambayo inaimarisha imani yao katika Yesu Kristo. Waombe washiriki mstari au hadithi hiyo na rafiki au mwanafamilia ambaye hajui kuhusu Kitabu cha Mormoni.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki pamoja na familia zao jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyowasaidia kujifunza zaidi kuhusu Kristo. Wahimize kushiriki mstari au hadithi kutoka katika Kitabu cha Mormoni kama sehemu ya ushuhuda wao.