“Desemba 14–20. Moroni 10: ‘Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe ndani Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Desemba 14–20. Moroni 10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Desemba 14–20
Moroni 10
“Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe ndani Yake”
Baadhi ya watoto darasani kwako wanaweza kuwa na uzoefu wenye maana wa kujifunza kutoka katika Kitabu cha Mormoni nyumbani. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia uzoefu huo kuwahimiza watoto wote kusoma maandiko nyumbani?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Pitisha nakala ya Kitabu cha Mormoni. Pale kila mtoto anaposhikilia kitabu, muombe kushiriki jambo analolipenda kuhusu Kitabu cha Mormoni—hadithi anayoipenda, ushuhuda, au uzoefu wa kujifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni nyumbani au Kanisani.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninaweza kujua mimi binafsi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.
Tafuta njia za kuwasaidia watoto kukubali mwaliko wa Moroni wa kumuuliza Mungu ikiwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya Moroni akizika bamba za dhahabu (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia), na waombe watoto kuelezea kile wanachoona. Waalike kuonyesha bamba, na elezea kwamba kwenye bamba hizi kuliandikwa maneno ambayo sasa tunayasoma katika Kitabu cha Mormoni. Acha watoto wajifanye kuwa Moroni akiandika kwenye bamba na kuzizika. Imbeni pamoja “The Golden Plates” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 86).
-
Onyesha Kitabu cha Mormoni na soma Moroni 10:4. Sisitiza kwamba tunaweza kumuuliza Mungu ikiwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli, na Yeye atatuma Roho Mtakatifu kutushuhudia. Ungeweza pia kutumia “Mlango wa 54: Ahadi ya Kitabu cha Mormoni” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni,156, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org). Shiriki jinsi Roho Mtakatifu alivyokusaidia kupata ushuhuda wako wa Kitabu cha Mormoni. Wasaidie watoto kuelewa vile ushahidi kutoka kwa Roho unavyokuwa. Imba wimbo kuhusu kutafuta ukweli, kama vile “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109).
Baba wa Mbinguni hunipa karama za kiroho.
Moroni alielezea karama ambazo Mungu hutoa kwa watoto Wake pale wanapokuwa na imani Kwake. Unaweza kuwasaidia watoto kuwa na imani kwamba Mungu atawapa karama za kiroho.
Shughuli za Yakini
-
Andika namba, 9 mpaka 16 kwenye vipande tofauti vya karatasi, na ufunge kila karatasi kama zawadi. Acha watoto wafanye zamu kufungua zawadi. Wanapofanya hivyo, someni pamoja mistari kutoka Moroni 10:9–16 ambayo inahusiana na namba, na wasaidie watoto kutambua kila karama ya kiroho. Elezea kwamba hizi ni karama ambazo Baba wa Mbinguni huwapa watoto Wake ili tuweze kusaidiana kila mmoja na kuifanya kazi Yake.
-
Waruhusu watoto kuzungumza kwa ufupi kuhusu zawadi wanayoipenda ambayo wamewahi kupokea. Waambie watoto kuhusu karama za kiroho ambazo umegundua Baba wa Mbinguni amewapatia wao, kama vile, karama ya imani, hekima, ushuhuda, ukarimu, na uwezo wa kujifunza.
Yesu Kristo anataka nije Kwake.
Fikiria jinsi utakavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa kile inachomaanisha “kuja kwa Kristo.”
Shughuli za Yakini
-
Wasomee watoto kutoka Moroni 10:32, “Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe ndani Yake,” na waalike watoto kurudia kifungu cha maneno pamoja nawe. Waombe wafumbe macho yao wakati ukiweka picha ya Yesu mahali fulani katika chumba. Kisha waruhusu wafumbue macho yao, watafute picha, na kukusanyika kuizunguka. Jadili pamoja na watoto jinsi tunavyoweza kuja kwa Kristo (ona, kwa mfano, Makala ya Imani 1:3–4). Rudia shughuli hii, ukiwaruhusu watoto kuweka picha mahala fulani darasani.
-
Wasaidie watoto kupamba beji zenye umbo la moyo zinazosema “Nampenda Mungu kwa uwezo wangu wote, akili zangu zote, na nguvu zangu zote” (ona Moroni 10:32. Ni kwa jinsi gani tunamwonyesha Mungu kwamba tunampenda Yeye?
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kujua ukweli kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Mungu anataka kila mmoja wetu ajue kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Wasaidie watoto kuelewa ahadi ya Mungu ya “kuonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”
Shughuli za Yakini
-
Andika ubaoni maneno Soma, Kumbuka, Tafakari, na Omba. Waalike watoto kutafuta maneno haya katika Moroni 10:3–4. Ni nini tunapaswa kusoma, kukumbuka, kutafakari, na kuomba ili kupata au kuimarisha shuhuda zetu za Kitabu cha Mormoni? Waombe watoto watafute mfanano kati ya mistari hii na wimbo “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109).
-
Wasaidie watoto kukumbuka baadhi ya uzoefu ambao mmekuwa nao kwa pamoja katika kujifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni. Shiriki hisia zako kuhusu Kitabu cha Mormoni, ikijumuisha jinsi ulivyopata au kuimarisha ushuhuda wako kwamba ni cha kweli. Waalike watoto kushiriki hisia na shuhuda zao.
-
Simulia kuhusu wakati ambapo Roho Mtakatifu alikushuhudia kuhusu jambo fulani. Elezea jinsi ulivyohisi na jinsi ulivyojua kwamba alikuwa ni Roho Mtakatifu. Wasaidie watoto kujifunza kutoka kwenye maandiko yafuatayo kuhusu jinsi Roho anavyozungumza nasi: Yohana 14:26–27; Mafundisho na Maagano 6:15, 23; 8:2–3; 9:7–9; 11:12–14.
Baba wa Mbinguni hunipa karama za kiroho.
Kuna wengi katika siku yetu ambao “wanakataa … karama za Mungu” (Moroni 10:8). Wasaidie watoto kuona kwamba karama hizi bado zipo leo.
Shughuli za Yakini
-
Andika karama zilizotajwa katika Moroni 10:9–16 kwenye vipande vya karatasi, na ziweke ndani ya boksi la zawadi. Andika namba 9 mpaka 16 ubaoni, na waalike watoto kufanya zamu kuchukua karatasi kutoka ndani ya boksi na kuioanisha na mstari ulioko ubaoni. Nini tunajifunza kuhusu karama hizi kutoka mstari wa 8 na 17–18?
-
Shiriki hadithi ya ujio wa Kitabu cha Mormoni (ona “Mlango wa 3: Malaika Moroni na Mabamba ya Dhahabu,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 13–17). Wasaidie watoto kutambua karama zilizotajwa katika Moroni 10:9–16 ambazo Mungu alimpa Joseph Smith ili aweze kuleta Kitabu cha Mormoni. Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka sisi kuamini katika karama za kiroho leo?
Yesu Kristo anataka nije Kwake.
Ni kwa jinsi gani utawaalika watoto “kuja kwa Kristo, na kukamilishwa ndani Yake”?
Shughuli za Yakini
-
Andika ubaoni maswali kama inamaanisha nini kuja kwa Kristo? Wasaidie watoto kutafuta Moroni 10:32–33 ili kupata majibu yanayowezekana. Shirikianeni kuorodhesha kile Kristo anachotaka tufanye na kile Yeye anachoahidi kufanya kwa ajili yetu.
-
Shiriki vifungu vya maneno au hadithi unazozipenda kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni ambazo zimekusaidia kuja kwa Kristo, na waalike watoto kufanya vivyo hivyo. Rejea pamoja na watoto maneno ya Joseph Smith kutoka kwenye dibaji ya Kitabu cha Mormoni: “Mtu angeweza kumkaribia zaidi Mungu kwa kuzingatia mwongozo wa [Kitabu cha Mormoni], kuliko kitabu kingine chochote.” Shiriki ushuhuda wako wa jinsi hii ilivyotokea katika maisha yako
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kusali kwa ajili ya ushuhuda imara wa Kitabu cha Mormoni na kisha kushiriki shuhuda zao pamoja na mwanafamilia au rafiki.